Tuliotembea umbali mrefu kwa miguu kwa sababu yoyote ile tukutane hapa

Binafsi umbali mkubwa kabisa kutembea naamini ni 30km kwenda na 30km kurudi ndani ya siku 2, nilikuwa mdogo sana probably darasa 3 na kwenda ilituchukua kama masaa 9. Cha kushangaza kesho yake wakati wa kurudi, 30 km zile zile ilitugharimu masaa chini ya 5
 
Sipigi fix mzee ni ukweli kabisa nishatembea sana umbali mrefu Hydom - Manyara hadi Babati.

Hata nikiwa Tanzania huwa naamua weekend natembea kutoka Maikocheni hadi Kimara naamua tu na wala sioni umbali wowote
kama kweli umetisha mkuu.
Runzewe kahama ni km 137 ndio maana tunasema sio mchezo, ukisema umefika hadi tinde maana yake umeongeza nyingine 67 umetembea zaidi ya klm 200 mkuu.

uko vzr kama kweli. Ulitumia siku ngapi mkuu.
 
Mnaotumia hili neno km muwa mnajua vipimo vizuri, eti km 100 kwa miguu!!! Weeee acha kbs
hahaha kuna wababe humu wanakatua hadi kilometa 200 mkuu, mia ni kawaida.
Mimi nashangaa miambili kwa sababu ninaowajua wanaokatua zaidi ya kilometer 200 hata humu jf siwezi kutegemea kuonana nao. Wapo wafugaji na wanunuzi wa ng'ombe flani huwa wanaluka vilometer vya kutosha
 
Binafsi nimewahi kutembea umbali takribani kilometer 100.

Ilikuwa ni safari ya kwenda na kurudi na ilinigharimu siku moja ya kwenda na siku ya pili ya kurudi.

ilikuwa nimeelekea msibani na nilikuwa na nauli ya kwenda tu, kwa sababu nikapata company ya mtu ambaye hakuwa hata na hiyo ya kwenda tukaungana na kuanza kupasua pori mdogo mdogo.

Safari ilihusisha kupanda na kushuka milima, mvua ilinyesha na kukatika karibu mara nne ila hatukukata tamaa.

Ninajua watu wametembea kwa miguu umbali mrefu kwa sababu nyingi zikiwemo:
kukoswa nauli
kutafuta kazi
Kuepuka hatari
hakuna namna ya kusafiri
na sababu nyingine nyingi ...

karibu utujuze

Tulikuwa JKT Bulombora. 2ic Major Mzena akaitisha mkutano wa Kikosi kizima jioni moja. Tumefika Conference Hall kikosi kizima kombania zote, tumekaa tumetulia na kombati zetu safi, baada ya roll call, tumekaa chini. Muda Afande Mzena akaingia. Afande RSM Mbilinyi baada ya kumsalimia kwa saluti ya ukakamavu sana, akaanza kumpa maelezo,... AFANDE MBELE YAKO KUNA WAPIGANAJI SO AND SO,... NA SERVICE MEN SO AND SO (RSM akataja idadi).....kumbe 2iC akaona idadi ya watu haiko sawa kulingana na takwimu za kikosi, imekuwa ndogo, akauliza WANGAPI? RSM akarudia tena kutaja idadi aliyoitaja mwanzo. Pale pale Afande Mzena,Aakaamuru kwa kusema "kesho asubuhi saa 12 hapa! Tukaanza kugawanwa tena,.. foleni, foleni,....na hatimaye tukatawanyishwa tukarudi kwenye mahanga yetu. Kesho yake saa 12 asubuhi kikosi kizima safari hii kwa idadi kamili ya watu, kikawa kipo tena mahali pale. Afande Mzena wala hakuonekana tena, akaja msaidizi wake CI Major Mtekele. Alipoingia tu conference room, akatamka maneno haya ROOT MUCH MPAKA NSIMBO, MIMI NITAKUJA NA PAJERO LANGU NINAWAFUATA! I see, Nsimbo iko km si chini ya 40 kutoka Bulombora JKT. Zoezi likabadilika ghafula, ikawa ni root much!. Nikajaribu kutengeneza mbinu niingie kwenye kundi la wapishi, ikashindikana, nikaamua kutoroka kupitia mahanga ya wasichana SERENGETI, nikakutana na msichana anakimbia amevurumushwa huko, ananiambia makanyaga huko kuna MP. I see, tulitembea root much mpaka Nsimbo kwenda na kurudi, km zaidi ya 80! I will never forget that day. Jeshini nilikuwa na tecnik za kukwepa visanga na kwa akili nyingi sana, lakini zote siku hiyo zilikwama!
 
mkuu safi sana.
story nzuri
 
Umbali mrefu nlitembea nlivyokua std 4 toka Upanga primary had knyama. Mambo ya utoto shuleni,rafki zetu boys wenyew nadhani walizoea hyo system so siku hyo wakatushawishi kua tutembee sio mbali n tukakubali! Njian nauli zetu tukanunua karanga safari ikapamba moto.
Nlienjoy njian japo nlifika home nmechoka sana na nakumbuka tukaja kurudia tena kutembea siku nyingne
 
Nilitembea kwa miguu siku England waliposhinda Rugby World Cup. Barabara zilifungwa nilikuwa ninarudi nyumbani nilitembea mbali sana. Kutoka Holborn mpaka Elephant and Castle.
KARIBU SANA HAPO Tube je ?
 
sawa mkuu unakatizia kichangani vipi umbali wake unauonaje?
Mkuu kawaida tu mie mdogo wangu alikuwa akija kunitembelea morogoro enzi nakaa hapo tulikuwa tunazunguka huo mji kwa mguu.Tunaanzia Mazimbu IpoIpo mpaka Town,tunakatiza katikati humo mpaka Nanenane then tunarudi kupitia Msamvu,Muslim University mpaka Ipo Ipo Tunatembea for funny tu.Mdogo mdogo tukifika sehemu tunakaa tunakunywa soda then tunaendelea na matembezi.Nataka nianze huo utamaduni hapa Dar.Trip ya Kwanza Natest Mwenge Lugalo Masana Goba mpaka Mbezi,kurudi napanda gari
 
Jua la dar unalijua vizuri mkuu?

labda upige hizo ruti usiku ila dar hii

Jua litakukwmisha na ukijikaza hata siku 1

kesho utaamka umekua mweusi kama tairi la boxa
 
Jua la dar unalijua vizuri mkuu?

labda upige hizo ruti usiku ila dar hii

Jua litakukwmisha na ukijikaza hata siku 1

kesho utaamka umekua mweusi kama tairi la boxa
Joto ndo tatizo tena msimu kama huu ni hatariiiii sana,kwa hili joto
 
Huwa natamani sana muda wa kutoka kazini nitembee angalau km 5 tu lkn sasa unakuta mtu umechoka joto kali halafu viatu vinasagika balaa labda nifanye utaratibu wa kuwa na nguo za michezo wakati wa kurudi navaa nguo zangu na raba zangu mdogomdogo mpaka home.Nadhani masuala ya dawa za kupunguza kitambi hayatanihusu
 
Back
Top Bottom