Tuliowahi kulala Sero/lock up kwa ujinga

Nakumbuka nilikuwa chokoraa enzi hizo moshi mjini. Nilikuwa nalala stendi bana nikiwa na wenzangu sasa bana siku hiyo kumbe kulikuwa na msako wa machokoraa hawatakiwi kulala stendi. Mida flani hivi kama saa mbili tatu hivi jamaa mmoja akajipendekeza akataka kunishika nikamkwepa afu nikamjibu mbovu sana. Kumbe alikuwa askari. Sasa mausingizi si yakanishika nikaenda kujilaza chocho flani hivi kumbe walinzi wote wa stendi walipewa agizo lakukamata machokoraa wote. Ilipofika mida ya takribani saa 9 kasoro mzee jamaa mmoja alinikwida mzegamzega mpaka nakuja kufahamu nini kinaendelea nimekaribia central. Khaaaa nikamuomba yule mlinzi chondechonde kaka nakuomba usinipeleke polisi... nikamuahidi pesa jamaa kakataa, mara paaaap central ndani sasa wahalifu wengine wakaanza kunikaribisha wako nyuma ya nondo mzee mimi ndo mgeni wala sikuwahi kuingia polisi hata siku moja. Sikuchanganywa na hao nikapitishwa moja kwa moja mpaka uani nikakuta kuna baadhi ya wenzangu kule duuuh. Asubuhi kulipokucha nilikuja kutolewa na OCD alikuwa ananijua maana nilikuwaga namuoshea gari lake sasa baada ya msako wa jana usiku alijua manyamera yasingeniacha.
Bless up King

Bila shaka sasahivi una kwako maisha yanaenda poa.

Nimesoma kisa chako nikakumbuka filamu ya Lion.

Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu ni moja ya kundi linalopata shida sana kwenye jamii.

Niliwahi kukutana na mtoto miaka minne yupo street. Moyo wangu ulivunjika.

Stay strong warrior
 
Pamoja sana kamanda! Nilipokua naiandika hiyo meseji machozi yalikuwa yananitoka aseeee! Kuna wakati najaribu kugeuka nyuma naangalia kule nimetoka najikuta tu nanyanyua mikono namshukuru Mungu kwakunilinda. Sikuwahi kuvuta kilevi chochote, sikuwahi kunywa pombe wala kuwa mdokozi au mwizi kipindi nimepita huko. Nilipendwa sana na watu wenye maduka yao hata wakati mwingine nilikuwa nalala kwenye maduka yao. Zamani maisha yalikua mazuri watu walikuwa na upendo mwingi sana lkn sasa hivi wanadamu wamekuwa hatari sana

Ni kweli sasa hivi nafamilia yangu maisha mazuri napambana kuhakikisha hali niliyopita wanangu wasijepitia by force, by fire!
 
Pole sana Madame B. Hakika Mungu alikuwa na wewe.
Asante mkuu.
Huwa wakati mwingine unapatwa na jambo mpaka unaona dunia imekuacha peke yako.
Halafu huwa najiuliza, laiti yule trafiki asingetokea pale na kusema kuwa kaambiwa gari imeonekana Magomeni, leo hii mimi ningekuwa wapi!!!
Wakati mwingine malaika huja kwa njia ingine tofauti na katika maumbo na mavazi mengine.

Mkuu kama wewe ni mpenzi wa movie za ushuhuda, tafuta hii movie "Miracles from Heaven" hakika unaweza lia kwa hisia.
Screenshot_2017-10-28-00-15-07-1.png
 
haahhahaha
NILIWAHI KUMTANDIKA OCCID MMOJA BAA
baada ya kuniuliza UNANIJUA MI NANI?MI NIKAMWAMBIA HATA UNGEKUA MUNGU HUWEZI KUNINYAKUA KADEMU KANGU
Aisee nilala lockup ila kesho yake nikatoka tukakutana tena palpale baada tukayamaliza kwani alinipoza na bia4

Na demu akamchukuwa au?
 
MIMI ananijua vilivyo nlimsumbua sana enzi hizo sema Mpaka leo Mwana sana alafu anashangaaa watu tumekuwa raia wema maana enzi hizo Ilikuwa shidaaaa

Ova

Kawaida tu!enzi za kuishaaa watu tuliwenda mbeleee n'a tukaja kurudi tena
Yahaya ndiyo alikuwa fundi mkuu wa simu mitaa ya posta enzi hizoooo
Wakati huo unauza simu azam n'a salamanda ....najua Kuna watoto humu salamanda hawajaikutaaaa

Ova
Watu wa ''Dalisalama'' Kiswahili chenu mnakijua wenyewe.....mimi umeniacha ''Magoti''............!!!!
 
Nilikuwa naendesha gari natokea Amani naenda meli 4. Kufika kwerekwe nikakutana na mshakaji wangu akaniambia turudi Amani kwenye baa flan tukapate msosi
Baada ya kula tukaanza kutupia vyombo, kuna wengine walikuwa wanacheza kamari ya pool. Nikawatamani, nikilewa nakuwa mtam sana kwenye pool,
Niliwapuna kumbe ni maaskari, kuna kioo kilikua chino kdg kumbe waliniwekea bange kwenye gari. Tunataka kuingia garini tu, tumevamiwa na askari 4. Tulikaa lockup lakini hatujalala. Niliwarudishia hela niliowala na zile bange zao tulizivuta pamoja!"
 
Asante mkuu.
Huwa wakati mwingine unapatwa na jambo mpaka unaona dunia imekuacha peke yako.
Halafu huwa najiuliza, laiti yule trafiki asingetokea pale na kusema kuwa kaambiwa gari imeonekana Magomeni, leo hii mimi ningekuwa wapi!!!
Wakati mwingine malaika huja kwa njia ingine tofauti na katika maumbo na mavazi mengine.

Mkuu kama wewe ni mpenzi wa movie za ushuhuda, tafuta hii movie "Miracles from Heaven" hakika unaweza lia kwa hisia.
View attachment 618912
Asante. Nitaitafuta.
 
Niliingia mahabusu nusu siku Magomeni Polisi ishu ilikuwa hivi:-
Siku hiyo nilikuwa zangu manispaa Kinondoni nafunga data sheet kwani nilikuwa nahama wilaya kwenda wilaya ingine.
Nilivyomalizana na wadada wa masijala Ile nakata kona kuondoka nje kupitia pale jengo la mkuu wa wilaya Kinondoni nikakutana na mkaka smart tu, simjui.... akaniambia dada mambo, unajua muda mrefu nakufatilia tangu unaingia, yaonekana wewe mstaarabu na blah blah nyingiiiii.....at the end akaniomba tukapate lunch pamoja.
Nami kwa kuwa nilikuwa na njaa nikaona kijana yuko smart afu anaonekana mstaarabu ngoja tu niende ila nikamwambia tusiende mbali sana maana file langu limepelekwa kwa afisa utumishi, akasema sawa.
Basi tukatoka nje akaita teksi tukaingia na kusepa.
Tukaenda mpaka mitaa ya Kigogo cha wote kula.
Dereva taksi baada ya kulipwa alivyotaka kuondoka yule kaka akamwambia kaa na wewe ule.
Dereva akakaa na kuanza kula.
Basi ile tunakaribia kumaliza dereva na yule jamaa wakainuka kwenda msalani, jamaa yule smart nikamuona anarudi kisha akachukua funguo ya gari akaingia kwenye ile taksi peke yake akaiwasha na kusepa.
Mie nikasema kwa kuwa walienda wote msalani itakuwa kamuazima gari.
Dereva anarudi haoni gari wala yule jamaa.
Akaanza kuuliza yule bwana ako yuko wapi?
Nikamwambia mie yule simjui nimekutana nae tu Manispaa.
Afu si mlikuwa wote msalani, nikajua mmeenda kuongea umuazime gari.
Weeeee......yule dereva akasema we dada sikuelewi, utanieleza leo.
Mie yule simjui na wala sijamuona akiingia msalani.
Akaanza kujaza watu....watu walivyojaa akawaeleza kila kitu A to Z.
Mie najitahidi kujitetea ila watu hawaelewi somo.
Wengine wakasema sie majambazi wa magari na nionyeshe yule kaka alikoenda.
Jamani omba yasikukute.
Bili ya chakula haijalipwa, soda hazijalipwa na bado nishaundiwa zengwe.
Kila nikijaribu kujitetea naambiwa wewe dada jambazi, onyesha alipo mwizi mwenzio.
Nikwaambia jamani mie simjui, dereva taksi akaniambia mbona ndani ya gari ulikuwa unaongea nae asi if mnajuana, mie nikamueleza niliamua kumchangamkia tu.
Nikaanza kulia pale....nililia kwa uchungu wa kutuhumiwa jambo ambalo sijafanya.

Baada ya majadiliano ya kama dk 5, ghafla trafiki mmoja akaja mpaka pale, akauliza kulikoni ikabidi wamuelezee maana mie hata nguvu sikuwa nazo.
Baada ya trafiki kusikia vile akasema kuwa kapigiwa simu na trafiki mwenzie kuwa kuna taksi imetelekezwa mitaa ya Magomeni Mapipa baada ya kuishiwa mafuta.
Ikabidi mie, trafiki, wapambe na yule dereva twende Magomeni.
Kufika pale mapipa tukakuta ni ile ile taksi ila ndani hakuna mtu.
Nilipiga magoti na kupiga ishara ya msalaba katikati ya barabara.

Mara akaja mkaka tu akasema vipi mbona mmejaa hapa, tukasema tunamtaka mwenye gari hii, yule kaka akasema huyo dereva kaenda kununua mafuta kasema nimlindie gari yake.
Tukamuuliza yukoje akatutajia, yaani ni yule mwizi kabisa.
Askari akasema tumsubiri ila tutoke hapa barabarani ili hata akija asijue.
Basi tukatoka tukajificha.
Dk 5 yule kaka mwizi akaja na kidumu.
Ila anasogelea gari tu watu wakajitokeza akaachia kidumu akakimbia, akaanza kufukuzwa akaenda kukamatiwa kule mtaa wa Dosi.
Basi alipokamatwa akasema mie siko peke yangu niko na huyu dada.
Weeee.....nililoa sana na kuanza kulia.
Tukabebwa wote tukapelekwa Magomeni polisi.
Kufika pale nikalambwa vibao kama 4 na askari kwa usumbufu kuwa nimewasumbua kumbe najuana na mwizi.
Jamani nilikuwa nalia kama mtoto.

Siku zote mtumaini Mungu hakosi msaada.
Ghafla katika shift za askari pale, aliingia askari ambae namjua na ananijua, baada ya kunikuta pale akaniuliza kulikoni ndipo nikaanza kumueleza yaliyonikuta.
Ndipo yule askari akawasiliana na shemeji yangu ambae ni Afisa uhamiaji airport.

Baada ya kufika pale akasema huyu dada ni shemeji yangu na hana tabia hiyo, huyu kaka mwizi anamsingizia tu.
Basi shemeji wakakaa group na wenzake wakaanza kumuhoji yule mwizi.
At the end ikaja kugundulika kuwa kweli siko nae na wala simjui ila nilikutana nae tu katika harakati zangu za ujana.

Basi kesi ikaisha hapo, yule askari aliyenizaba makofi akanitaka radhi.
Shemeji akanibeba kwenye gari aliyokuja nayo akanishusha nyumbani ye akaelekea ofisini kwake.
Yule dereva akapewa gari yake na mwizi akachapwa makofi na mateke kisha akapelekwa Central.

Tangu siku hiyo:
1. Kama sikujui na ukijifanya kunichangamkia ujue utaishia kutukanwa

2. Ofa za wanaume walio smart, nimekoma tena nimekoma kabisa.

3. Ukinisalimia njiani na nikakuitikia ujue una bahati.
Ila All in All ule ulikuwa ni umalaya tu ambao sitakaa niusahau.
Nilijua nimeopoa mkaka smart kumbe kimeo na kuishia mahabusu.
Kuna kitu cha kujifunza apa
 
Wengi naona wamelala sero ajiri ya pombe, kwaiyo muache pombe ipo siku mtajukuta na jipsi bando tepe tepe
 
Ni mlevi kiasi, huwa naogopa, nakwepa, sipendi ije itokee na sijawahi wekwa sello!

Kuwekwa selo kwa sababu ya ulevi ni aibu kubwa
 
nilikuwa na mahusiano na afande mmoja, nikajifanya pendapenda nikatoka na frend wake akipo gundua akanipa kesi ya kuiba laptop na simu kwa afande flani.

Nimekaa sero kama 6hrs akaja nikuta afande mmoja jamaa yangu, kunitoa hawezi maana njagu mwenzake ndo kaniweka. akaenda muomba msamaha akakubali. ila kwa sharti tuendelee mahusiano sikuwa na ujanja nikakubali.
Bila Shaka Huyo alikuwa afande WA Kiume
 
Niliingia mahabusu nusu siku Magomeni Polisi ishu ilikuwa hivi:-
Siku hiyo nilikuwa zangu manispaa Kinondoni nafunga data sheet kwani nilikuwa nahama wilaya kwenda wilaya ingine.
Nilivyomalizana na wadada wa masijala Ile nakata kona kuondoka nje kupitia pale jengo la mkuu wa wilaya Kinondoni nikakutana na mkaka smart tu, simjui.... akaniambia dada mambo, unajua muda mrefu nakufatilia tangu unaingia, yaonekana wewe mstaarabu na blah blah nyingiiiii.....at the end akaniomba tukapate lunch pamoja.
Nami kwa kuwa nilikuwa na njaa nikaona kijana yuko smart afu anaonekana mstaarabu ngoja tu niende ila nikamwambia tusiende mbali sana maana file langu limepelekwa kwa afisa utumishi, akasema sawa.
Basi tukatoka nje akaita teksi tukaingia na kusepa.
Tukaenda mpaka mitaa ya Kigogo cha wote kula.
Dereva taksi baada ya kulipwa alivyotaka kuondoka yule kaka akamwambia kaa na wewe ule.
Dereva akakaa na kuanza kula.
Basi ile tunakaribia kumaliza dereva na yule jamaa wakainuka kwenda msalani, jamaa yule smart nikamuona anarudi kisha akachukua funguo ya gari akaingia kwenye ile taksi peke yake akaiwasha na kusepa.
Mie nikasema kwa kuwa walienda wote msalani itakuwa kamuazima gari.
Dereva anarudi haoni gari wala yule jamaa.
Akaanza kuuliza yule bwana ako yuko wapi?
Nikamwambia mie yule simjui nimekutana nae tu Manispaa.
Afu si mlikuwa wote msalani, nikajua mmeenda kuongea umuazime gari.
Weeeee......yule dereva akasema we dada sikuelewi, utanieleza leo.
Mie yule simjui na wala sijamuona akiingia msalani.
Akaanza kujaza watu....watu walivyojaa akawaeleza kila kitu A to Z.
Mie najitahidi kujitetea ila watu hawaelewi somo.
Wengine wakasema sie majambazi wa magari na nionyeshe yule kaka alikoenda.
Jamani omba yasikukute.
Bili ya chakula haijalipwa, soda hazijalipwa na bado nishaundiwa zengwe.
Kila nikijaribu kujitetea naambiwa wewe dada jambazi, onyesha alipo mwizi mwenzio.
Nikwaambia jamani mie simjui, dereva taksi akaniambia mbona ndani ya gari ulikuwa unaongea nae asi if mnajuana, mie nikamueleza niliamua kumchangamkia tu.
Nikaanza kulia pale....nililia kwa uchungu wa kutuhumiwa jambo ambalo sijafanya.

Baada ya majadiliano ya kama dk 5, ghafla trafiki mmoja akaja mpaka pale, akauliza kulikoni ikabidi wamuelezee maana mie hata nguvu sikuwa nazo.
Baada ya trafiki kusikia vile akasema kuwa kapigiwa simu na trafiki mwenzie kuwa kuna taksi imetelekezwa mitaa ya Magomeni Mapipa baada ya kuishiwa mafuta.
Ikabidi mie, trafiki, wapambe na yule dereva twende Magomeni.
Kufika pale mapipa tukakuta ni ile ile taksi ila ndani hakuna mtu.
Nilipiga magoti na kupiga ishara ya msalaba katikati ya barabara.

Mara akaja mkaka tu akasema vipi mbona mmejaa hapa, tukasema tunamtaka mwenye gari hii, yule kaka akasema huyo dereva kaenda kununua mafuta kasema nimlindie gari yake.
Tukamuuliza yukoje akatutajia, yaani ni yule mwizi kabisa.
Askari akasema tumsubiri ila tutoke hapa barabarani ili hata akija asijue.
Basi tukatoka tukajificha.
Dk 5 yule kaka mwizi akaja na kidumu.
Ila anasogelea gari tu watu wakajitokeza akaachia kidumu akakimbia, akaanza kufukuzwa akaenda kukamatiwa kule mtaa wa Dosi.
Basi alipokamatwa akasema mie siko peke yangu niko na huyu dada.
Weeee.....nililoa sana na kuanza kulia.
Tukabebwa wote tukapelekwa Magomeni polisi.
Kufika pale nikalambwa vibao kama 4 na askari kwa usumbufu kuwa nimewasumbua kumbe najuana na mwizi.
Jamani nilikuwa nalia kama mtoto.

Siku zote mtumaini Mungu hakosi msaada.
Ghafla katika shift za askari pale, aliingia askari ambae namjua na ananijua, baada ya kunikuta pale akaniuliza kulikoni ndipo nikaanza kumueleza yaliyonikuta.
Ndipo yule askari akawasiliana na shemeji yangu ambae ni Afisa uhamiaji airport.

Baada ya kufika pale akasema huyu dada ni shemeji yangu na hana tabia hiyo, huyu kaka mwizi anamsingizia tu.
Basi shemeji wakakaa group na wenzake wakaanza kumuhoji yule mwizi.
At the end ikaja kugundulika kuwa kweli siko nae na wala simjui ila nilikutana nae tu katika harakati zangu za ujana.

Basi kesi ikaisha hapo, yule askari aliyenizaba makofi akanitaka radhi.
Shemeji akanibeba kwenye gari aliyokuja nayo akanishusha nyumbani ye akaelekea ofisini kwake.
Yule dereva akapewa gari yake na mwizi akachapwa makofi na mateke kisha akapelekwa Central.

Tangu siku hiyo:
1. Kama sikujui na ukijifanya kunichangamkia ujue utaishia kutukanwa

2. Ofa za wanaume walio smart, nimekoma tena nimekoma kabisa.

3. Ukinisalimia njiani na nikakuitikia ujue una bahati.
Ila All in All ule ulikuwa ni umalaya tu ambao sitakaa niusahau.
Nilijua nimeopoa mkaka smart kumbe kimeo na kuishia mahabusu.
Duuh pole...kwanza ni aibu kukaa mule...natamani kujua nyumbani ulibrush vipi
 
Pamoja sana kamanda! Nilipokua naiandika hiyo meseji machozi yalikuwa yananitoka aseeee! Kuna wakati najaribu kugeuka nyuma naangalia kule nimetoka najikuta tu nanyanyua mikono namshukuru Mungu kwakunilinda. Sikuwahi kuvuta kilevi chochote, sikuwahi kunywa pombe wala kuwa mdokozi au mwizi kipindi nimepita huko. Nilipendwa sana na watu wenye maduka yao hata wakati mwingine nilikuwa nalala kwenye maduka yao. Zamani maisha yalikua mazuri watu walikuwa na upendo mwingi sana lkn sasa hivi wanadamu wamekuwa hatari sana

Ni kweli sasa hivi nafamilia yangu maisha mazuri napambana kuhakikisha hali niliyopita wanangu wasijepitia by force, by fire!
Maisha watu tunatoka mbali sana mkuu,safi sana kuona umepiga hatua maana ulipotoka ni kugumu

Ova
 
Duuh pole...kwanza ni aibu kukaa mule...natamani kujua nyumbani ulibrush vipi
Yaani ilikuwa shemeji akija nyumbani kusalimia nilikuwa sitoki chumbani mpaka anaondoka.
Ila nashukuru Mungu hii ishu ilikuwa siri kati yangu, dada na mmewe (shemeji aliyenisaidia) tu
 
Back
Top Bottom