Tuliowahi kulala Sero/lock up kwa ujinga

Tuliowahi kulala Sero/lock up kwa ujinga

carnte

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2017
Posts
362
Reaction score
425
Sitakuja kuisahau siku ile niliamka asubuhi nikiwa sina chochote, bahati mbaya ndugu mmoja akanipigia simu na kuniambia maneno ya dharau sana.

Nilikasirika sana bahati mbaya mimi ni kati ya wale ambao hukimbilia pombe nikivurugwa, sikuwa na pesa mfukoni ila kuna mtu alikuwa anitumie pesa yangu baadae, nikaondoka nikaenda kwenye pub moja hivi nikaweka simu bond nikaanza kutupia vitu mpaka nikatosheka.

Yule mtu hakutuma pesa, kesho yake nikaamka na hangover nikasema nikacheki simu na pesa labda itakuwa imetumwa kufika sikumkuta yule jamaa, nikakuta wafanyakazi wake, ujinga nikaanza kupakia vitu tena.

Sasa kwenye kulipa, nikawaambia nitakuja kulipa jamaa ana simu yangu, bili inasoma elfu 15, duu bahati mbaya yule mmiliki akatokea, akaniuliza pesa yangu nikawa najiuma uma duh!

Kumbe anamshikaji wake askari, dakika sifuri jamaa alikuja akanichukua hadi lock up, aibu kwanza ni Mara ya kwanza, jamaa hakunipa hata room nikachukue hiyo pesa nililala huko sio pazuri kabisa.

Kesho yake jamaa alienishtaki akaja na simu yangu bahati pesa ilikua imeingia
kilichonitia hofu ni ndugu kama wangejua nimelala huko, liliisha bila kujua na waliponiuliza niliwaambia tuliharibikiwa gari.

Sitakuja kusahau hili
 
Miaka ya nyuma nlizinguana na wazee tena tulikuwa bar kumbe sikujua kama jamaa Wale ni askari....nliwazidi nguvu basi jamaa wakaita wenzao Baada ya nusu sasa difenda londo hiyo wakanichukuaa hadi obay kutoka obay wakaniandikia statemnt eti nmewapga hadi kuwachania nguo.....wakaniweka selo nlipokuwa selo nkaomba sim nkawambia Nampigia ndg yangu maana wazee walitaka Laki tatu....waliponipa sim skumpigia ndg yng nlimpigia kalinga enzi Hzo ndy mkuu wa kituo hicho Dk5 nyingi wenyewe walintooa

Ova
 
haahhahaha
NILIWAHI KUMTANDIKA OCCID MMOJA BAA
baada ya kuniuliza UNANIJUA MI NANI?MI NIKAMWAMBIA HATA UNGEKUA MUNGU HUWEZI KUNINYAKUA KADEMU KANGU
Aisee nilala lockup ila kesho yake nikatoka tukakutana tena palpale baada tukayamaliza kwani alinipoza na bia4
 
sikulala selo ila nikaaa kwa masaa 8, baada ya kumfanyia vurugu mama mmoja jirani, nakumbuka nilitupa ndoo ndoo ya maua dirisani kwake ikavunja tv, kisa alimsemea mbovu bibi yangu nikamsikia, bibi aliwanyima kuchota maji waliaacha yanachuruzika tuu, na geti hawakufunga...

kilichofanya nitoke ni kujuana kwangu na maaskari na nilikuwa mmoja wa viongozi vijana kabisa wa UVCCM, pale Majengo Moshi Mjini,hivyk viongozi wangu wa kata walisaidia dia japo kipindi hiko nilikuwa form 2, jamaa akaniambia we kaa kwanza mpaka saa mbili atulie tutakutoa duuh nilijuta maana kukaa chini nilichoka na kusimama nilichoka hamna nafasi ya kujilaza na hewa ni nzito...

nnakumbua mdingi mmoja aliishia kulia tuu kama fala
 
Mimi sikulala ndani ila niliwekwa kaunta pale wanapokaa polisi kama masaa 6 hivi. Nilikuwa bado mdogo sana kati ya miaka 7-10. Nilipasua kioo cha gari la advocate maarufu Bukoba (Advocate Rweyemamu) wakati nawinda ndege mshande na njiwa. Jioni baada ya wazazi kurudi na kupata taarifa wakaja kituo kikuu cha polisi Bukoba na kumalizana kwa kulipa gharama ya kioo.

Rweye.png
 
Enzi hizo tunauza sim azam take away pale Kuna sim nlipewa na fundi mmoja pale anaitwa yahaya mitaa ILE,akikopa nkaiuze nkaichkua nkaipeleka central police Kuuza Kuna poti mmoja alikuwa ananisumbua sana kutaka sim kuipeleka kumbe Ilikuwa ya jamaa yake polisi yule alikuwa anaitwa koba kabanda wacha aninganganie hadi kuniweka selo chini kule...
Ushkaji uliwekwa kando hapo ...nlijipeleka mwenyewe Yaani

Ova
 
Nakumbuka nilikuwa chokoraa enzi hizo moshi mjini. Nilikuwa nalala stendi bana nikiwa na wenzangu sasa bana siku hiyo kumbe kulikuwa na msako wa machokoraa hawatakiwi kulala stendi. Mida flani hivi kama saa mbili tatu hivi jamaa mmoja akajipendekeza akataka kunishika nikamkwepa afu nikamjibu mbovu sana. Kumbe alikuwa askari. Sasa mausingizi si yakanishika nikaenda kujilaza chocho flani hivi kumbe walinzi wote wa stendi walipewa agizo lakukamata machokoraa wote. Ilipofika mida ya takribani saa 9 kasoro mzee jamaa mmoja alinikwida mzegamzega mpaka nakuja kufahamu nini kinaendelea nimekaribia central. Khaaaa nikamuomba yule mlinzi chondechonde kaka nakuomba usinipeleke polisi... nikamuahidi pesa jamaa kakataa, mara paaaap central ndani sasa wahalifu wengine wakaanza kunikaribisha wako nyuma ya nondo mzee mimi ndo mgeni wala sikuwahi kuingia polisi hata siku moja. Sikuchanganywa na hao nikapitishwa moja kwa moja mpaka uani nikakuta kuna baadhi ya wenzangu kule duuuh. Asubuhi kulipokucha nilikuja kutolewa na OCD alikuwa ananijua maana nilikuwaga namuoshea gari lake sasa baada ya msako wa jana usiku alijua manyamera yasingeniacha.
 
Nakumbuka mwaka juzi nililala sero mwaka juzi, kisa wanawake.. Inshu ilikua hivi,, ilikua nyumba ya kupanga tulikua wapangaji wanne kulikua na mwalimu mmoja ameolewa na ana mtoto mmoja uku na uku akashoboka nikamtia mara kibao tu, kuna mpwa wao alikujaga kuwatembelea alikua binti mzuri tu uku na kule nikapita nae ikawa mboga kila nkijisika nakula sa yule dada akajaga akastuka kua namchanganya na mpwa wake (uyu mpwa alikua upande wa mwanaume) Akantukana sana tu nkamtema uyo dada nkaendelea na mpwa wake ilimuuma mno.. Baada ya
siku kadhaa kupita kuna mpangaji mwenzutu akaleta beki tatu mbichi mzuri chuchu yimesimama mwisho wa siku nikaimba nae akaingia king nikamnywa pia,, yule mwalimu alipokuja kujua akaanza kuniponda kwa watu kitaa kua nina ukimwi iliniuma sana, nkamtafutia nafasi na mi nkamtukana kama haitoshi nkamvizia usiku wakati anaoga nkarushia upupu nkasepa zangu nkarudi mda umeenda wakaja kunishitukia kua ni mimi kesho yake wakaenda polisi, ilikua wanidake usiku wakanikosa kesho yake mida ya saa tatu asubui wakanikamata

Kesi ilipokuja kuishia ni baada ya kuweka wazi mambo yote chanzo cha ugomvi nkawaambia askari uyu mi nilikuaga natembea nae na nkatembea na mpwa wake na beki tatu pia sa uyu kinachomsuambua ni wivu mbele ya kaka yangu na kijana wa mwenye nyumba yule dada aliona aibu akasema basi mi naomba aya mambo yaishe yakifika kwa mme wangu ataniua.. Mambo yakaisha na pale nkaama nilikaa polisi toka saa tatu asubui hadi sa kumi na mbili jioni
 
Miaka ya nyuma nlizinguana na wazee tena tulikuwa bar kumbe sikujua kama jamaa Wale ni askari....nliwazidi nguvu basi jamaa wakaita wenzao Baada ya nusu sasa difenda londo hiyo wakanichukuaa hadi obay kutoka obay wakaniandikia statemnt eti nmewapga hadi kuwachania nguo.....wakaniweka selo nlipokuwa selo nkaomba sim nkawambia Nampigia ndg yangu maana wazee walitaka Laki tatu....waliponipa sim skumpigia ndg yng nlimpigia kalinga enzi Hzo ndy mkuu wa kituo hicho Dk5 nyingi wenyewe walintooa

Ova
 
Enzi hizo tunauza sim azam take away pale Kuna sim nlipewa na fundi mmoja pale anaitwa yahaya mitaa ILE,akikopa nkaiuze nkaichkua nkaipeleka central police Kuuza Kuna poti mmoja alikuwa ananisumbua sana kutaka sim kuipeleka kumbe Ilikuwa ya jamaa yake polisi yule alikuwa anaitwa koba kabanda wacha aninganganie hadi kuniweka selo chini kule...
Ushkaji uliwekwa kando hapo ...nlijipeleka mwenyewe Yaani

Ova
Pamoja ya kuwa hapa mjini mimi ni Mgeni, hivi yule Fundi Simu YAHAYA Mmakonde bado yupo pale juu kigorofani....................!!!!!?????
 
Back
Top Bottom