EINSTEIN112
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 21,709
- 35,702
- Thread starter
- #161
We jamaa visa vyako vya ugomvi kinoma unaonekana ulikua mbavu shuleSuspension nyingine nilipata kizembe sana .
ILIKUWA HIVI:
Kuna demu nilikuwa nikipata kuongea nae kupitia simu kwa sababu shule yao inakatazwa simu basi hiyo siku naazimisha kwa kupiga msuli mpaka asubuhi sasa siku hiyo nimeongea nae nikajikuta mwamba nikachukua kitini cha Advanced Mathematics cha Necta za Nyuma kama zote nikaenda kuzisolve sasa nikajikuta narudi bwenini saa 11.30 alfajiri bichwa langu lilikuwa lime jam balaa na kesho ndo j3 Assemble ambayo na mkuu wa shule huonekana na mara nyingi wote hutakiwa kuonekana asubuhi hiyo parade.Bwana wee nikajiroga nilale kidogo hata li saa limoja khaa kumbe wenzangu wameshajiandaa wametoka wameenda assemble mida kama ya saa 1.45 wakaja walimu wanne wanaosifika kwa unoko pale shuleni kusweep madoja daa si wakanivuta shuka ghafla na kuanza kuniamsha si nikaamka na wenge langu nikaanza kuwatia mitusi ya nguoni kuja kuangalia vizuri kumbe ni walimu aisee nilikokotwa mpaka assemble nikiwa nimevaa surual truk na kesho yake barua.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app



