Kwanini walimu wa vyuo vikuu wanakuwa ni watu wenye ufaulu wa juu sana tofauti na walimu wa shule za msingi na sekondari?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Mimi mdogo wenu wa mwisho (last born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu;

Kwanini walimu wa vyuo vikuu wanakuwa ni watu wenye ufaulu wa alama za juu sana katika masomo yao (GPA kubwa) tofauti na walimu wa shule za msingi na secondary ilhali huku chini kabisa ndio nguzo muhimu ya kujenga wanafunzi bora?

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba kuna mtoto mmoja wa shangazi yangu (jina kapuni) alihitimu kidato cha sita mwaka jana na kupata ufaulu hafifu wa division 3 ya mwisho kabisa.

Baada ya wazazi wake kushindwa kumudu kumlipia ada ya kujiunga na chuo kikuu kwa ufadhili binafsi watu wanamshauri KWANINI ASIOMBE HATA UALIMU kauli ambayo huwa inanikera sana nikilinganisha na mfumo unaotumiwa na vyuo vikuu wa kupata walimu wao kwa kubakisha wanafunzi wale wenye ufaulu wa alama za juu sana.

Kwanini mtu akipata ufaulu hafifu anashauriwa aombe walau ualimu? Kwani ualimu ndio kimbilio la watu walioshindwa shule?

Kwanini kuna hali kama hii? What's the logic/rationale behind all this?

NB: TUENDELEE KUWA WAZALENDO NA TUIPENDE TANZANIA KWA MAANA USTAWI WA NCHI YETU UNAANZIA KWANGU MIMI PAMOJA NA WEWE
 
kwani wa vyuo vikuu ulishasikia wameenda chuo kwa ajili ya kufundisha chuo kikuu?
Walimu wa primary pamoja na secondary huenda vyuo vya ualimu kufundishwa teaching skills pamoja na psychology. Kwa hiyo unataka kuniambia mtu akimaliza chuo kikuu tayari anakuwa na teaching skills pamoja na kujua students' psychology?
 
Nadhani hao kwa vile ni kama marobot na wanatakiwa wapate PhD (Permanent Head Damage) na ni wajuzi wa NADHARIA hivyo uwezo wao wa kuandika na/au utafiti inasemakana ni mkubwa. So kama atakuwa na hako ka-GPA kadogo huenda asifae!!nawaza tuu
 
Umeuliza swali la msingi kabisa. Penye pesa ndipo panapopiganiwa. Zamani ilikuwa waalimu wa shule za msingi walikuwa wenye ufaulu mkubwa lakini mambo yamebadilika siku hizi waalimu hawalipwi vizuri hivyo thamani yao imepungua na serikali inawalipa kiduchu.
 
Brother umebugi.

Kwa mjibu wa mfano wako.

Huyo jamaa yako ndio kamaliza form six kapata division three.

Huo ualimu wa shule ya msingi au sekondari kautoa wapi? Wakati bado hajahitimu chuo.

Hiyo GPA unayoisema ndogo kaitoa wapi?

Hujui huyo huyo aliyepata division three, advanced level, akifanya vizuri chuo kikuu anakuwa mwalimu wa chuo kikuu?
 
Naomba nichangie kidogo hapo kwa mada yako mtoa uzi.Kuna ndugu yangu alipata three ya mwisho ya 25 form four ,akaamua kuanza na certificate ,akaenda soma deploma ,akasoma degree na kupata GPA 4.1 baadae akasoma masters na sasa hivi ni mhadhiri chuoni.Sasa wewe unachoongea hapo ni matokeo ya taaluma yaani form four na form six.

Mwalim wa primary naenda chuo kwa divsn three na anasoma cherti anapata GPA ya 4 but ataenda kufundisha hiyo primary hatabakizwa eti awe mkufunzi wa kufundisha walim kisa GPA kubwa.Akiwa amemaliza form six akapata D moja na E moja atakuwa na vigezo vya kusoma deploma ya ualim na huko atapata GPA ya 4.4 but hatabaki pale kuwa mkufunzi chuoni.Atarudi afundishe secondari kulingana na elimu yake ya deploma.

Lakini mwanafunzi akiwa na D mbili form six ataenda kusoma chuo kikuu na akipata GPA ya 4.5 anaweza bakizwa kusoma masters na akawa mhadhiri msaidizi na akisoma PHD anakuwa mhadhiri kamili.Kwahyo mtu anaweza kuwa mhadhiri chuo kikuu akiwa na three form four na three form six.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi pia nilipenda kada ya ualimu ilindwe na iwe yenye masharti makali katika kudahiliwa na mchakato mzima, kama wanavyojaribu katika fani za udaktari, japo si kote.
Ila changamoto ninayoona ni malsahi pia serikali hii na zijazo hamna yenye uthubutu wa kuwekeza pesa nyingi kwenye elimu.

Elimu yetu bado ina mapungufu mengi sana kuanzia ngazi ya chini mpaka ya juu kabisa, na njia pekee ya kuinasua ni PESA PESA PESA.

Tunaweza kuleta hoja nzuri na zenye tija lakini utekelezaji wake mtaji ni PESA.

Nahitimisha kwa kusema hivi Elimu yetu itakuja kuwa nzuri siku Tanzania itakapokua nchi tajiri vinginevyo generation 20 zijazo bado watakua wanajenga matundu ya choo.
 
Mkuu usiwe subjective, amini usiamini, kuna wahadhiri hawajawahi kupata dvn one wala two ya kidato chochote.

Wapo wengine pamoja na GPA kubwa walizonazo, hawaeleweki, hawezi kukufundisha ukamuelewa.

Pia, kuna kada nyingi zingine zinawaajiriwa wenye vyeti vibovu zaidi kuliko walimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfumo ni mbovu sana wa kudahili walimu wa chuo kikuu kwa sababu wao wanaangalia GPA tu na sio knowledge lakin nimeambiwa na mwalimu wangu wa chuo kuwa siku hizi wanaangalia na knowledge ukiwa nayo kubwa kama una GPA by rote learning basi hutopata nafasi.

Lakini pia mwanafunzi wa chuo hasa cha ualimu masomo mengi anayofundishwa ya kufundishia mfano hesabu ya chuo sio hesabu ya sekondari wala msingi.Ila inakusaidia ukitaka kusoma Master's level.

Wale waliochanganua sentensi za kiingereza by x-bar ukimchanganulia mwanafunzi wa sekondari lazima wakimbie somo.
Cha kufanya naona wangerecruit vijana wenye high knowledge wafundishe chuo kikuu bila kuweka GPA kama kigezo cha kwanza.Mfano Wanafunzi wote wenyw GPA kuanzia 3.0 wanauwezo mkubwa na knowlege.sawasawa na mwenyewe GPA 4.4.
Kuna wana wanaelezea vitu kwa uzuri sana mpaka unaelewa lakini ukiwauliza wana GPA 3.2 wakati wewe unaeelekezwa mara mbilimbili na mwenyewe GPA ndogo unakutuka una GPA 3.9.Wale ma group leader wanaoeleza vizuri sana kwenye magroup ya chuo huwa wao ndo wanakuwa na GPA ndogo kuliko wanaowaelekeza.Mwingine domo zege halafu GPA juu. Atafundisha nini?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilitaka kuchangia lolote, lakini nimejionya kuwa napaswa kubaki msomaji tu.
 
Back
Top Bottom