Troubleshooter
Senior Member
- Mar 30, 2016
- 103
- 95
Wakuu habari? Mimi mwenzenu nikiri wazi kuwa nilisoma chuo kikuu cha Taifa cozi ikiwa ni Computer Science lakini nilitoka half cooked sikuwa nimeiva kabisa na hii ikanipa wakati mgumu sana kwenye kusaka ajira.
Sababu:
Waalimu wengi waliokuwa wakitufundisha walikuwa wanatufundisha katika mfumo wa kutukaririsha zaidi kuliko kutufanya tuelewe na kulifurahia somo. Kama vile walikuwa wakitukomoa na kututishia ku-sup, niliishia kukariri ili nisifeli au kupata alama za chini.
Tunafundishwa mambo mengi kwa wakati mmoja tena ndani ya semister moja mnaweza kuwa na cozi zaidi ya 6 main, hivyo mwisho wa siku unajikuta unakariri zaidi badala ya kuelewa.
Ukosefu wa vitendea kazi kama laptop nayo ilikuwa tatizo kwasababu vifaa kama computer ni lazima, Computer lab ya chuo ilikuwa hoi computer nyingi zikiwa mbovu na hakukuwa na utaratibu maalum wa wanachuo kuzitumia zile zilizopo.
Walimu wetu kuwa shallow baadhi walikuwa wanatufundisha vitu ambavyo hata wao wenyewe hawavijui mpaka nikawa najiuliza hivi wamefikaje pale? unakuta mtu anakufundisha programing let say Java halafu hata yeye mwenyewe haijui na hakuambii utaiapply wapi?
Maisha magumu wakati mwingine Boom linaisha, pia wakati mwingine lilikuwa linachelewa sana kutoka hivyo kunifanya kuwa na wakati mgumu wa kufuatilia masomo halinikiwa na njaa, muda mwingi nilikuwa nautumia kuwaza nimpigie nani simu nimpige kizinga.
Mpaka unafika mwaka wa tatu nagraduate nilikuwa najiuliza nimevukaje na vipi nagraduate halikuwa hata kuprogram "Hellow world!" sijui ndio ikawa hivyo. Mambo mengi nimejifunza baada ya kumaliza chuo ikiwemo website designing na PC mainternace.