Tuliosoma shule za kata tujikumbushe harakati tulizopitia mpaka kufikia vyuo vikuu na kuwatia moyo wadogo zetu

Halafu haka kausemi ka mwalimu anatoa 25% na mwanafunzi ajitafutie hiyo iliyobaki ndio kalihalalisha walimu kuwa irresponsible na kutofundisha vizuri ilihali wanalipwa
 
Tandika Secondary School.
Aiseee noma ile kuingia form 1 2009 watu shazi mikondo kuanzia A-H daaaah ndo brother wa kitaa akanisanua jinsi ya kutoboa katani. Na mimi sikulemba naamkia mchikichini napiga vitu then nakuja shule kuitikia jina nasepa home mwisho wa siku nikatoboa tu Ndabo now nakula boom tu daadeq
Da mkuu mimi nilikuwa miburani mwaka huo huo hatari sana now napiga md apa udsm na ndio tupo katika pepa tunakaza tu ivo ivo.
 
Watu tumesoma shule za Tarafa kabla ya Shule za Kata kuanzishwa.Nakumbuka mwaka huo tunamaliza katika shuke yetu ambayo ilikuwa watu hawafaulu kwenda A level.Nakumbuka One ya kwanza ilikuwa yangu,halafu wanangu wawili wakapiga two.Mpaka Leo nimewa inspire madogo wengi saana.Shule ya day,bila kunywa chai na kurudi kwa miguu 4km vijana wa kata Shule IPO 0.5km halafu hata credit za Grade IIIA zinakishindaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nimesoma terrat secondary school,
Shukrani zangu za dhati ziwaendee
Mwl Amiri English /history
Mwl sungi Bui English/civics
Mwl Raymond Maplani geography
Mwl Darmian Sumaye kiswahili
Mwl Octavian Ginwe chemistry
Mwl George Ngadada biology
Hawa walimu heshima kwao!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
haikuwa shule ya kata (kiluvya secondary school)

nakumbuka sana life la kupanga gheto watu wa tatu/wanne ili mtoke kimaisha

nakumbuka kwenda kupiga msuli msitu alafu unatafuta undugu na montress (nikajiongeza) ili aweke tiki kama nipo skul kumbe sijatokea kama siku tatu


da nakumbuka siku nikiwa skul head master kajakunitafuta kumbe hanijui kaita jina class me nikakausha, si dogo mmoja kajakunichomoa back_bencher et "ticha huyu hapa" daa! nilipigika kinoma SITASAHAU

sem ndo hivyo kila mtu anatoka kivyake mda wa mapindi nilikuw nipo makini na mda wa usumbufu nimesumbua kweli bila kusahau matwiti kwa wingi

sema sifa kujiongeza na kuacha ujinga!!!!!
 
Daah, nyie achen tuu wana sisi skuli kwetu idadi ya walim walikua kama 7 mwalim wa physics mmoja tuuu,, hatukua na mwalim wa hesabu,,, yaan tumeingia form one January tulikua tunasoma masomo ya arts tuu pekee ila sayansi (biology, chemistry and physics) hata definition zao hatujui ,,ilikua hali ngumu sana kupata elim ,,ila fimbo tulikua tunachezeshewa sio kidogo,,, watu walianza kupata akili ya kujitafutia matirio na twisheni Huko nje ya shule,, tulikua tuna ushindan mkubwa darasan kwetu na wanafunz sisi kwa sisi ndo tulikua walim,, kila siku mtu anaejua topic flan anaenda mbele anafundisha na wanafunz wanakaa kumsikiliza,, ki ukweli tulipambana sanaa,, na hatimae mtihan wa kidato cha nne 2010 tulifaulu wanafunz 30 kujiunga na kidato cha tano,, yaan tulimake history na haijawah kutokea mpk leo hii,,
(Mbugani sekondar school- mwanza)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah klerruu sec , picha linaanza natokea second selection , naingia form 1, mwez wa 4 baada ya kuwa mchunga ng'ombe na mbuzi, naingia kwa kuchelewa lkn mtihan wa mwez wa 6 nafaulu kwa wastani, nakaza sana ,form 2 natoboa japo nakuwa mtoro wa kiwango cha juu, naanza kuwa nashinda library kichangani misheni ya roman , naanza kuyapenda masomo ya sayansi, kemia ,physics yananikubali , hesabu inanikataa, kwakuwa form 1 topic hazikuuisha, na sina hela za twisheni, form 2 nakaza, necta hesabu napata D, chemistry B physics C ,history B Geo B, nayakumbuka haya,

Nakaza hatimaye form 4, nafaulu kwa division 2 ya 21, huku nikiwa mtoro kupindukiwa hata graduation sikwenda, shukran kwa shule niliyosoma ,Practical tulifanyia kwenye maabara za chuo cha ualimu cha klerruu, naenda A level PCM , shule ya kata ndio tunakuwa wa kwanza kuianzisha, yaan ni mpya, ila shukran maabara ipo na ni mpya, ila changamoto za walimu kama kawa, nakuwa mtoro kupindukia had nataka kufukuzwa shule, walimu wanakuwa wavivu hawamalizi topic, nasoma msuli yatima, tukifunga likizo wwnzangu wanaenda dar kwakina mudy, mkandawile na wengineo ,mimi huyo home iringa, napiga,msuli peke yangu sebulen na barid ya iringa, maana mtaani aliyefaulu kusoma PCM ni mimi pekee, nafikia mahala nakuwa nakata tamaa, lakini nakaza, mwisho wa siku nafaulu KWENDA UDSM , hiyo 2013

Maisha ya shule ya kata yamenifunza mengi ,

NAMSHUKURU ALIYELETA WAZO LA SHULE ZA KATA MAANA NINGEBAKI KUWA MCHUNGA MBUZI,
Jembeee mzee baba kama mm vile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom