Super Sub Steve
JF-Expert Member
- Jul 9, 2011
- 17,287
- 10,702
Dah ni shida sana unaonekana kama mzururajibora hata vibaka utawakimbia,usiku ukikutwa sehemu zngine difender imekubeba.
Dah ni shida sana unaonekana kama mzururajibora hata vibaka utawakimbia,usiku ukikutwa sehemu zngine difender imekubeba.
haswaaaa halafu si unajua nao ndio wanatafuta pesa hivyooDah ni shida sana unaonekana kama mzururaji
umejuaje etiWengi humu waongo. Asilimia 90 waongo
Na kwa Dar hali ya Hewa ndio tatizo kubwa.Isingekuwa joto watu wangetembea sana kwa mguu.Unakuta mtu anatoka Mapipa anaenda Fire au Muhimbili au Kariakoo anapanda gari ile sehemu ni ya kucharaza tu mguuJua la dar unalijua vizuri mkuu?
labda upige hizo ruti usiku ila dar hii
Jua litakukwmisha na ukijikaza hata siku 1
kesho utaamka umekua mweusi kama tairi la boxa
Mkuu mie naona 90% ni wakweli.Ila wanaosema 100km kwa siku moja hawa hapana aiseeee nawaona waongo.Wengi humu waongo. Asilimia 90 waongo
Bila kusahau kwenda mashamba ya kilimo yaliyopo mpakani na kenya hasa kwa wachaga, umbali makadirio km 50 na zaidi kwa baadhi yao.Tuliokulia vijijini kutembea umbali mrefu wala siyo story.
Moja kufuata huduma za kijamii kama hospital, maduka etc
Mbili,kwenda kusaga mahindi vijiji jirani vyenye machine ya diesel.
Kwenda minadani kuuza mazao kilometa kadhaa ili kupata kipata cha familia
Kwa kupitia wapi na wapi mkuu?Nakumbuka nilitembea toka Kirua vunjo uparo kwa babu mzaa baba mpaka Kiraracha,Komalagwe nilipofika pale marangu mtoni nikatamani kurudi
Hivi jamani hili neno ni root much au ni route xxxx... yaani hakuna hata wa kunirekebisha! Kiranga uko wapi? Halafu kuna siku niliwahi kuandika packed badala ya parked na sijamsikia mtu akinirekebishaTulikuwa JKT Bulombora. 2ic Major Mzena akaitisha mkutano wa Kikosi kizima jioni moja. Tumefika Conference Hall kikosi kizima kombania zote, tumekaa tumetulia na kombati zetu safi, baada ya roll call, tumekaa chini. Muda Afande Mzena akaingia. Afande RSM Mbilinyi baada ya kumsalimia kwa saluti ya ukakamavu sana, akaanza kumpa maelezo,... AFANDE MBELE YAKO KUNA WAPIGANAJI SO AND SO,... NA SERVICE MEN SO AND SO (RSM akataja idadi).....kumbe 2iC akaona idadi ya watu haiko sawa kulingana na takwimu za kikosi, imekuwa ndogo, akauliza WANGAPI? RSM akarudia tena kutaja idadi aliyoitaja mwanzo. Pale pale Afande Mzena,Aakaamuru kwa kusema "kesho asubuhi saa 12 hapa! Tukaanza kugawanwa tena,.. foleni, foleni,....na hatimaye tukatawanyishwa tukarudi kwenye mahanga yetu. Kesho yake saa 12 asubuhi kikosi kizima safari hii kwa idadi kamili ya watu, kikawa kipo tena mahali pale. Afande Mzena wala hakuonekana tena, akaja msaidizi wake CI Major Mtekele. Alipoingia tu conference room, akatamka maneno haya ROOT MUCH MPAKA NSIMBO, MIMI NITAKUJA NA PAJERO LANGU NINAWAFUATA! I see, Nsimbo iko km si chini ya 40 kutoka Bulombora JKT. Zoezi likabadilika ghafula, ikawa ni root much!. Nikajaribu kutengeneza mbinu niingie kwenye kundi la wapishi, ikashindikana, nikaamua kutoroka kupitia mahanga ya wasichana SERENGETI, nikakutana na msichana anakimbia amevurumushwa huko, ananiambia makanyaga huko kuna MP. I see, tulitembea root much mpaka Nsimbo kwenda na kurudi, km zaidi ya 80! I will never forget that day. Jeshini nilikuwa na tecnik za kukwepa visanga na kwa akili nyingi sana, lakini zote siku hiyo zilikwama!
Dadeq!Leo nimetembea kutoka Kigogo kituo cha Polisi (First In) mpaka Tabata relini nikanywa Juisi, nikaendelea kutembea hadi Tabata Mawenzi.
Huo umbali mtoto wa kijijini Kila siku anatembea kwenda shule na kurudi
ShikamooKuna siku nilienda kumsalimia bibi . Wakati wa kwenda nilipanda gari, nilishuka kituoni nikatembea kuanzia saa 9alasiri hadi saa 12 na nusu jioni(Sijui ni km ngapi)
Kesho yake tukaondoka saa 12 nasu asubuhi tukafika saa 4 asubuhi
Pia kuna siku nilitembea kutoka mnazi mmoja hadi ukonga banana. Ilikuwa 1987