Tuliotembea umbali mrefu kwa miguu kwa sababu yoyote ile tukutane hapa

Umbali wa kutoka nane nane (morogoro) to Forest hill nadhani wa kazi wa morogoro mnaelewa hiyo distance,nilitembea by ngoko moja moja mpk nafika home.
Huo ni umbali Kama wa kutoka mjini mpaka kihonda magorofani. Watu wanachapa lapa toka mkundi au kiegea mpaka mjini, wengine wanapanda na kushuka hiyo milima ya ulugulu kila siku.
 
Tukiwa shule kipindi cha likizo mm na group langu tulipenda kutembea, toka bihawana hadi dodoma mjini. Tulikuwa tunanunua juice karanga na biskut, mizigo tunapakia kwe gari, sisi tunatembea. It was fun.
 
Raha ya kutembea uwe na kitu mfukoni ( hela), ila kutembea ukiwa huna kitu ni kama mateso flani hivi na safari inakuwa ndefu sana.
 
Mawasiliano-mtoni kwa azizi ally

Nishatembea na rafiki angu maswala ya job hay tunarudi hom naul ipo ndogo tukatembea toka mawasiliano via tandale road,tukapita magomeni tukaibuikia jangwani tukapita kariakoo,karume..veta..,taifa hdi kwa aziz ally ndo tukapandia daladala hpo maan balance ndo ilkua inaruhusu
 
Huku kwetu kuna mze mmoja alitoka arusha moshi kumtafuta kijana wake enzi hzo 1998
 
Nadhani nimetembea saana katika maisha yangu....saana...

Nashangaa kuona watu wanatumia siku nzima kutembea km100.
Ndugu, kumbuka hio ni dar - chalinze. 15yrs ago nilitembea toka airport mpaka kurasini kesho yake niliumwa kabisa na sitoisahau hio siku.
 
mkuu lunzewe kahama sio mchezo kama utupigi fix.
kufika ushilombo tu lazima usizi, ukikomaa sana unaishia masumbwe.
 
Ilikua 2012 natoka gheto tandika nashuka chuo ifm sina nauli ya kurudi cz najua chuo kuna wadau siwezi kosa naul ya kurudi.

Bwana wee.Nafika nakuta maandamo kwenza wizara ya mambo ya ndani kisa kuna wanafunz wa ifm wamelawitiwa kigambon so kuna fujo fujo kidogo pale na ole wako uonekane darasan.

Simu haina vocha so nikashindwa kuonana na wadau wangu.Nikaona isiwe kesi nikaunga maandamano but kabla hatuja fika nikafanikiwa kuchomoka nikaingia POSTA MPYA kwa mguu safari ikaanza kurudi TANDIKA.

Kwa hali ya hewa ya hapa town niliona kama naenda mbinguni.
Nafika pale kamata kkoo akutana na defender ya FFU na gari ya maji ya kuwasha..Nikawaonea huruma sana niliowaacha huko..Walipigwa wakachaa..Kipigo cha mbwa koko walikula.
Ila na mm nilichakaa kwa mwendo
 
Tukiwa shule kipindi cha likizo mm na group langu tulipenda kutembea, toka bihawana hadi dodoma mjini. Tulikuwa tunanunua juice karanga na biskut, mizigo tunapakia kwe gari, sisi tunatembea. It was fun.
mkuu mimi nikiwa na Muwa tu hata afrika nazunguka.
hongea sana, mkiwa wengi kila mmoja anakuwa anajimwambafy hataki kuonekana mnyonge mnaweza kufika mbali.
 
ila tandika posta ukipata shortcut sio shida sana ila tatizo joto najua lazima ufike kama ulikuwa unaongelea swimming.
hayo maandamano nayakumbuka mkuu
 
ila tandika posta ukipata shortcut sio shida sana ila tatizo joto najua lazima ufike kama ulikuwa unaongelea swimming.
hayo maandamano nayakumbuka mkuu
Mm nilikuaga mgen town enz hizo nimekuja tu kusoma so nikanyoonya njia kama daladala.
Ahahahahahh
 
Nakumbuka 2010 mashindano ya CECAFA waliruhusu mashabiki kuingia bure,mim namshikaji wangu tukapanga tuende. Mechi kuisha gari zote zinazotoka Mbagala na Temeke kwenda Mwenge zilikuwa zimejaa na ambazo zilikuwa zinanafasi watu walikuwa wakipanda huku gari bado inatembea. Ikabidi tutembee tu toka huko U wa taifa hadi Mwenge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…