Avanti
JF-Expert Member
- Aug 24, 2010
- 1,209
- 239
Du! You have made my day amazing!Hahahahahaaaaa, duh wakuu mmenikumbusha mbali sana, tulikuwa tukiwahi namba na endapo una mshkaji wako kachelewa unamuwekea jiwe au dumu la maji kwenye mstari ikiwa ni ishara kuwa kuna mtu, hlf Jumatatu na Alhamis ilikuwa ni ukaguzi, kuna mwalimu alikuwa na ruler ya mbao kwenye ukaguzi yeye alikuwa anapenda kutazama kucha tu, akikukuta na kucha ndefu unakula ruler za vidoleni sita! Hlf uniform ilikuwa ni viatu vyeusi au brown tu! Hahahaaaaa, ikifika wakati wa kuingia darasani baada ya assembly kuna band inapiga kama gwaride la jeshi vile! Hlf watoto wa kihindi na kiarabu ndo walikuwa matajiri zetu mida ya break, anakununulia mihogo ya kukaanga na visheti ili umpe ulinzi kwa wababe wa shule au umpange kwenye timu ya darasa! Duh it was sooo funny, I really miss those great great moments, hlf kuna mwalimu mkuu alinunua gari yake Land rover alikuwa akipaki chini ya mwembe karibu na assembly, hataki mtu aiguse, ukiigusa tu unakwenda kusafisha vyoo ambavyo vilikuwa vichafu balaa, alikuwa akiitwa Mwalimu Sitta, hiyo ilikuwa ni experience ya Lake Primary huko Mwanza! Miaka ya 86- 92!