Tuliowahi kuwaona Marais wote watano kwa macho tukutane hapa. Taja na maeneo uliyomuonea

Sisi wengine tumeshawaona hadi kero, maana ndio tunaowapelekea vitabu vya Memorandom ili wasaini wanapoingia maeneo mbalimbali, ila tu hatupendi show-off.
 
Wakati nipo mtoto mdogo mwaka 1969 nilibebwa na J.K. Nyerere pale wilayani Kilosa Morogoro na kama sikosei mwaka 1975 Tulisalimiana naye kwa kupeana mkono pale Mikumi National Park akiwa anampokea rais Sianok wa Chekv. Pia nimewahi kumuona rais Alli Hassan Mwinyi akifungua kiwanda cha samaki Mwanza, marais waliofuata sijawahi kuwaona kwa live.
Shikamoo mzee wangu..!
 
1. Mwalimu Julius K. Nyerere.
Barabara ya uhuru enzi hizo akitokea airport.


2. Mzee Ali Hassan Mwinyi.
Nimemuona kwa ukaribu kabisa akiwa raisi JMT na ata mkono nimemshika.


4. Jakaya Mrisho Kikwete.
Nimemuona kwa ukaribu kabisa akiwa raisi wa JMT na ata mkono nimemshika.
 
Nyerere, mkapa na kikwete niliwaona laivu kwenye ishu za kampeni. Mwinyi nilimuona na mkewe mama siti siku wanaaga na kurudi zenji baada ya uraisi wake kuisha.huyu maza alikuwa chuma sana enzi zake. magu bado sijamuona laivu.
 
1. J. K. Nyerere - Kwenye Tv, YouTube na magazeti.

2. A. H. Mwinyi - Kwenye TV na magazeti.

3. B. W. Mkapa - Kwenye TV, YouTube na magazeti.

4. J. M. Kikwete - Mkutano wa kampeni 2005, Tv, YouTube na magazeti.

5. J. P. Magufuli - Kwenye Tv, YouTube na magazeti.
Jamaa tumefanana aiseeeee, hata mimi nimemuona kikwete tu kwenye kampeni za mwaka 2005 wilaya ya Magu.
 
Badala useme nani kamuona yesu ana kwa Ana kupitia Makubwa anayomtendea unasema binadamu kama wewe?
 
Sio kuwaona tu,hadi kula nao gambe nimekula nao wote tena huyu wa sasa juzi juzi tu kule............................
 
1. Mwalimu Julius K. Nyerere.

Nilimuona kwa macho yangu mwaka 1990 wakati Mandela alipokuja Tanzania.

2. Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Mwaka 1994 chuo Cha ualimu kigurunyembe.

3. Benjamin William Mkapa.

Edinburgh Scotland.
Rome Italy
Mpwapwa dodoma.

4. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mwanjelwa Mbeya.
Misungwi mwanza.
Kakonko biharamulo.
Bujumbura Burundi.
Morogoro pangawe jeshini.

5. John Joseph Pombe Magufuli.

Dodoma.
Kampala Uganda.
Arusha.

Super B.
Kwa kuuliza hivyo kuna ambao wamewaona kupitia pua?
 
Back
Top Bottom