Tuliowahi kuwa wahanga wa kufanyiwa umafia, kukodishiwa wezi au wauaji kwenye madili tukutane hapa

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Watu huwa wanasema mnyama hatari asie na huruma ni Mbwa mwitu na fisi lakini mimi niseme kwamba kuna wanadamu ni wanyama hatari kuliko kiumbe chochote

Njlifika mkoa x kukamjlisha dili la milioni kadhaa, ni mali ambayo ilibidi niifuate.

Nilipofika wenyeji wakanipeleka, niliona ni ukarimu maana hata watu wa mkoa huo ukarimu sifa yao, walionekana kufahamina na wahudumu wa lodge.

Nikiwa chumbani hapo nilipigiwa simu, aliepiga alikuwa ni jamaa flan tuliwahi kusoma wote shule moja ila ni miaka mingi ilipita, aliitafuta namba yangu kwa class mates wengine, baada ya kujuliana hali akaniambia kuwa hao jamaa ni rafiki zako au, mi nikamwambia kuna mishe tu nmekuja kupiga, ndio akanipa a-z za hao majamaa kwamba ni matapeli na majambazi, kuna mwengine nae aliwahi kuja kwa style kama yangu akalizwa. aliniambia hakutaka tuonane mwanzoni alipoona nipo nao.

Huyo jamaa nilimtoa laki 2, Usiku tukapanga niondoke hapo.

Yani hapo ilibidi niondoke kininja, nilikata umeme wa lodge kwenye circuit breka, Mlinzi akawa anawapanga wahudumu ili nipate njia ya kuchomoka bila wao kujua, nikafanikiwa kuchomoka, Teksi moja kwa moja wilaya nyingine kabisa.

Usiku nilipigiwa simu na jamaa kwamba mida ya saa tano kuna watu wanne walikuja hapo huku walioniketa wakiwa nje kwenye gari, waligonga sana hodi hadi wakafungua mlango kukuta chumba hakina mtu.

wale wa kwenye gari waliingia nao walianza kuwafokea wale wahudumu, mlinzi nae akawaambia hakuniona,

Walienda nyuma ya lodge huko, mlinzi nae akaenda kusikilizia nyuma ya ukuta basi wakawa wanaambiana kuna mtu kamuuzia huyu fara ramani, wamekosa pesa ndefu, n.k.

Kesho ndio wanapiga simu eti kwamba walikuja asubuhi lodge ila hawakunikuta,

Daah!!!
 
Last edited:
>> Moved >>
Mpaka ufikie level ya kuwa tajiri, ni lazima uwe umefanyiwa umafia hadi na wewe unakuwa mafia mkubwa.

Utajiri ni himaya, kila jicho linaiangalia himaya kwa husda. Kuna uchawi, ujambazi, figisu na michezo yote michafu.

Ukiwa tajiri utajilinda wew na uzao wako kiroho, kimwili na kitàaluma ili usipitwe na teknolojia.

Bila kuwekeza kwenye teknolojia utajiri wako utakuwa ni wa muda mfupi tu
 
Kwenye pesa binadamu tunakuwaga maadui yaani hata ndugu sio wa kumuamini muda mwingine
 
Watu huwa wanasema mnyama hatari asie na huruma ni Mbwa mwitu na fisi lakini mimi niseme kwamba kuna wanadamu ni wanyama hatari kuliko kiumbe chochote

Njlifika mkoa x kukamjlisha dili la milioni kadhaa, ni mali ambayo ilibidi niifuate.

Nilipofika wenyeji wakanipeleka, niliona ni ukarimu maana hata watu wa mkoa huo ukarimu sifa yao, walionekana kufahamina na wahudumu wa lodge.

Nikiwa chumbani hapo nilipigiwa simu, aliepiga alikuwa ni jamaa flan tuliwahi kusoma wote shule moja ila ni miaka mingi ilipita, aliitafuta namba yangu kwa class mates wengine, baada ya kujuliana hali akaniambia kuwa hao jamaa ni rafiki zako au, mi nikamwambia kuna mishe tu nmekuja kupiga, ndio akanipa a-z za hao majamaa kwamba ni matapeli na majambazi, kuna mwengine nae aliwahi kuja kwa style kama yangu akalizwa. aliniambia hakutaka tuonane mwanzoni alipoona nipo nao.

Huyo jamaa nilimtoa laki 2, Usiku tukapanga niondoke hapo.

Yani hapo ilibidi niondoke kininja, nilikata umeme wa lodge kwenye circuit breka, Mlinzi akawa anawapanga wahudumu ili nipate njia ya kuchomoka bila wao kujua, nikafanikiwa kuchomoka, Teksi moja kwa moja wilaya nyingine kabisa.

Usiku nilipigiwa simu na jamaa kwamba mida ya saa tano kuna watu wanne walikuja hapo huku walioniketa wakiwa nje kwenye gari, waligonga sana hodi hadi wakafungua mlango kukuta chumba hakina mtu.

wale wa kwenye gari waliingia nao walianza kuwafokea wale wahudumu, mlinzi nae akawaambia hakuniona,

Walienda nyuma ya lodge huko, mlinzi nae akaenda kusikilizia nyuma ya ukuta basi wakawa wanaambiana kuna mtu kamuuzia huyu fara ramani, wamekosa pesa ndefu, n.k.

Kesho ndio wanapiga simu eti kwamba walikuja asubuhi lodge ila hawakunikuta,

Daah!!!
sky soldier script nzuri saana hii kutengenezea muvi mkuu
 
Back
Top Bottom