Tulioshuhudia vituko kwenye mabasi ya mikoani tukutane hapa!

Nakumbuka siku moja nilipanda basi maarufu la Morogoro toka Ubungo kwenda Moro. Pale Ubungo walipanda familia moja hivi walikuwa na mgonjwa wamemtoa Mwananyamara hospitali wanampeleka Mikese ambapo ni kwao kwa mujibu wa maongezi yao kwenye simu. Walikuwa mwanamke (ambaye ni mke wa mgonjwa) watoto wadogo wawili (nahisi ni watoto wa mgonjwa na kaka ya mgonjwa. Walichukua siti ya nyuma yote. Yule mgonjwa alikuwa hajiwezi kabisa na walimuingiza kwenye gari kwa kumbeba. Mwanzoni mwa safari alikuwa akiongea kwa shida sana na kuna kipindi alikuwa anapigiwa simu yake ambapo mkewe alikuwa anapokea na baadae kumpa aongee na waliompigia ingawa alikuwa anaongea kwa shida na vitu visivyoeleweka na alikuwa mkali sana kwa mkewe pindi akimwuliza kitu.

Mie nilikaa siti moja toka ile siti yao ya nyuma hivyo nilikuwa nausoma mchezo wote kwa ukaribu sana. Tulisafiri huku yule kaka yake mgonjwa akiwa amemlaza mgonjwa mapajani kwake akiwa amekaa kwenye siti na mke wake akiwa pembeni ya yule mgonjwa. Tulipokuwa tunakatiza maeneo ya Vigwaza jamaa si akaanza kutoa miguno ya ajabu baadae akaanza kunyoosha miguu huku akisukuma siti yetu, alikuwa akikata roho. Yule mke wake alitaharuki akaanza kulia jamaa (kaka) akamtuliza kuwa avumilie ili wafike Mikese so akanyamaza. Hapo wale watu wote wa siti za karibu tumetulia tunajiuliza ni nini hiki kimetokea.

Tukaendelea na safari mpk baada ya kufika maeneo ya Bwawani, yuke kaka yake mgonjwa akawa anawapigia simu watu wao ambao walikuwa wameshawapanga toka wanapanda kuwa waje kumpokea mgonjwa pale Mikese kuwa wakodi hiace jamaa hali imebadilika sana na waende msikiti wa karibu waazime mkeka.

Tulipofika mizani Mikese jamaa akaenda kuongea na dereva na kisha abiria wote tukaombwa kushuka jamaa wakaingia na kanga na mkeka wakashusha mwili ukaingizwa kwenye hiace tukaendelea na safari.

Tukio lile lilinipa hofu sana juu ya kifo maana niliuona mchezo wote live pale nyuma.
 
Hahahahaha, alijipulizia KURUTHUM nini mkuu?
mwingine tulifika njian akatoa elf 10 akachukua soda ya buku yule muuza soda akasema ngoja nikatafute chenchi (sjui ndo hivyo) eeh mara gari likasepaaaa aiseee nilimuonea hurumaaa sana
 
  • Thanks
Reactions: mij
Nakumbuka siku moja nilipanda basi maarufu la Morogoro toka Ubungo kwenda Moro. Pale Ubungo walipanda familia moja hivi walikuwa na mgonjwa wamemtoa Mwananyamara hospitali wanampeleka Mikese ambapo ni kwao kwa mujibu wa maongezi yao kwenye simu. Walikuwa mwanamke (ambaye ni mke wa mgonjwa) watoto wadogo wawili (nahisi ni watoto wa mgonjwa na kaka ya mgonjwa. Walichukua siti ya nyuma yote. Yule mgonjwa alikuwa hajiwezi kabisa na walimuingiza kwenye gari kwa kumbeba. Mwanzoni mwa safari alikuwa akiongea kwa shida sana na kuna kipindi alikuwa anapigiwa simu yake ambapo mkewe alikuwa anapokea na baadae kumpa aongee na waliompigia ingawa alikuwa anaongea kwa shida na vitu visivyoeleweka na alikuwa mkali sana kwa mkewe pindi akimwuliza kitu.

Mie nilikaa siti moja toka ile siti yao ya nyuma hivyo nilikuwa nausoma mchezo wote kwa ukaribu sana. Tulisafiri huku yule kaka yake mgonjwa akiwa amemlaza mgonjwa mapajani kwake akiwa amekaa kwenye siti na mke wake akiwa pembeni ya yule mgonjwa. Tulipokuwa tunakatiza maeneo ya Vigwaza jamaa si akaanza kutoa miguno ya ajabu baadae akaanza kunyoosha miguu huku akisukuma siti yetu, alikuwa akikata roho. Yule mke wake alitaharuki akaanza kulia jamaa (kaka) akamtuliza kuwa avumilie ili wafike Mikese so akanyamaza. Hapo wale watu wote wa siti za karibu tumetulia tunajiuliza ni nini hiki kimetokea.

Tukaendelea na safari mpk baada ya kufika maeneo ya Bwawani, yuke kaka yake mgonjwa akawa anawapigia simu watu wao ambao walikuwa wameshawapanga toka wanapanda kuwa waje kumpokea mgonjwa pale Mikese kuwa wakodi hiace jamaa hali imebadilika sana na waende msikiti wa karibu waazime mkeka.

Tulipofika mizani Mikese jamaa akaenda kuongea na dereva na kisha abiria wote tukaombwa kushuka jamaa wakaingia na kanga na mkeka wakashusha mwili ukaingizwa kwenye hiace tukaendelea na safari.

Tukio lile lilinipa hofu sana juu ya kifo maana niliuona mchezo wote live pale nyuma.
Duh! so sad aisee.
 
Wanaume huwa ni majasiri sana kaka akamkumbatia mdogo wake huku akijikaza asilie lkn mke alishindwa akaanza kulia

Poleni sana aisee
 
Yote ya yoteeeee! Usiombe ukabanwa na tumbo la kuhara ukiwa safarini kuelekea mikoani
 
Kuna siku nilisafiri kutoka Mwanza to Dar kwa bus la Isamilo, mama mmoja alibanwa na mkojo , alipoomba kuchimba dawa, fuse zikawa zishakatika akaumwagia mlangoni abilia tukishuhudia mishanga ya kiunoo.
 
Hawa masista duu was kwenye mabasi ni wa hovyo sana.
Mwaka Jana mwezi wa sita natoka Dodoma kuja dar siti ya pembeni yangu alikuua demu flani mweupe kisu kinyama nikasema saaafi, leo Nina bahati. Sasa bwana picha linaanza ndani ya gari Luna joto lakini yeye kapigilia jacket la mvua Kubwa kinoma, hadi nikawa namuonea huruma, nikamwambia si uvue Tu hilo dude,akalivua.
Tumefika Moro kanunua mahindi ya kuchemsha akanigawia na Mimi, ile napeleka mdomoni, yakikuwa yamechacha nikaacha kula lakini yeye alikuwa anayapeleka balaa, sasa nikakawa najiuliza yeye hahisi kuwa yameharibika?
Sasa alikuja kuniua mbavu kuna jamaa alikuwa anauza mbuzi (ya kukunia Nazi) akaniuliza ile nini nikamwambia kuwa hicho ni kifaa cha kukunia Nazi, eti akanijibu mbona kimekaa kama msalaba eti anakiogopa.

Nikavaa headphones nikalala.
Hahahahahhahahahhaa
 
Back
Top Bottom