Tuliofurahia maumivu ya Sabaya ndio tunaomlilia Mbowe na kuiingilia Mahakama

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
8,256
9,085
Hakika siku zinakwenda mbio sana na ,ni siku chache sana zimepita toka lile kundi lililojawa furaha isio kifani baada ya aliekua mkuu wa wilaya ya Hai, Sabaya, kupandishwa mahakamani, tabasamu lilikuwa kama lote na Rais Samia kupongezwa na kuambiwa anaupiga mwingi mno.

Ghafla kibao kimegeuka ,Mama Samia kawa mbaya, na anapewa shutuma kibao na wanaomlilia Mbowe, ambaye anatuhuma za kupanga ,kufadhili ugaidi nchini.

Hakika hakuna aijuae dakika moja ijayo kwenye maisha yetu, utulivu ni jambo jema, tusiwe wepesi wa kufurahia madhila ya wenzetu ikiwa sisi hatuijui kesho yetu.

Mwisho, wahenga walinena "Mkuki mtamu kwa nguruwe, kwa binadamu ni mchungu"
 
Nikuulize swali hili; pale Mlimani Calvary au Golgota walikuwa wamesulubiwa wangapi? Unadhani umati uliokuwa umekusanyika pale ulikusanyika kwa ajili ya nani? Mambo rahisi hivi huelewi, makubwa utaelewa kweli?
 
ni ushahidi mwingine kuwa kumbe tupo tupo tu; hatujui tunaelekea wapi wala tunataka nini. yapo mengi sana ya kutafakarisha kuhusu hawa jamaa lakini ngoja nijipigie kimya tu. nilimuona mama mmoja jana pale kisutu (kupitia tv lakini) akijigalagaza chini huku akiwaambia polisi, ''niueni, niueni tu lakini mbowe lazima aachiwe sitoki hapa!'', nilisikitika kweli kwa maajabu haya ya kipumbavu!
 
Tunasubiri ushahidi wako mahakamani kuwa mbowe nishahidi maana Kwa sabaya tunaona watu wanatoa ushahidi wadhahiri kabisa kahiyo karibu mahakama kuu tar.13
 
Tusubirie ushahidi tuone,walio toa ushahidi kwa sabaya ni viongozi wa CCM na wanachama wake,upinzani walifura vipi ikiwa mshitaki na mashahidi ni Wana ccm?Mlalamikaji wa kesi ya sabaya ni serikali ya ccm, tutapigana mpaka mbowe awe huru msitake kutuchezea mbuzi wakijani nyiee!!!!
 
Hakika siku zinakwenda mbio sana na ,ni siku chache sana zimepita toka lile kundi lililojawa furaha isio kifani baada ya aliekua mkuu wa wilaya ya Hai,Sabaya, kupandishwa mahakamani ,tabasamu lilikuwa kama lote na Rais Samia kupongezwa na kuambiwa anaupiga mwingu mno ,kibao ghafla kimegeuka Mama Samia kawa mbaya na anapewa shutuma kibao na wanaomlilia Mbowe, ambaye anatuhuma za kupanga ,kufadhili ugaidi nchini .
Hakika hakuna aijuae dakika moja ijayo kwenye maisha yetu, utulivu ni jambo jema,tusiwe wepesi wa kufurahia madhira ya wenzetu ikiwa sisi hatuijui kesho yetu.

Mwisho ,wahenga walinena "mkuki kwa nguruwe ,kwa binadamu ni mchungu"
Toka mumeo Meko amefyekwa na Corona ndio umezidi kuwa pumbavu kabisa wewe Mama.
 
Mbowe na genge lake walifurahia sana kukamatwa kwa Sabaya, kifupi akifikiri kuwa sasa atakuwa free kufanya lolote bila kuwa na mtu wa kumdhibiti. Alichosahau au kutokukijua Mbowe ni kwamba Sabaya alikuwa anajua mambo mengi ya Mbowe kupitia kwa wapambe wake, lkn hakutaka kuweka kila kitu wazi kwa sababu ya utu wake. Sasa kitendo cha Mbowe kushangilia kukamatwa kwake ndio kuliko fanya Sabaya na yeye amwage mboga.
 
... nikuulize swali hili; pale Mlimani Calvary au Golgota walikuwa wamesulubiwa wangapi? Unadhani umati uliokuwa umekusanyika pale ulikusanyika kwa ajili ya nani? Mambo rahisi hivi huelewi, makubwa utaelewa kweli?
Swali la kijinga sana
 
ni ushahidi mwingine kuwa kumbe tupo tupo tu; hatujui tunaelekea wapi wala tunataka nini. yapo mengi sana ya kutafakarisha kuhusu hawa jamaa lakini ngoja nijipigie kimya tu. nilimuona mama mmoja jana pale kisutu (kupitia tv lakini) akijigalagaza chini huku akiwaambia polisi, ''niueni, niueni tu lakini mbowe lazima aachiwe sitoki hapa!'', nilisikitika kweli kwa maajabu haya ya kipumbavu!
Mkuu ukisikia wendawazimu ndio huo,yaani huyo eti anau uchungu sana na Mbowe kuliko mkewe na wanae na hatukuwaona frontline
 
Tunasubiri ushahidi wako mahakamani kuwa mbowe nishahidi maana Kwa sabaya tunaona watu wanatoa ushahidi wadhahiri kabisa kahiyo karibu mahakama kuu tar.13
Unanipangia ?,ni suala la muda tu ,mtatafuta pa kujificha,hatubaatishi safari hii
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya mashtaka ya sabaya na mbowe.usifikiri watu ni wajinga sana wanashindwa kutofautisha kesi za hao watu wawili na matendo yao.
Brainwashed mind,yaani gaidi ni nafuu kuliko jambazi,swine
 
Back
Top Bottom