MENTOR:JINSI YA KUMPATA ATAKAYEKUFAA.
Umeshawahi kuwaza kama ungepata mtu akufundishe Forex? ushawahi kuwaza ingekuwaje mtu anayefahamu kuliko wewe angekuwa anakupa msaada na maelekezo ya jinsi ya kutrade? ushawahi mfuata mtu inbox kumwomba mtu akupe personal classes? ushawahi hisi hauwezi kufikiria vizuri kuhusu strategy gani utumie ili uwe profitable trader, na hivyo unahitaji mtu akupe mwongozo?
kama ndio, basi mtu huyo anaitwa Mentor.
View attachment 713036
bahati mbaya wengi wetu twadhani kila mtu anayejua kuliko sisi anafaa kuwa mentor. hapo ndipo tunapokosea na kupotea. inakuwa kama kumwona mtu ana joho basi twamkamata na kumkabidhi madhabahu aendeshe ibada, kumbe sio wote wenye majoho ni mapadre, wengine masheikh!
Kuna sifa kadhaa za mentor ambazo unapaswa kuzijua kabla hujamuomba mtu awe mentor wako.
1. huo mfano wa mchungaji na sheikh umeuelewa? mentor wako anapaswa kutrade kwa staili unayotrade, la sivyo utajikuta unabadili staili ya kutrade kila ukibadili mentor. kama wewe ni naked trader, tafuta mentor naked trader, kama wewe watumia indicator, tafuta mentor anatumia same indicators... naked hawezi kummentor anayetumia indicator, the same mentor anayetumia indicator katu hawezi kumfunza naked trader... Birds of same feathers........ utamalizia hapo...
2. kama ambavyo fundi makenika wa treni hawezi mwelekeza fundi makenika wa IST jinsi ya kuziba pancha, mentor scalper hawezi kummentor swinger, and vice versa, so kama wewe ni swinger tafuta mentor swinger kama wewe ni scalper, tafuta mentor scalper.
3. ni nzuri pia kama mentor na mentee wakatrade same market, and same pairs.. sio wewe unatrade EURUSD na mentor wako muda wote anatrade Coffee au Orange Juice!
4. kama watumia indicators, ni nzuri mentor atumie same indicators kama umeamua kutumia OG Forex strategy, then mmiliki wa hiyo startegy atakuwa mentor mzuri zaidi... kama unatumia MCV, na ,mentor pia atumie hiyo, hali kadhalika kama watumia moving averages, then mentor wako awe anazitumia hizohizo....
View attachment 713035
5. mentor anapaswa awe na muda wa kukuelekeza, full time trader ni mzuri zaidi, maana anakuwa na uwezo wa kukusaidia wakati wote unapohitaji msaada.
View attachment 713034
6. kitu kikubwa zaidi.... AFFORDABILITY ya mafunzo/mentorship.. kama mtaji wako ni $50, ni hasara sana kutafuta mentor wa $2000.
Kwa maelekezo hayo machache, hope itakuwa rahisi zaidi kumpata mentor, and please note, i dont give mentorship services, mi mwenyewe nahitaji kuwa na mentor!
cheers!