Tulinusurika nae kifo, namtafuta Sospeter Wambura Masagi

nzalendo

JF-Expert Member
May 26, 2009
10,949
10,377
Huyu rafiki yangu tulipotezana nae (2005) akiwa katika matibabu kwa shemeji yake Tabora (shemeji yake ni Dr. Hospitali ya Kitete, jina limenitoka).

Dada yake ni mwl. shule ya Viziwi Tabora. Toka kipindi hicho sijapata taarifa yake yoyote, nimeona bora nijaribu kumtafuta huku.

Huyu jamaa tulivamiwa na majambazi katika machimbo madogo ya dhahabu maeneno ya Muzani.

Ndanindani, majambazi walikuwa na silaha nzito na Kiswahili chao lafudhi ya Kikongo ''leo tutabhauwa'' tulinyang'anywa kila kitu tulichokuwa nacho, jamaa yangu kwa uchungu na kutokukubali akawa mbishi. Aisee walimpiga na kitako cha AK 47 kwenye ugoko, sauti ilitoka kama vile shoka linakata mti.

Sitosahau, tuliteseka sana na majeraha ya kutosha manake tulichapwa kama vile wanasafisha/ wanafyeka shamba, eti tutoe dhahabu daaah! Mungu wangu.

Tulilia sana aisee na kumwomba Mungu, usicheze na kifo (jamani mdomo wa kifo unatisha). Kesho yake usubuhi tukapata msaada wa Polisi na kwenda kutibiwa Hospitali ya wakimbizi Lukole (Ngara).

Tulikaa pale kwa wiki mbili mpaka tulipopata msaada wa mawasiliano toka kwa dada yake na kuanza safari ya Tabora. Mie hali yangu iliendelea vizuri, Sospeter alifungwa muhogo mguuni nikamwacha pale akiendelea na matibabu. Mie nikaenda nyumbani kutambikia mizimu.

Kwa yeyote anayemfahamu huyu ndugu tafadhali anijuze. Kaka yake alikuwa ni Operator mgodi wa Buhemba, naye jina limenitoka.

Nashukuruni sana.
 
Back
Top Bottom