Tuliosoma mchikichini tution tukutane hapa tukumbushie vituko tulivyokutana navyo

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,276
6,585
15622617_366985523654560_7775518281308552515_n.jpg



Dah ngoja me nianze aisee...

Tukiwa class kwa mudy physics tulikuwa na utaratibu wa kuuliza maswali kwa kuandika kikaratasi halafu unampa wa mbele yako naye anampa wa mbele mpaka kinafika ubaoni kwa mudy then anasoma swali lako kwa sauti kubwaaa kila mtu asikie.Hahahahah umo tulikuwa watu zaidi ya mia nne tunakula pindi la electronics aisee huku nikiwa nimekaa mlangoni na mrembooo mzuri balaaaaaaa.

Nilikuwa nimevalia T-shirt yangu nzuri ya kupendeza niliyovaa kuwakilisha chama langu la home "Kwa Temba " UKONGA lililoandikwa "LUNDUNO THE INK".

Sasa kuna mdau mmoja humo class akanisoma nilivyo kuanzia nywele mpaka shati langu kisha akaandaa kikaratasi ili aanze kuulizwa swali

Dah sitasahau kabisa Namna ile karatasi ilivyokuwa inasomwa huku watu wote wakiniangalia mimi aiseee huku nikibaki naona aibu huku natabasamu.Muuliza swali aliamua kabisa kunikomoa na alifanikiwa kabisa maana mimi ndio nilikuwa TOPIC baada ya kipindi kuisha

Muuliza swali aliandika hivi :

"Mudy,mimi ni handsome niliyevaa T shirt ya LUNDONO THE INK nyeusi hapa mlangoni,sio siri Mudy nimeamua tu kusema ukweli maana hapa sielewi chochote tangu unaanza.Huyu mrembo niliyekaa nae ananichanganya kabisa akili maana hili paja aliloniwekea sidhani kabisa kama sitapiga bao hapa.Hivyo mudy nakuomba uniombee nafasi hapo mbele nije kukaa japo hata nielewe dakika hizi za lala salama maana hapa usalama hakuna".

Muddy aliniita nikakae mbele na ndio nikaona nafuu japo sikuuliza swali ila amenisaidia sana,nikainuka kwenda mbele huku watu wote wakiamini kuwa mimi ndio niliandika maana nilikuwa naenda kukaa mbele kwa furaha kabisa huku watu wakinipigia makofi na kunishangilia

Dah kwa waliosoma kwa mudy wanaijua sauti yake akiwa anasoma karatasi kama hivi maana anasoma kwa sauti kubwaaaa na bass kidogo kiasi kwamba kila mtu anasikia.Dah wakati anasoma darasa lote linaniangalia mimi huku wanacheka.Namimi nikajikuta natabasamu tu :):):):).Baada ya kipindi nikapokea mambo kibao kutoka kwa mademu na washikaji kibao wakanifuata kunipa hongera ya kujilipua

Hahaahah hata GOBORE Kauzu ila kesho yake akaniruhusu nisome bure.Gobore ni jamaa fulani hivi ana mdomo mweusi na sauti mbaya kuliko ya teja.Sasa usiombe Gobore akudake umezamia pindi :):):)

Huyu Gobore anasifa ya kwenda kulinda amani huko KONGO

Sitasahau siku hii aiseee:D:D:D:D:D:D
24174604_919010924941067_8315084492446551893_n.jpg



Je unakumbuka nini mdau wa mchikichini mwenzangu enzi hizo?

=======

THE TIME IS ALMOST APPROACHING TO ZERO,LET US END HERE TODAY AND TOMORROW WE WILL SEE HOW TRANSISTOR WORKS
 
aisee ile mihogo ya pale mchikichini ilikuwa kibokoo...

kusimama nje ukichelewa unakuta watu nyomi,

kubalance muda wa pindi la physics, geograph, chemistry na math aisee unakuta watu wanakimbia speed za hatar uku wanaruka mitalo ya maji machafu hahaha....yale sio maisha kabisa aisee
 
aisee ile mihogo ya pale mchikichini ilikuwa kibokoo...

kusimama nje ukichelewa unakuta watu nyomi,

kubalance muda wa pindi la physics, geograph, chemistry na math aisee unakuta watu wanakimbia speed za hatar uku wanaruka mitalo ya maji machafu hahaha....yale sio maisha kabisa aisee

Mkuu kule ni sawa na kambi ndogo ya mafunzo ya Kijeshi.Kuna ule uchochoro wa kutoka kwa HIDDEN AGENDA kwenda kwa MBUGA aiseeee.....

Kuna sehemu unapita kunyata juu ya mawe huku chini maji ya kijani yametulia kama nyasi
 
Hahaahahahahaha nilikua napenda kusikia muddy akijibu mapigo ya mgote
Mudy aliulizwa kama ni kweli alisoma na mtata PRIMARY akajibu yesss nilisoma nae yule kilaza.Mimi darasani nilikuwa wa kwanza nikifuatiwa na dada mmoja hivi sijui yuko wapi....Anaendelea hivi yule mtata kwa jinsi alivyokuwa na sura mbaya hivi ana demu kweli yule?????

Dah long aiseeeee
 
Mudy aliulizwa kama ni kweli alisoma na mtata PRIMARY akajibu yesss nilisoma nae yule kilaza.Mimi darasani nilikuwa wa kwanza nikifuatiwa na dada mmoja hivi sijui yuko wapi....Anaendelea hivi yule mtata kwa jinsi alivyokuwa na sura mbaya hivi ana demu kweli yule?????

Dah long aiseeeee
Hahaha alikua anampatia kwelikweli yani anajibu vijembe vya mgote by the way pindi lilikua linaenda fresh sana big up Muddy phy popote alipo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom