Tuliosoma chuo tukatoka patupu tukutane

Mkuu mimi nilisoma ka digirii ka computer Data Science chuo Fulani hivi hapo nchi jirani, kati ya wakufunzi watano waliokuwa wanatufundisha 4 walikuwa wanakuja kazini wakiwa tiyari wamepiga vyombo kichwani. Mimi niliambulia labda 30% ya elimu iliyokusudiwa. Nimetoka pale nimehangaika for 2 yrs kutafuta ajira bongo, jamaa mmoja akaniambia mimi ninamiliki shule ya computer studies kariakoo nakupa laki 2 kwa mwezi unapiga darasa mara nne kwa siku unasemaje? nikamwambia poa, Jamaa alichokifanya alinikabidhi vitabu vikubwa vya computer na ka ofisi kangu kadogo kama nyumba ya panya akanitupia na syllabus ya shule akaniambia piga msasa na huku ukifanya practical na utatumia computer hii (computer mbovu mbovu hivi na yazamani sana). Hapo ndio nilipoanza hasa kujua computer ni nini na inatumika vipi
 
Chuoni ni mahali pa kujifunza sio kulishwa kama kinda la ndege!!

Ama kweli mlienda shule kusomea ujinga!
 
Kozi za kitaalam kama IT, Computer science na engineering ni lazima upate wakufunzi waliobobea ili na wewe uwe bora, haya mambo ya kumwambia mtu ajifunze mwenyewe ilhali mambo ni mengi muda mchache ni kuumizana tu.
 
Wewe ni kilaza, usie jitambua na wanaokusapoti ni vilaza vilevile.Chuo kikuu sio mahala pa kufundishwa kama darasa la kwanza bali ni sehemu ya kujifunza.Ukiwa chuo lazima ujitambue vinginevyo utaona maluweluwe tu.GURU wa İt duniani wamejifunza komputer science hawakufundishwa na mtu.Wenzio walisoma tu vitabu vya komputer science wakaunda na programu za komputer, mfano Elon mask aliunda computer game kwa kusoma tu vitabu sembuse wewe na mwalimu ulikua nae, wanafunzi wenzio nk.Ni ajabu kusikia mtu analalama kuwa mwalimu wake sio mahili hali ana smart ya kisasa ambayo ina internet ambapo kuna lecture mbalimbali, kuna vitabu vya kila aina.Udhaifu wako usiwe lawama kwa wengine'Self defensive mechanism'.Najiuliza tu ukisoma open university utamlaumu nani?.
hahahha ngoja nikucheke kwanza, mkuu hizi kozi ya computer kama huna uelewa wa kujiongeza utaishia patupu, mimi nikiwa field mwaka wa kwanza (IT) nilienda chuo X aisee sitosahau nilifika nikaunganishwa na wanafunzi wa palepale wao walichagua kufanyia field pale chuoni kwao, walikuwa na PROJECT ya kutengeneza FILE TRACKING SYSTEM imagine wao pia ni mwaka wa kwanza kami mimi ila wamesoma mambo mengi balaa kama C, C++, PYTHON, RUBY, PASCHAL, PHP, SQL, HTML, CSS na bado wanaweza kufanya mpk network hacking ya pale chuoni kwao.

eeeh bwana wakaniuliza umesoma Language zipi nikasema HTML na CSS walinicheka then wakaniuliza kwanini hujui nikasema hatujafundishwa hvyo vingine ilibidi nianze kupigwa pindi la hatari, baadae sana ndio wanasema wana mwalimu wako ni hatariii kubwa huwa anawafundisha vitu vingi vya ziada.

kwahiyo basi wakufunzi wanachangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kutoka kapa hata hao wanasoma OPEN wanatafuta wakufunzi nondo usijidanganye eti wanajisomea wenyewe home lazima wana wakufunzi nondo sana...

Baada ya kurudi chuo aisee nilionekana ni waya ya stima mpk baadhi ya wakufunzi wakashangaa nimepigwa msasa wa aina gani huko nilipokuwa.
 
aailimia nyingi ya wanafunzi wa chuo hawaelewi hata chuoni wanafanya nini , wanalinda heshima ya wao kuitwa wasomi machoni kwa wanajamii ila ndani hamna kitu
 
Pole sana...

Darasani ni sehemu ndogo sana, ujuzi unaupatia kwa juhudi zako kwenye maisha ya baada ya chuo...

Huko ndiyo unakutana na vitu ambavyo, unaweza jiuliza chuo nilienda kufanya nini...

Cc: mahondaw
 
Wakuu habari? Mimi mwenzenu nikiri wazi kuwa nilisoma chuo kikuu cha Taifa cozi ikiwa ni Computer Science lakini nilitoka half cooked sikuwa nimeiva kabisa na hii ikanipa wakati mgumu sana kwenye kusaka ajira.

Sababu:
Waalimu wengi waliokuwa wakitufundisha walikuwa wanatufundisha katika mfumo wa kutukaririsha zaidi kuliko kutufanya tuelewe na kulifurahia somo. Kama vile walikuwa wakitukomoa na kututishia ku-sup, niliishia kukariri ili nisifeli au kupata alama za chini.

Tunafundishwa mambo mengi kwa wakati mmoja tena ndani ya semister moja mnaweza kuwa na cozi zaidi ya 6 main, hivyo mwisho wa siku unajikuta unakariri zaidi badala ya kuelewa.

Ukosefu wa vitendea kazi kama laptop nayo ilikuwa tatizo kwasababu vifaa kama computer ni lazima, Computer lab ya chuo ilikuwa hoi computer nyingi zikiwa mbovu na hakukuwa na utaratibu maalum wa wanachuo kuzitumia zile zilizopo.

Walimu wetu kuwa shallow baadhi walikuwa wanatufundisha vitu ambavyo hata wao wenyewe hawavijui mpaka nikawa najiuliza hivi wamefikaje pale? unakuta mtu anakufundisha programing let say Java halafu hata yeye mwenyewe haijui na hakuambii utaiapply wapi?

Maisha magumu wakati mwingine Boom linaisha, pia wakati mwingine lilikuwa linachelewa sana kutoka hivyo kunifanya kuwa na wakati mgumu wa kufuatilia masomo halinikiwa na njaa, muda mwingi nilikuwa nautumia kuwaza nimpigie nani simu nimpige kizinga.

Mpaka unafika mwaka wa tatu nagraduate nilikuwa najiuliza nimevukaje na vipi nagraduate halikuwa hata kuprogram "Hellow world!" sijui ndio ikawa hivyo. Mambo mengi nimejifunza baada ya kumaliza chuo ikiwemo website designing na PC mainternace.

Hizi changamoto ulizoainisha hapa zipo almost kila mahali, sio Tanzania tuu.

Mimi nimefanya Computer Networking na Telecom na nilibahatika kusoma nje pia.Kozi ni nyingi hivyo hivyo nilikua naingia darasani saa 08h15-13h00 na 14h00-18h00 wiki nzima ....Kwa mtazamo wangu kazi nilijifunzia kwenye kampuni kipindi cha internship na baadae nikiwa kazini.

Nakumbuka tulikua na mwalimu wa Java/Java EE kichwa sana ila yeye alikua hawezi kutuelewesha.Yaani darasani tunaona kabisa alivyo kichwa ila mkihoji hawezi kuwaelewesha na kila mmoja wetu aliona hivyo ......

Networking/Telecom ni kozi yenye mambo mengi sana na kazi zipo nyingi ambazo zinatofautiana sana.Yaani leo tukikutana maclass mate na kila mmoja akaanza kuelezea kazi yake kiundani unaweza ukadhani hamkusoma darasa moja kwani utakua na uelewa wa juu juu sana kuhusiana na anachofanya.

Hivyo nadhani uzoefu/kubobea ni kazini na sio chuoni.Chuoni tunapewa hints tuu na academic principles.
 
Wakuu habari? Mimi mwenzenu nikiri wazi kuwa nilisoma chuo kikuu cha Taifa cozi ikiwa ni Computer Science lakini nilitoka half cooked sikuwa nimeiva kabisa na hii ikanipa wakati mgumu sana kwenye kusaka ajira.

Sababu:
Waalimu wengi waliokuwa wakitufundisha walikuwa wanatufundisha katika mfumo wa kutukaririsha zaidi kuliko kutufanya tuelewe na kulifurahia somo. Kama vile walikuwa wakitukomoa na kututishia ku-sup, niliishia kukariri ili nisifeli au kupata alama za chini.

Tunafundishwa mambo mengi kwa wakati mmoja tena ndani ya semister moja mnaweza kuwa na cozi zaidi ya 6 main, hivyo mwisho wa siku unajikuta unakariri zaidi badala ya kuelewa.

Ukosefu wa vitendea kazi kama laptop nayo ilikuwa tatizo kwasababu vifaa kama computer ni lazima, Computer lab ya chuo ilikuwa hoi computer nyingi zikiwa mbovu na hakukuwa na utaratibu maalum wa wanachuo kuzitumia zile zilizopo.

Walimu wetu kuwa shallow baadhi walikuwa wanatufundisha vitu ambavyo hata wao wenyewe hawavijui mpaka nikawa najiuliza hivi wamefikaje pale? unakuta mtu anakufundisha programing let say Java halafu hata yeye mwenyewe haijui na hakuambii utaiapply wapi?

Maisha magumu wakati mwingine Boom linaisha, pia wakati mwingine lilikuwa linachelewa sana kutoka hivyo kunifanya kuwa na wakati mgumu wa kufuatilia masomo halinikiwa na njaa, muda mwingi nilikuwa nautumia kuwaza nimpigie nani simu nimpige kizinga.

Mpaka unafika mwaka wa tatu nagraduate nilikuwa najiuliza nimevukaje na vipi nagraduate halikuwa hata kuprogram "Hellow world!" sijui ndio ikawa hivyo. Mambo mengi nimejifunza baada ya kumaliza chuo ikiwemo website designing na PC mainternace.

Bora wewe una vyeti vyako halali. Mimi hapa nilipo muda huu sina kazi na wala sina vyeti ila natafuta vyeti vya kufoji vya chuo kikuu ili nikatafutie kazi. Kama unawajua walio navyo, tafadhali naomba unipe taarifa.
 
Vyuo binafsi vinafundisha wanafunzi zaidi ya vyuo vya Umma. Basically, ufundishaji wa vyuo binafsi ni kama ule wa sekondari kwasababu wanafunzi wa kule ni wa iana fulani hivi (pengine hawana msuli sana kama wa vyuo vya Umma), lakini vyuo vya Umma wanafunzi kwa seheum kubwa wanajiongeza wenyewe. Wakati fulani niliwahi kuwa nafundisha vyuoni, binafsi na vya Umma. Bidii zaidi unaweka vyuo binafsi, kwasababu wana control quality na unalipwa. Huku kwenye vyuo vyetu vya kawaida (Umma) ni business as usual, ila kwa sasa sijui utaratibu ukoje, nimetoka kwenye hiyo game zaidi ya miaka 5 iliyopita.
 
Mkuu mimi nilisoma ka digirii ka computer Data Science chuo Fulani hivi hapo nchi jirani, kati ya wakufunzi watano waliokuwa wanatufundisha 4 walikuwa wanakuja kazini wakiwa tiyari wamepiga vyombo kichwani. Mimi niliambulia labda 30% ya elimu iliyokusudiwa. Nimetoka pale nimehangaika for 2 yrs kutafuta ajira bongo, jamaa mmoja akaniambia mimi ninamiliki shule ya computer studies kariakoo nakupa laki 2 kwa mwezi unapiga darasa mara nne kwa siku unasemaje? nikamwambia poa, Jamaa alichokifanya alinikabidhi vitabu vikubwa vya computer na ka ofisi kangu kadogo kama nyumba ya panya akanitupia na syllabus ya shule akaniambia piga msasa na huku ukifanya practical na utatumia computer hii (computer mbovu mbovu hivi na yazamani sana). Hapo ndio nilipoanza hasa kujua computer ni nini na inatumika vipi
Mkuu nataka nijenge uelewa mpana wa computer kuanzia kwenye word, niombe uniambie namna ya kupata nondo muhimu, PC ninayo.
 
Back
Top Bottom