Tuliowahi kupewa hela na wanawake

Asante kwa kunielewesha dada carleen

Sent using Jamii Forums mobile app
 
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Inaonekana unauzoefu wa parasite ๐Ÿ˜…
Pole sana..
 
Kuna wanaume nikiwakubali wanakula hela yangu kiroho safi tuu. Nimelelewa maadili ya kuwa, mwanaume ni ikichwa cha familia hivyo akihitaji hela kwangu kama nnayo nampa bila kutaka kujua atairudisha lini, anaifanyia nini.

Ila akikuta nimekaukiwa sina kabisaa hela ya kumpa, daah ntajikuta namwambia usijali ntakupigia simu kukwambia nakupaje hiyo hela, hivyo akiona kimya ajue ndo getegete.

Pesa si kitu mbele ya upendo ila ambacho sifanyi ni kuhonga, pesa yangu sihongi mwanaume ila akiniambia ninahitaji pesa na sauti yake ikapata kibali kutoka moyoni kuwa mpe, pasi shaka namtumia tuu.

K' Matata.
 
Xmas ya 1990 Niko Mby kipindi hicho nilikua na rafiki wa kike, alikua na watoto 2 wakati mimi kijana. Kwa kweli huyu mdada, msafwa mweusi mtamu alinipa sh 700 kipindi hicho ni hela nyingi sana.

Wakati nimelala kwake usiku kazitia kwenye mfuko wa suruali yangu. Wakati nakatiza mitaa ya Makunguru kutia mkono mfukoni nikaibuka na mzigo 700 shillings cash.
 
Nakumbuka wakati naanza mahusiano na huyu niliyenaye nilikuwa bado sina ajira. uzuri nilikuwa na kabiashara kangu ka tigo pesa nashanga siku anakuja kwenye kiofisi changu akaniambia anatoa pesa nikampa code ya wakala yangu akatoa 700000.

Ile namwesabia nimpe akasema amenipa niongezea mtaji daaah sikuamini na sikuwahi muomba kabisa.

Thanks God ile hela ilikuwa na bahati mtaji ulikuwa na biashara ikatanuka.kuna wanawake wanaletwa kwenye maisha yetu kama ngazi ya mafanikio.hawa ni wakiwaheshimu na kuwajali.
 
Na wala hukuwa na haja ya kumuuliza katoa wapi? ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ˜‚
 
Ili nigindue nn mkuu[emoji1787] mdada anajielewa sinaga mawazo mgando kwake.namwamini ananiamini
Na wala hukuwa na haja ya kumuuliza katoa wapi? [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ˜‚
Wooiiii..!
Wengine ni marafiki tu lakini wanajua kutuchuna walaqhi'..!
Halafu wanaume wadangaji mara nyingi ni wale wenye muonekano mzuri, wanajua uzuri wao unawapa credit wakitaka chochote.!
Ha ha!
Pole zaidi inaonekana unatufahamu vilivyo.. na nyie itabidi muone tuuchungu twa kuomba hela hela..
Vijana wanahangaika ajira hakuna elimu tuliyonayo ya kuajiliwa unataka wajiajiri ndo wanajiajili hivyo Sasa๐Ÿ˜‚

Binafsi tabia za kumuomba mtoto wa kike hela dah!! Kusema kweli sijawahi labda sister au mother wangu hao ndo naweza lkn na wao Mara chache sanaaa.. ila mother ye ndo mdekezaji ananidekeza kiziwanda chake๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜…
Nampenda Sana mama yangu japo sideki ila anajua kunidekeza..๐Ÿ˜‚๐Ÿคฃ
 
Ila tabia ya kuomba omba sio nzuri. Kama mwanamke anakupenda na anaiona hali yako ilivyo ya kimaisha na yeye kidogo ana kitu cha kuniangalizia hela,atakusaidia tu.
 
Binafsi nikimuelewa mtu na asipokuwa na mambo mengi basi atanikula helaa๐Ÿ™„sijui huwa napatwa na nini๐Ÿ˜‘
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ