Tuliowahi kusafiri na magari ya magazeti tukutane hapa

Ndugu zangu na rafiki zangu nawaombeni kabisa msipande hizi kitu.Nakumbuka ilikuwa mwaka 2008 nikapanda hizi gari kwenda Moshi sitosahau nimetoka dar saa 6;20 usiku saa kumi na moja kamili niko njia panda ya himo sitosahau jinsi gani nilirisk maisha yangu.Kuna rafiki yangu alipotea kwenye hizi gari maeneo ya mwanga alikuwa anawahi msiba wa mjomba wake na yeye akatangulia( RIP).Niliapa sitofanya huu ujinga tena.Nawausia maisha ni jinsi unavyopanga na kuzingatia mda usijaribu.
Aisee mwenye masikio nadhani amesikia
 
Mimi nilisafiri toka mafinga mpaka mbeya. Sitaisahau ile siku nimeshika roho juu juu tu. Yaan tulitumia saa moja na nusu tu. Gari inatembea utazan ipo angan. Siwezi panda tena gari la magazeti
Safari fupi hivyo unalalama, je ingekuwa Mbeya to Dar ?
 
Nakumbuka nilikosa bus za tunduma zinazokwenda dar pale mbeya nanenane
Basi ilibid nisogee adi uyole nikakuta hizo gari za magazet ndio zinataka kurud dar, sasa kuna fundi viatu ndio alinilengesha na nikiiangalia hzo gari yan naona kama ananitania hiv, yan gar hii nitoboe dar ila nikasema haina shda
Safar ikaanza saa 8 kamil mchana ilipigwa gia za kibabe na matrafk weng wanajuana nao so hazina kusimamishwa hzo, iv mnajua gia za kibabe,??? ikabd niwajurulshe ndugu jamaa na marafik wenye mioyo migum kwamba nipo safarin lakn gar ya magazet lolote litakalo tokea wakubaliane na matokeo
Tunafika maeneo ya kibaha kuna mzee alikua karibu yangu ananiambia apo wamepunguza speed, uwakute wanapeleka mzigo
Dar ubungo sheli tunaingia saa 3:30 usku, waliopanda bus saa 12 asubuhi waliniacha masaa mawil iv

Na nilipiga calculation zangu, saa 1 asubuh magazet yanasomwa mbeya sasa jiulize uku dar yanavyotoka saa 6 usiku yanaenda speed gan??
Niliapa hiz gar sipand tena ata nikikutwa na umaut ntaacha wosia huo
 
Rafiki yangu wa utotoni/ndugu yangu ni dereva wa haya magari,nimeshagomaga kuyapanda kabisa,huwa anakimbia sana sana
 
mmmh sitakuja kupanda tena ilitokea mwaka mmoja naenda kufanya usaili erolink asee nimekaa pale njia panda saa 12 jioni wakanishauri nipande gr la magazeti nlivumilia ule mwendokasi saa 5 nipo mjini nakumbuka kuna mjeda mmoja tylikua naye kwenye gari alipowaambia wapunguze speed wakataka kumrudishia hela yake kuna jamaa mwingime alishuka Mombo!
 
Elezea uzoefu wako, mara ya kwanza kusafiri na gari la magazeti ulikutana na changamoto gani?

Nini ushauri wako kwa ambao hawajawahi kutumia usafiri huo?

Aisee kipindi cha nyuma kuna siku nilipatwa na msiba wa uncle nikaomba gari la ofisi wakaniambia nigharamikie mafuta ya kwenda na kurudi mmm nikapiga hesabu hizo gharama nikaona natumia hela nyingi ndo jamaa zangu wakanishauri nipande hilo gari aisee nilienda pale kinondoni biafra linapoanzia safari aisee hapo njiani linapaa kwa kweli wale madereva nadhani kuna kitu wanatumia yaani nimefika njia panda ya himo makuta hata wale wapika chai pale hawajawasha moto na nikafika home hata maandalizi ya kwenda kuchukua mwili bado hata kaburi hawajaanza kuchimba
 
Back
Top Bottom