Tiketi mtandaoni kwenye Mabasi ya Mikoani bado changamoto

Very poor

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
347
509
Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Kazi iendelee,

Mimi ni Moja ya wazalendo ninayeunga juhudi zinazofanywa na serikali yangu chini ya Rais wangu.

Niingie kwenye mada husika niliyolenga kuileta hapa jukwaani kuhusu usafri wa Mabais ya kwenda mikoani, bado kuna changamoto sana kwa abiria tunaopendelea kukata ticket mtandaoni.

Moja ya changamoto ninayoiona mimi ni pale umekata ticketi mfano gari Company ya Dar Kwetu, gari inapofika unapanda kondakta unamwambia nimekata tiketi mtandaoni anaanza kushangaa na kukuuliza pesa ipo wapi, inabidi uanze kutoa shule tena!

Pili, unaingia kwenye gari siti uliyoikata unakuta ina mteja mwingne tayari.

Ushauri wangu kwa wamiliki wa mabasi wawaeleweshe wafanyakazi wao jinsi ya kutumia hii mifumo Ili kuepuka usumbufu.
 
Back
Top Bottom