Tuliowahi kushuhudia jamaa zetu au wenyewe kubahatika kuokota pesa na tusijue cha kufanya

Ndenji five

JF-Expert Member
Nov 1, 2021
1,985
3,083
Kuna jamaa yangu mmoja yeye alikuwa mbeba mkaa siku moja pindi anatoka kuchukua mkaa wake
Mara paa akaokota begi la pesa kiasi kama milioni 50, Hivi jamaa kuona hivyo akawa kama haelewi nini afanye basi akalifunga lile begi kwenye baiskeli yake mdogo mdogo na mkaa wake

Baada ya nusu saa akatokea padri mmoja hivi ana asili ya Uhindi yaani ni mmishonali basi akawa amesimama kwa yule mmbeba mkaa akamuuliza hili begi umetoa wapi mbeba mkaa akasema nimeokota huku ninakotoka

Yule mmishonali akaanza kumkalipia na kumtia makofi mawili matatu na kumwambia kesho uje mission nikuombee
Sikujua kufanya vile alikuwa na maana gani

Na kuna jamaa mwingine yeye alikuwa akifanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya kahawa mabosi wake walimuamini sana

Mwisho wa siku jamaa akacheza dili akatoka na begi lenye hela alitoka usiku anatembea chocho mpaka kufika kwao ni kama siku mbili hivi alipofika kwao moja kwa moja kumwita mkewe

Kufunga milango yao kuanza kuhesabu zile pesa asijue anafuatiliwa imefika limetumia tu saa moja nyumba ikazingirwa na polisi jamaa kutazama dirishani anakuta polisi kwakuwa alikuwa akicheza kareti akatokea juu ya paa ya nyumba yake maana kulikuwa na uwazi akajivilingita pale na kuwapoteza wale polisi mwenyewe hela akasema achaneni nae wakaangalia mnzigo wao wakaona uko sawa wakachukua chao wakaondoka jamaa hukugawa hata mia na anakwambia mpaka wanafika pale polisi alikuwa mahesabu milion mia nne na ujinga na hakufika hata robo ya hela asiyoihesabu

Jamaa mpaka leo hana ramani
 
True story
Una uwezo wa kuhesbu milioni 400 kwa saa tena kwa mkono mkuu?. Milioni 400 unajua ni noti ngapi za shilingi elfu kumi?, sawa na bundles ngapi za milioni kumi kumi?.

Hapo assumption ni kwamba zote zilikuwa shilingi elfu kumi kumi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom