Semester10 za wababe wachache hiziNilipata Sup ya kibabe semester ya 10, tulikua wawili tu Mimi na shori Fulani, tuliichomoa kibabe, kwa sasa mambo ni mazuri kabisa mahusiano yameimarika.
Wewe itakuwa IFM au TIA Business law huwa inakamata wengi sanaNilipata supp ya business law first year nkachomoa chaap ..nkapata supp ya audit second year third year management chupu chupu nidakwe wakatuongezea marks nikaponea mdomoni ...aisee Supp n tamu san kama unazijulia !disccssn za supp mnakutana wote vilaza mnaelekezana ad raha , ambao hawajawai pata supp nadhan kuna k2 kama wamekikosa sana ktk elimu ya chuo
Supp 7 hiyo disco mkuuNishawahi pata supp 7 mwaka wa pili na nikatoboa, vita ni vita haijalishi unaipigana vipi!. Komaa! (ila siwasahau waalim wa FA, OP na FM
Kama wewe unasomea uhandisi na hujawahi pata supp huo ni umama!!!
wale wa UDSM COET sitamsahau Prof Chambega second year ile shule ilijua kuninyoosha hakuna pakushika miti yoote inateleza first year gpa ya 4 second year gpa 2.8 na sup juu nilinyooka aisee....Chambega popote ulipo mzee wa Electrical analysis shkaoooo
kumbe DIT mna haki kuwa hivyo!.. Dogo wangu anasoma hapo telecom techs nilimwambia aache ubishoo!...Asee watu mmesoma kwa raha yaan semister 1 masomo 6?? Sie semister ikiwa na masomo machache ni 9 tena hio semister inakuwa ya bata hatari bt mostly semister ilikuwa na modules 12 mpka 13 so kwa mwaka ni modules 24 &26 kwhyo kukuta watu wana sup zaidi ya 10 ilokuwa kawaida sana... shkamoo wana DIT alumn
Kitu aina moja ni KIPINDI CHA MITIHANI YA SUPP sema majina yanatofautiana kwa vyuo!..Hivi hiyo SeptConf iko CBE tu au na vyuo vingine ?
Hapo sawa maana mimi nilikosoma sijawahi kusikia hilo jina. Asante sana bro kwa ufafanuzi mzuri.Kitu aina moja ni KIPINDI CHA MITIHANI YA SUPP sema majina yanatofautiana kwa vyuo!..
kwa chuo nilichosoma Supp 8 umeenda na maji, 7 bado upo relini!.Supp 7 hiyo disco mkuu
Nachokuonea huruma ni kwamba umemaliza/utamaliza chuo halafu sisi vilaza tutakuajiri kurekebisha mitambo yetu kwa rousse ya kimshahara 'DONGE NONO' ukisahau we will remain your boss!..Chuo gani hicho mkuu? CBE ama TEKU? naomba ukitaje nisije nikamruhusu mwanangu kukisoma.
Hahaaaa...kuliwa kubaya!!Nilipataga supp moja third year semester ya Mwisho.. Ilikua supp ya Audit. Nilipata stress maana naogopa Sana shule halafu miaka yote nimecheza mwaka wa tatu ndo nikala supp halafu sijui naichomoaje.
Uzuri ni kwamba ile supp tulipata karibia 75% ya tuliokua tunasoma hilo somo. Kuna mkaka nakumbuka alikuaga anafundisha review classes za CPA nae akashikwa kwenye supp.
Kuna mwalimu alikua anataka kunizoea sasa alivyojua Nina supp akataka kutumia chance anile halafu akaniombee kwa mwalimu mwenzie kwenye supp nichomoke. Nikamwambia Niko radhi kurudia mwaka ila sio kubadilishana mwili wangu Na supp. Nikajiapiza kutoomba msaada kwa mwalimu yoyote yule nitaifanya supp Na nitachomoa.
Siku ya kwenda kufanya supp Na nilivyo Na allergy Na masomo ya kuandika niliandika nilivyochoka nikabeba vitu vyangu nikakusanya pepa nikaondoka. Nikampigia bf wangu kumtaarifu mwakani narudia mwaka maana sina uhakika wa kufaulu. Hapo nimetoka kwenye pepa hata lisaa halijaisha.
Japo nilishazoeleka kutoka wa kwanza kwenye mitihani huu walijua imekula kwangu maana ulikua ngumu hatari. Nashukuru Mungu nilipita salama maana ile supp hata nikilala nilikua naiota. Nikawa nawauliza rafiki zangu ambao hamna semester inapita hawajahudhurua September Conference waliwezaje kukaa kwa amani wakati wakiwa Na supp mbili Na zaidi maana Mimi moja tu ilinikondesha
Mimi kozi ikiwa haina hesabu alafu iwe na essay nilikua napata tabu sana... Hesabu is sweet, cool and fun!!Sijawahi kutana na Commercial Arithmetic nikapona bila ya supp aisee
Naichukia sana hesabu