Tulioonewa na kufungwa na serikali

billionaire17

Member
Mar 31, 2017
31
43
Miaka miwili iliyopita yalinipata haya kwa sababu ya kusupport UKAWA.
Sikuwahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha kisiasa ila niliamini katika MABADILIKO YA UKAWA

Nilijitahidi sana kuwaelimisha watu juu ya uhitaji wa mabadiliko Pasipo kuvunja sheria.

Kilichotokea siku moja usiku tuliingiliwa na watu watano wakiwa na silaha na sare za kipolisi, wakatukamata kimyakimya nikiwa na rafiki yangu tuliekuwa tukiishi naye hapa jijini mwanza.

Walianza kwa kusema wamepigiwa simu na wananchi wema kuwa tunatengeneza kemikali.

Wakaingia ndani kwa nguvu hawakukuta kiashiria chochote cha hicho walichodai kemikali.

Ajabu wakatupakia kwenye deffender mpaka Central Police Mwanza,
Cha ajabu kingine walikataa tusimjulishe mtu yeyote hata ndugu juu ya ukamataji wetu.Tuliwekwa sero week nzima.

Siku ya tano usiku alikuja mkuu wa kituo na kuuliza "wale vijana wa chadema wako wapi?" Tulikaa kimya kwani tulijua labda miongoni tuliopo sero kuna wanachadema wamekamatwa, la hasha! kumbe alikua akimaanisha ni sisi.

Akatuita kwa majina, tulishangaa sana, tukamuuliza mbona wakati mnatukamata mlisema tunatengeneza kemikali? Sasa mmetubatiza jina vijana wa chadema, pia kuwa chadema ni kosa kisheria? Tulimuuliza kwa upole tukitaka msaada wa kutoka sero.

Akatujibu "Mbowe yupo nyumbani kalala usingizi nyie mpo huku sero mnaliwa na mbu" tulishangaa kwani maswali na majibu hayaendani.Tulirudishwa sero.

Asubuhi yake tulikua na hasira sana tukaanza kupiga kelele angalau ndg zetu wajulishwe kuwa tupo kituoni, baadae wakatupeleka mahakamani na wakaja na vibobo vimejaa liquid flani wakidai ni ushahidi wameupata.

Case iliendelea baada ya kupewa dhamana na mahakama na hivi karibuni mahakama ikatuachia maana hakuna case ya kujibu.

Najua si sisi yaliyotupata haya, kama na wewe ulipatwa na haya share nasi.

Maisha yanaendelea niliathirika sana kisaikolojia, nilipoteza fedha nyingi katika case na kilichoniuma sikuwahi kuwa mfuasi wa CHADEMA ila niliunga mkono mabadiliko
Nimerudi nyuma kimaisha na kimaendeleo kwani mnajua case ni ugonjwa mbaya sana.

Nipo namuomba mungu anipe nafasi niweze kulipa kisasi kabla sijafa na kupotea kabisa.

Mtanisamehe siyo mzuri kudeliver story.
 
"Wale vijana wa CHADEMA wako wapi?"-Mkuu wa Kituo. Kimsingi, nchini kunajengeka tabia kuwa yeyote mwenye mawazo tofauti ya Serikali au ya CCM ni CHADEMA. Huu ni uminyaji wa haki ya kutoa maoni kwakuwa tupo tusio na vyama. Kwanza, hapa Tanzania hakuna CCM na CHADEMA tu.
 
"Wale vijana wa CHADEMA wako wapi?"-Mkuu wa Kituo. Kimsingi, nchini kunajengeka tabia kuwa yeyote mwenye mawazo tofauti ya Serikali au ya CCM ni CHADEMA. Huu ni uminyaji wa haki ya kutoa maoni kwakuwa tupo tusio na vyama. Kwanza, hapa Tanzania hakuna CCM na CHADEMA tu.
Mkuu huwa nakuona sana Unajihusisha na Siasa na Ni mfanyakazi wa UDSM. Chagua Moja you will end up in disasters!
 
Watu wanaonewa sanaana kusingiziwa ma kesi makubwa ya uongo ndio kazi wanayoijua zaidi polisi wa Tanzania waonevu upeo wao mdogo!! Wengi wameiba vyeti sio vyao hope less
 
Mkuu huwa nakuona sana Unajihusisha na Siasa na Ni mfanyakazi wa UDSM. Chagua Moja you will end up in disasters!
Kakosea nini? Mwakyembe, Kabudi, Kitila, hawa vipi? Hawakua wafanyakazi WA UDSM? Acheni utemi nyie, mnahati miliki ya hii nchi?
 
Back
Top Bottom