Tuliofurahia maumivu ya Sabaya ndio tunaomlilia Mbowe na kuiingilia Mahakama

Hakika siku zinakwenda mbio sana na ,ni siku chache sana zimepita toka lile kundi lililojawa furaha isio kifani baada ya aliekua mkuu wa wilaya ya Hai, Sabaya, kupandishwa mahakamani, tabasamu lilikuwa kama lote na Rais Samia kupongezwa na kuambiwa anaupiga mwingi mno.

Ghafla kibao kimegeuka ,Mama Samia kawa mbaya, na anapewa shutuma kibao na wanaomlilia Mbowe, ambaye anatuhuma za kupanga ,kufadhili ugaidi nchini.

Hakika hakuna aijuae dakika moja ijayo kwenye maisha yetu, utulivu ni jambo jema, tusiwe wepesi wa kufurahia madhila ya wenzetu ikiwa sisi hatuijui kesho yetu.

Mwisho, wahenga walinena "Mkuki mtamu kwa nguruwe, kwa binadamu ni mchungu"
This thread is a round peg in a square hole. You cannot compare a thug to a just person.
 
Tunaujua udhaidu wa wafuasi wa chadema,huwa na kawaida ya kukimbia maswali magumu.
Labda ni kweli, lakini siyo maswali yako, mkuu Mkorinto! Sina nia ya kukushusha kwa vyovyote, Lakini kama walivyo Mataga wengi, Wewe ni mwepesi sana kichwani!
 
Labda ni kweli, lakini siyo maswali yako, mkuu Mkorinto! Sina nia ya kukushusha kwa vyovyote, Lakini kama walivyo Mataga wengi, Wewe ni mwepesi sana kichwani!
Nyumbu wengi mnaamini nyinyi pekee ndio wazito kichwani,huu nao ni ugonjwa mbaya.ndio maana wananchi wanawapuuza.
 
Aliyemshauri mama amkamate Mbowe akutamkia mema,kamuingiza mkenge.Amezungukwa na mafisi
 
Kulinganisha uonevu na Makosa Ni kukufuru mbele za Mungu. Mbowe Hana kosa Bali Sabaya amejaza Makosa Hadi darini hivyo acha watu waonyeshe hisia zao
 
Mbowe na genge lake walifurahia sana kukamatwa kwa Sabaya, kifupi akifikiri kuwa sasa atakuwa free kufanya lolote bila kuwa na mtu wa kumdhibiti. Alichosahau au kutokukijua Mbowe ni kwamba Sabaya alikuwa anajua mambo mengi ya Mbowe kupitia kwa wapambe wake, lkn hakutaka kuweka kila kitu wazi kwa sababu ya utu wake. Sasa kitendo cha Mbowe kushangilia kukamatwa kwake ndio kuliko fanya Sabaya na yeye amwage mboga.
1628420592331.png

Enzi za utoto na ujana wetu, mlio adimu wa ndege huyu ulikuwa kiashiria chema cha kuja mvua. Siku hizi sauti yake yasikika hovyo hovyo tu
 
Back
Top Bottom