ndukulusudicho
JF-Expert Member
- Aug 14, 2017
- 502
- 771
Mi nilikua naishi na anko wangu alikua RPC mkoa fulani Kanda ya ziwa . Nikapelekwa kusoma huko o level huku nikiishi nae ili aninyooshe mana nilikua mtukutu kweli nishafumwa na kesi nyingi zikiwemo ugomvi, wizi, utoro, uzinzi na ganjaNikiwa Form 5 Moringe Sokoine Sec tuligoma A-level wote kisa kukataa kufanya usafi dining na library wakati huo Lowasa akiwa Waziri wa Maji na ndio Mwenyekiti wa bodi ya shule tukapigwa suspension ya miezi miwili wanafunzi 9 na turudi na wazazi...
ila niliishia kupata adhabu ndogo siku niliopewa suspension nilifungua tyre ya rand rover ya shule iliokua imeharibika imepaki muda mrefu nikaenda kuiuza nikishirikiana na rafki yangu ambae sa hivi ni mtu maarufu.Nitakuja kutoa full story nikitulia nashkuru wadhifa wa anko ulinibeba sana, utoto bhana ahsante mungu leo hii nimebadilika kiasi kwamba najisikia vibaya hata kukumbuka matukio ya nyuma.
