Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

Mwaka jana nililima tikiti hekari mbili maeneo ya ruvu yalistawi vizuri sana ila yakiwa yamebakiza wiki moja niyavune lahaula naamka asubuhi nakuta mto ruvu umefurika shamba lote lipo ndani ya maji.

Miguu iliisha nguvu nikajikuta nimekaa chini hata sijui nilikaaje, kuna mzee pale kijijini akaniambia nisikate tamaa msimu wa mvua utakua umewahi, akanipa shamba lake lenye ukubwa wa hekari tatu na nusu ambalo lipo mbali kidogo na mto akaniambia lima bamia.

Ikabidi nivunje kibubu ili nipate hela ya kulimia, mbegu na mbolea hiyo ilikua mwezi wa 11 mwaka jana, hadi kufikia mwezi wa tatu mwaka huu mavuno ya bamia yakawa yamenirudishia mtaji na kafaida kidogo.

Hapa nilipo nimelima shamba lilelile lililonizamishia matikiti mwanzoni tena nimeliongeza limekua hekari nne.

Baada ya kufanya tathmini niligundua kua pamoja na msimu wa mvua kuwahi kama alivyoniambia mzee lakini pia nilichelewa sana kupanda maana nakumbuka nilipanda mwezi wa nane nikiwa na matarajio mvua itaanza mwezi wa 11 mwishoni ambapo nitakua nimeshavuna.

Changamoto za shamba zipo ila uwezekano wa kuzikabili upo mkubwa tu, changamoto ambazo sizijui niza sokoni kwa upande wa tikiti japokua nafanya utafiti wa hapa na pale.

Nitakuja kuleta mrejesho mwezi wa 9.
Mrejesho TAFADHALI?

#YNWA
 
Mimi nililima hekari 40 za mpunga Ifakara (signal). Nilitumia milioni kumi lakini nilikuja kuvuna gunia 14 tu. Na hizo gunia 14 ndiyo pesa ya vibarua; mfano kukata, kukusanya, kupiga kupepeta, kununua viroba. Kwa ufupi ziliishia humo tu.

Niliambulia kupata gunia moja la mpunga nikakoboa nikapata mchele kilo 70. Kesho yake nikapanda basi kurudi Dar Nikawaletea chakula tu kilichopatikana. Nipo Ilala nawaza bora ningefungua duka la spea, ILA YA MUNGU MENGI.
Muongo wewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom