Tuliowai kupata Supplemental kwenye final exam za UE/IE tukutane hapa

Taarifa za mitihani yote ya msingi, sekondari na vyuo huwa tunasikia leo inaanza tuwaombee. Ila hizi ratiba za supp huwa hatuzisikii na watu hawahiataji maombi. Sasa wote wanaofanya supp ni watakatifu huwa hawahitaji maombi? Na kwa nini inakuwa siri kuliko nyeti?
 
Nilipata supp ya business law first year nkachomoa chaap ..nkapata supp ya audit second year third year management chupu chupu nidakwe wakatuongezea marks nikaponea mdomoni ...aisee Supp n tamu san kama unazijulia !disccssn za supp mnakutana wote vilaza mnaelekezana ad raha , ambao hawajawai pata supp nadhan kuna k2 kama wamekikosa sana ktk elimu ya chuo
Wewe itakuwa IFM au TIA Business law huwa inakamata wengi sana
 
wale wa UDSM COET sitamsahau Prof Chambega second year ile shule ilijua kuninyoosha hakuna pakushika miti yoote inateleza first year gpa ya 4 second year gpa 2.8 na sup juu nilinyooka aisee....Chambega popote ulipo mzee wa Electrical analysis shkaoooo
 
Sem1 nilifeli Networking

Sikufeli tena hadi namaliza chuo
 
wale wa UDSM COET sitamsahau Prof Chambega second year ile shule ilijua kuninyoosha hakuna pakushika miti yoote inateleza first year gpa ya 4 second year gpa 2.8 na sup juu nilinyooka aisee....Chambega popote ulipo mzee wa Electrical analysis shkaoooo

Chambega na mkumbuka sana katika somo lake la DESIGN OF ELECTRICAL MACHINE .....


Maswali mengine nisiulizwe sababu sitajibu.....
 
Asee watu mmesoma kwa raha yaan semister 1 masomo 6?? Sie semister ikiwa na masomo machache ni 9 tena hio semister inakuwa ya bata hatari bt mostly semister ilikuwa na modules 12 mpka 13 so kwa mwaka ni modules 24 &26 kwhyo kukuta watu wana sup zaidi ya 10 ilokuwa kawaida sana... shkamoo wana DIT alumn
kumbe DIT mna haki kuwa hivyo!.. Dogo wangu anasoma hapo telecom techs nilimwambia aache ubishoo!...
Sisi wafanyabiashara kutujazia masomo mengi unataka tugundue kipi kipya!?:)
 
Kitu aina moja ni KIPINDI CHA MITIHANI YA SUPP sema majina yanatofautiana kwa vyuo!..
Hapo sawa maana mimi nilikosoma sijawahi kusikia hilo jina. Asante sana bro kwa ufafanuzi mzuri.
 
Chuo gani hicho mkuu? CBE ama TEKU? naomba ukitaje nisije nikamruhusu mwanangu kukisoma.
Nachokuonea huruma ni kwamba umemaliza/utamaliza chuo halafu sisi vilaza tutakuajiri kurekebisha mitambo yetu kwa rousse ya kimshahara 'DONGE NONO' ukisahau we will remain your boss!..
ACHA DHARAU!
 
Nilipataga supp moja third year semester ya Mwisho.. Ilikua supp ya Audit. Nilipata stress maana naogopa Sana shule halafu miaka yote nimecheza mwaka wa tatu ndo nikala supp halafu sijui naichomoaje.
Uzuri ni kwamba ile supp tulipata karibia 75% ya tuliokua tunasoma hilo somo. Kuna mkaka nakumbuka alikuaga anafundisha review classes za CPA nae akashikwa kwenye supp.
Kuna mwalimu alikua anataka kunizoea sasa alivyojua Nina supp akataka kutumia chance anile halafu akaniombee kwa mwalimu mwenzie kwenye supp nichomoke. Nikamwambia Niko radhi kurudia mwaka ila sio kubadilishana mwili wangu Na supp. Nikajiapiza kutoomba msaada kwa mwalimu yoyote yule nitaifanya supp Na nitachomoa.
Siku ya kwenda kufanya supp Na nilivyo Na allergy Na masomo ya kuandika niliandika nilivyochoka nikabeba vitu vyangu nikakusanya pepa nikaondoka. Nikampigia bf wangu kumtaarifu mwakani narudia mwaka maana sina uhakika wa kufaulu. Hapo nimetoka kwenye pepa hata lisaa halijaisha.
Japo nilishazoeleka kutoka wa kwanza kwenye mitihani huu walijua imekula kwangu maana ulikua ngumu hatari. Nashukuru Mungu nilipita salama maana ile supp hata nikilala nilikua naiota. Nikawa nawauliza rafiki zangu ambao hamna semester inapita hawajahudhurua September Conference waliwezaje kukaa kwa amani wakati wakiwa Na supp mbili Na zaidi maana Mimi moja tu ilinikondesha
Hahaaaa...kuliwa kubaya!!
 
Mh huu uzi haunihusu , maana hata sijaelewa kinachoongelewa.
Sijui kwa nini nilikula ada
 
Back
Top Bottom