Tulipokuwa primary,unakumbuka?

Du! You have made my day amazing!
 

Ninyi mlikuwa mjini na maendeleo yalikuwepo. Kwetu miaka hiyo 1984-1990 kijijini kuvaa kiatu ni neema ya ajabu, wengi tulitinga shule pekupeku hadi darasa la sita ndio wengi wanapata kutia kiatu mguuni. Hata hivyo ilikuwa lazima kuhakikisha visigino vyako havina nyufa, vinginevyo fito kila siku halali yako...habari ya mwalimu kununua gari enzi hizo inaashiria 'ujasiriamali' wa hali ya juu maana hata leo walimu wa shule ya msingi ni wachache wanaweza kumudu kununua na kuhudumia gari!
 
Mkuu nakukumbusha tu japo Mimi ni wa enzi za mwinyi kwenye English alikuwa Neema ,Musa and Baraka namkumbuka Neema kwa kuibiwa kikapu sokoni tukiwa darasa la sita pia nakumbuka Baraka alipomshauri baba yake waanzishe mradi wa ufugaji wa Kuku ili jogoo wakiwika wamwamushe awahi shule
 
aisee ni unakumbuka "CHOPEKO NA MNOFU"?? HESABU ZA KIKWETU nilikua noma sana aisee kulikua hakuna swali linalonishinda,ila naona mtaani kitabu kilichotupa msingi wa kujua kusoma wengi wetu enzi hizo "SOMA KWA HATUA" nakumbuka enzi hizo mwalimu wa darasa la kwanza lazima awe bibi,sio siku izi mwalimu hajui ata uchungu wa mtoto upo vipi bana!!!! nimekumbuka mbali sana wacha tu nilie.mimi
 
Hakika ya kale ni dhaabu, ki ukweli ukiusoma uzi huu lazima ulengwe na machozi pia lazima ucheke sana kwa furah, vilevile lazima upatwe na hisia kali za kuyatamani yaliyopita. Kwa kizazi cha leo hawawezi kujua lulu ya yaliyo andikwa hapa ila wale wa zamani wanajua. Mambo yanavyoenda sasa hivi katika sekta ya elimu ni tofautu sana. Zamani tulifundishwa mambo ya kizalendo, mtu kujitambua, heshima na kujua kuwa unadeni katika jamii na taifa, lakini leo vitabu vimevurugwa hadi kero. My God ! Watoto wetu nani atawaonesha njia?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…