Tuliowahi kurogwa tupeane uzoefu

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
9,514
Reaction score
23,525
Kurogwa sio udhaifu wakuu ni utamaduni tu.

Nilipigwa biti mahala nikaambiwa nimepewa muda wa maangalizi wa miezi miwili baada ya hapo ni kurogwa kwa kwenda mbele.

Kwa kweli baada kipindi cha mpito niliamka siku ile nywele zimenyolewa hadi kakipara flani kakaonekana juu ya kisogo.

Tangu siku hiyo naendelea kusubiri kifuatacho ITV naona kimya. Mimi naendelea na michongo yangu huku wao wanaendelea na ujima wao.
 
ifike kipindi huu uchawi tuu`advance kwa ajili ya maendeleo endelevu ya mazingira yanayotuzunguka..
ili kila mtu anufaike nao,sio unakuwa mchawi,kazi yako kukaba watu waliojipumzisha baada ya mahangaiko ya kutwa nzima,afu unajisifia uchawi,kweli hili ni bara la giza...ndio maana pia kila kitu kizuri kuhusu dini walikifanya weupe,sisi hatukupigiwa chapuo sababu ya upuuzi wetu.
 
Umenikumbusha chuo kuna mwanafunzi alisimamishwa kujibu swali mbele ya darasa, katika kutoa karatasi mfukoni akadondosha bonge la hirizi, kama kikapu cha sokoni, halafu ye hakushtuka.

Wakati anaaondoka kwenda kukaa baada ya kumaliza yaliyompeleka mbele. Lecture akaliona (Lecture mtu mzima sanaa na alikua mtata kinoma yani). Ila siku hio aliongea kwa upole sana kwa mara ya kwanza, uoga wa kuiona ile POWER BANK ilivyokubwa. Ikabidi amwite kwa upole "Bro umesahau zana yako kwenye stage".

Jamaa hakuonesha nidhamu ya uoga, mdogo mdogo akarudi na kuiokota tena kwa swagger aisee. Ma Lecture/Wanafunzi tulikua tunamuogopa jamaa kama gonjwa la UKIMWI, maana muda wowote unajua ukimzingua kina nuka.

Darasa zima tuliangua kicheko, hatari
 
Mfukoni litoke kapu la sokoni?
 
Pape Ndew huyo
 
Kweli kabisa kama wanaweza kuruka kwa ungo kwanini waingie gharama za kusafiri kwa basi, meli au ndege?
 
Hahaaa haaa haaaaaaa'' Jamaa alikuwa anatembea na kisimbuzi
 
Amina mtumishi wa Mungu. Ukisimama kwenye maombi wachawi wanaanza kukuita wewe ndo mchawi maana unakuwa kwenye viwango vingine ambavyo nao vinawachanganya!!!!! Mungu yupo na anafanya Kazi na wanaomhitaji!!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…