Mkuu IDIMI nashukuru sana mzee kwa information hizi, kwa kweli nimekumbuka mbali sana na najihisi hata machozi kunidondoka mtu wangu.
Nilikuwa dogo enzi hizo napiga soka balaa, begi kubwa mgongoni ndani madaftari kibao,Kuhusu ile Stori ya Twende Tukawinde ,nimeikumbuka majamaa wameenda kuwinda ngedere ,dingi kabeba gobore, dada yao kawaandalia
Mabumunda. katika hiyo stori nakumbuka jamaa alivyokuwa akilalamika kwa machungu jinsi ngedere wanavyomaliza mazao shambani, nanukuu "Ni nani aliyekula Matango yetu?, huyu atakuwa ni Mnyonyaji".
Umenikumbusha tena kuhusu sikiri na Sadiki
Sadiki sasa ashiba
Chakula kingi kwa baba
Nirudi tena kwa baba
Nakufa hapa kwa nini?
Halafu kuhusiana Na Bendera ya Tanzania
kulikuwa na shairi pia, nakumbuka ubeti mmoja
wakoloni walifika,huku na dharau zao
Kudharau Afrika,kutukuza nchi zao
Sasa wanaaibika, hawana tena kikao
..........................,,,,>
Pia kitabu hiki kilikuwa na shairi la kuukaribisha mwenge, kama kuna mtu analikumbuka basi si vibaya akatukumbusha
Nakumbuka kidoogo kuhusiana na shairi hili
Twakukaribisha Mwenge
Mgeni wetu uringe
na wenyeji tukupambe
Huku tukishangiria!
Idimi unaikumbuka ngonjera ya(mimi nimeikumbuka kwa mbaali,nadhani nitakuwa nimekosea ila najaribu kuvuta feeling)
Dada Asha sikilza
Maneno ya kupendeza
Azimio la Arusha
Lilizaliwa Arusha
Arusha unaitaja
sijui inavyokuja
Azimio la arusha
Azimio kitu gani?