Tuliowahi kupewa suspension tukutane hapa

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,518
Nikiwa Form 5 Moringe Sokoine Sec tuligoma A-level wote kisa kukataa kufanya usafi dining na library wakati huo Lowasa akiwa Waziri wa Maji na ndio Mwenyekiti wa bodi ya shule tukapigwa suspension ya miezi miwili wanafunzi 9 na turudi na wazazi.

Form 6 watu watano
Form 4 wanne
PCB nikiwa peke yangu

Nlijificha kwa anti Lyamungo Sec Moshi akanitoa nduki ikabidi niende home Morogoro dingi mjeshi alinitandika viboko vingi sitasahau.

Siku tunarudi kuna mwanafunzi mmoja tuliripoti pamoja kumbe alimkodi mtu awe mzazi wake yule jamaa alipandwa na mori kama mzazi kweli alimtandika jamaa viboko mbele ya headmaster.

Nilijua kakodiwa wakati tuna wasindikiza wazazi stendi wakaanza kupigana njiani

Kama ulishawahi kupigwa suspension tukutane hapa na kisa chako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipigwa mara 3, form one, form 3, na Form 4 nilipigwa ile suspension isiyo na muda mpaka kikao cha Bodi kikae,

Walikuja kukaa wiki moja kabla ya Necta, nikapiga pepa na kupita hivi,

Uchakataji huu ulinitia hasara sana,

Kosa:
Hiyo supsension ya Form 4.
Nilimlimtorosha dogo wa hostel na kwenda kulala naye gheto Asubuhi namrudisha tukafumwa na Matron.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tosamaganga nilikula suspension ya wiki 4. Kisa ilikua chakula wanafunzi tulilalamika msosi mbovu. Kuna jamaa alikuja na info sijui kazitoa wapi kwamba kila mwanafunzi wa boarding inatakiwa ale msosi wa elfu 6 kwa siku.

Ila chakula tunachokula kwa siku hakina ata thamani ya elfu 2. Basi jioni tunaongea kama vikao maroom tunapita room kwa room kumbe mshikaji mmoja alikua spy. Jamaa aka tuchoma kesho nashangaa assemble barua. Duh. Mkiwa wengi raha ila unavopokea barua alone huna backup.

Tulikua na mtoto wa mtu mkubwa sana pale Iringa katika kituo cha polisi (sikumbuki vema cheo chake) ila alivorudi week 1 akarudishwa kwa escorte si wengine hadi week 4. Mshua alishindwa kuja alikua anaumwa kaka akaja kwa niaba. Ila alibeba ID ya mshua na vielelezo vingine.

Izo week 4 sikua na raha home, nikicheki hali ya nyumbani mbaya, msosi upo kwakua kuna mashamba ila baadhi ya mahitaji dah hayatimizwi kwakua hela ngumu. Niliumia sana na nikajiona fala. Nilivorudi shule nikakaza fresh nikatoboa somehow form 4. Ila ujana na utoto mbaya sana. Hawa madogo nikiwaona chuo/shule wana leta usela nawacheki nasema sawa ngoja miaka 10 ijayo.
 
Nilipigwa suspension nikiwa nimebakiza wiki mbili kabla ya necta form four,sintosahau Mama yangu alivyokuja anatoa machozi, kisa ilikuwa kukataa kupigwa fimbo za kushitukizwa zisizokuwa na kipimo wala eneo maalumu la kupiga, nikasamehewa,

Na sintosahau ile tunaanza necta kwa kuanza na hesabu niliadhibiwa na headmaster fimbo za kushika kucha, afu ndo uruhusiwe kuingia kwenye chumba cha mtihani. Nilipata F mtihani wa hesabu kitu ambacho kilinifanya kupata division three japo nilipata one, kwa sababu ya penalty ya F ya hesabu.
 
EINSTEIN112, Mimi yangu ndefu Sana lakini kufupisha ni kuwa nilipewa suspension o level nikiwa form four ya wiki mbili kisa nasoma tuition nje na shuleni na ilikua shule ya day.

Suspension ya pili nilipewa nikiwa advance kisa nilikuwa mmoja wa waanzisha mgomo,

Na hii nilikula ya wiki 6, na nilipewa barua ya kwenda kuisaini kwa afisa elimu wa mkoa nirudi nayo shule siku suspension ikiisha

Sasa kimbembe kilikua kuisainisha hiyo barua, maana nilimkuta afisa elimu ambae alikuwa ni mkuu wa shule katika hiyo shule niliyokuwa ninasoma mwaka mmoja uliopita kabla ya Mimi kuingia hapo form 5.

Nilipoingia ofisini kwake, hii ofisi iko katikati ya jiji , akaniambia nishuke chini nikatafute fimbo (ofisi iko ghorofani) maana hawezi kukubali shule aliyokua akiiongoza iwe na wanafunzi wasio na nidhamu kama mimi hivo alitaka aniadhibu pia,

Kweli nikashuka chini nikaenda mpaka kwa mlinzi nikamueelezea situation akanikubalia kukata tawi la mti mmoja uliokua nje ya geti pale, nikarudi ndani, sasa wakati napishana na watu wakati napanda ngazi nilikuwa najifanya nachechemea ili waone ule ni mkongojo

Nikafika mpaka juu ofisini kwake, akaniangaliaa halafu akaniambia nilikua nakupima tu nione kama Una nidhamu, akachukua barua akaisaini, basi ndio ikawa pona pona yangu, nikarudi zangu chini kwa style Ile Ile ya kuchechemea, nakumbuka Ile fimbo nilipanda nayo gari mpaka nyumbani kama ukumbusho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa alilala darasani nikamuandika Kwenye shati na marker pen, NINA K*#MA TAMU
Jamaa alikuwa form4 lakini alikuwa age imeenda kidogo,midevu na misharubu imejaa halafu alikuwa wale washkaji too much know,ambao rafiki zake wengi ni madem

Alipoaamka ilikuwa break time sasa kipindi anazurula mda wa break kutafuta sifa akawa anashangaa madem wanamcheka, kuwauliza nini? Wakamwambia ana maandishi nyuma ya shati..

Jamaa alipoyasoma akaanza kulia akaja pale Dukani akatukuta backbenchers tunakula akaja akauliza huku analia oya mazee nani kaniandika mgongoni?...itaendelea
 
Nilipewa sio sbb nilihusika kwenye vurugu. sababu Nilikua HP na nilijua vugu vugu lote la mgomo na vurugu ila sikuripoti.

Ndio ulikua mwisho wa U HP na suspension juu. Kufika home machungu yote nikahamishia kwenye msuliii.

Nilirudi siku ya Mtihani ya kanda. Matokeo yanatoka wa tatu kwa kanda.
Wakanipa u accademic.

Nako nikadakwa na wana Jikoni muda wa prepo tunakula mikate na chai ya asubuhi karibia nusu jabaaa. Kuanzia pale nikaambiwa wewe utakua mlinzi wa jikoni mpk unamalizaaa....

All in all nilikua na upepo sana wa uongozi hasa u headboy kipindi na somaa....
Nilikua nakubalika na ushawishi sanaaaa....

Kati ya watu ambao hata walimu na kwenye mahafali pia watu wengi waliamini nitakua mwanasiasaaa..
Ila hata sina huo upepoo, labda hata masomo niliyochagua yamechangia kutoenda kwenye siasa..

Washkaji niliosoma nao hawaamini mpk leo upande niliopooo...

Nimesoma shule nying...
Natamani nitaje ila kuna watu watani ng'amua humu.. naamini wapo wengi tuu humu..

Pia nilishawahi kujihamisha shule mwenyewee. Nishawahi singizia pia dingi kavuta kisa nimebanwa ada iko wapi maana nishakulaa ili nisamehewe.

Ilibakia Kidogo tuu nipate msaada wa wazungu flan hv waliokua wanasaidia yatimaa...
Ile aibu sitoisahau.

Mzee, bimkubwa na Sista ilibidi wacheke tu.

Ila sasa nimetulia kuliko watoto wao woteee..
Pamoja na kua mtukutu sana.....
Ila sikua na sifa ya kiburi wala jeuri na pia nilikua nakaza darasanii..
 
Kuna jamaa alilala darasani nikamuandika Kwenye shati na marker pen, NINA **** TAMU
Jamaa alikuwa form4 lakini alikuwa age imeenda kidogo,midevu na misharubu imejaa halafu alikuwa wale washkaji too much know,ambao rafiki zake wengi ni madem
Alipoaamka ilikuwa break time ...sasa kipindi anazurula mda wa break kutafuta sifa akawa anashangaa madem wanamcheka,kuwauliza nini? Wakamwambia ana maandishi nyuma ya shati...jamaa alipoyasoma akaanza kulia akaja pale Dukani akatukuta backbenchers tunakula akaja akauliza huku analia oya mazee nani kaniandika mgongoni?...itaendelea
Jinsi alivyokutandika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawai kuona suspension ya muda mrefu Kama ya kwangu. Nilibambikiziwa kesi kwamba nimekutwa na msichana wa o-level Mimi nilikuwa form five tena ndo Kwanza miezi minne toka tumeanza hyo form five.

Nilifukuzwa nikaambiwa utaludi kufanya mtiani wa taifa wa form six. Ni story ndefu Ila ngoja niishie hapa Ila nacho mshukuru mungu matokeo ya form six yalipo toka mm ndo niliongoza shule.
 
Back
Top Bottom