Tuliochaguliwa UDOM tukutane hapa

Tuliochaguliwa UDOM tukutane hapa

Niwapongeze wote mloweza kuchaguliwa Chuo kikuu cha dodoma,ni nafasi ya pekee kwani kipindi hiki kumekuwa na ushindani mkubwa wa kupata nafasi vyuon hasa vyuo vya serikali kutokana na mazingira,ada,ubora wa elimu n.k!
Kama mwanafunzi mwenzenu (4th year,Bsc Petroleum engineering) nilowatangulia ni vyema kuwapa ushauri/mwanga kidogo kabla hamjaripoti na kuanza masomo.
"UDOM" ni chuo kichanga ambacho kinaendelea kukua kadri siku zinavyokwenda,Kuna changamoto nyingi zinazokikabili chuo ambazo kwa asilimia kubwa zimepungua kwani chuo kilivyo kwasasa ni tofauti na kipindi kinaanza.Hata sifa mbaya zilizokuwepo miaka ya nyuma kwasasa hazipo tena,imekuwa ni moja ya kimbilio kubwa la wanafunzi kuomba nafasi.
Nini cha kufanya uweze kuzikabili changamoto zilizopo
1.KUSOMA KWA BIDII
Kumbuka jambo la msingi linalokupeleka chuo ni kusoma hivo jitahidi sana kusoma kwa bidii.Chuo kina ukosefu mkubwa wa "lecturers" hasa kwa kozi za sayansi(engineering) hivyo juhudi binafsi inahitajika sana kuhakikisha unasoma vitabu vingi,tumia sana mtandao kwa lengo la kujifunza.
Uzuri wa chuo mwalimu(lecturers) anakupa "course content" ambayo inaonyesha "topics" zote unazotakiwa kuzisoma katika kila "semester" hivyo ni vyema kuhakikisha unaipitia,chochote ambacho mwalimu hakukifundisha/hukukielewa vizuri unatafuta vitabu zaid uweze kuelewa!Kumbuka mwalimu anakupa 25% ilobaki ni jukumu lako,usiishie kusoma "notes",vitini vya mwalimu tu!
Ubora wa mwanafunzi pindi umalizapo chuo hutokana na wewe mwenyewe kujibidiisha kumlaumu mwalimu au chuo hakutakusaidia
2.JINSI YA KUISHI CHUONI
Tofauti na ulivyokuwa sekondari,chuon mtu uko huru kufanya lolote hakuna wa kukuonya!Hivyo ni vyema kuhakikisha unafwata kilichokupeleka pale achana na makundi mabaya,starehe na mambo mengine ambayo yanaweza yakakufanya ukashindwa kumaliza chuo(ku disco) au kumaliza chuo na matokeo mabaya!
Uzuri wa UDOM wanafunzi wote mnaishi ndani ya hostel za chuo na chuo kimejitenga kidogo na mji hivyo una mda mzuri wa kusoma na kujichanganya na wenzako kusoma pamoja!Tena ni vizur zaid ukimaliza usajili wakat wa kupewa chumba uishi na wanafunzi walokutangulia mwaka(2,3,4,5) uweze kupata ushauri kutoka kwako kwani wanakuwa na uzoefu zaid ktk masomo,Ukiona tabia zao sio nzuri ni vyema kurudi kwa "warden" akubadilishie chumba!

Naamini hayo hapo juu ndo ya msingi zaid japo yapo mengine mengi mtakayokutana nayo mkifika huko
MAZINGIRA YA CHUO
Chuo kwa ujumla ni kizuri na kikubwa,Naweza kusema kwa Tanzania hakuna wanafunzi wanaoishi vizuri na wenye mazingira mazuri ya kusoma chuon kama UDOM,madarasa ya kutosha,huduma mbalimbali kama maduka,benki n.k vinapatikana ndani ya chuo!Kila college inakila kitu chake inajitegemea "cafeteria,library","dispensary",hostel,maduka,ATM machines n.k!
Maji ya Dodoma sio mazuri kwani yana magadi hivyo maji ya kunywa inakubidi uwe unanunua ya kwenye madumu ya lita 5/10(Uhai) yanapatikana maduka ya chuo!Maji kwa ajili ya matumizi menngine kidogo yanasumbua kwa baadhi ya "colleges" hivyo ni muhimu kuwa na vyombo vya kutosha kuhifadhia maji pindi yanapokatika uwe una akiba chumban kwako!
Hayo ni baadhi tu ya mambo yaliyopo chuo,mengi utakutana nayo ukifika!

Kwa maelezo zaidi unaweza kunitafuta kwa namba 0753651270,0656759802
 
Jaman Hv Hyo Tution Fee Kwa Sisi Wa Special Diploma Tunalipiwa Na Selikali Au Mwanafunzi Mwenyewe
 
Jamani Msaada umu ndan kuhusu tuition fee inakuaje kwamba tunalipa sisi bado cjaelewa naomben ufafanuzi pleaz
 
Karibuni tubadilishane mawzo huku tukisubiri siku ya kwenda chuo

Naomben mxaada wa haraka jaman pleaxe, hivi joining instruction inapatikana xehem gan wakuu? maana nimefanikiwa kufungua 2 adimition letter bado cjajua joining na document zingne znapatikana wp!! MXAADA JAMAN
 
Naomben mxaada wa haraka jaman pleaxe, hivi joining instruction inapatikana xehem gan wakuu? maana nimefanikiwa kufungua 2 adimition letter bado cjajua joining na document zingne znapatikana wp!! MXAADA JAMAN

kumbe admission letter na joining ni tofauti?
 
Msiwe na wenge vijana...hata mkikosa joining instructions kwa sasa utapata tu ukiwa chuoni..joining instructions na medical form huwa haina complications kama ya admision letter, kama unayo admission letter ni vizur maana hiyo ndo utambulisho wako pale chuoni...
 
Wakubwa hii bachelor of Education in Early Childhood education kaz zake ni zipi ? au kufundisha watoto?
 
Jaman nisaidie eti kulipa ada za udom mpaka kwenye benk za chuo au hata kwenye benk za huku nyumbani unaweza kulipia mana kuna mtu ameniambia unalipia kwenye benk za pale chuo wakat huo huo admssion letter inasema tufike chuo tareh 31 tukiwa na payment slip sasa mimi nashindwa kuelewa tunalipia kwenye benk za huku huku kupitia account zao au inakuaje kwani account zao za udom si zinatumika mikoa yote hapa Tanzania au?
 
Jaman nisaidie eti kulipa ada za udom mpaka kwenye benk za chuo au hata kwenye benk za huku nyumbani unaweza kulipia mana kuna mtu ameniambia unalipia kwenye benk za pale chuo wakat huo huo admssion letter inasema tufike chuo tareh 31 tukiwa na payment slip sasa mimi nashindwa kuelewa tunalipia kwenye benk za huku huku kupitia account zao au inakuaje kwani account zao za udom si zinatumika mikoa yote hapa Tanzania au?

unalipia ukiwa nyumbani ila kwenye account ya chuo kama ilivyoandikwa .ni kwa crdb na nmb
 
Back
Top Bottom