Hembu advise mlitaka afanyeje??
Alitakiwa ayafanye haya anayoyapigia kelele saiv (rejea hotuba yake ya kwenye Kigoda cha mwalimu)
Alitakiwa ajenge uwezo wa Watanzania badala yake akabeba bango kuwatukana.
Alitakiwa kuwajengea Watanzania morali kwa kuwashehenesha na maono yake, badala yake hadi leo hamna mtanzania masikini aliyependa na kunufaika na utandawazi.
Tuache kulewa na ujasiri wa simba katika kuunguruma wakati katafuna watoto wake, watu wengi "makini" wanayumba na ujasiri wa Mkapa katika kujenga hoja na kuchambua current issues matokeo yake wanabebwa na huruma katika kuchambua Uongozi wake!
Ila sio Mimi.
Kwangu Mkapa ataendelea kuwa Mpuuzi fisadi kama walivyo mafisadi wengine tu tena ye namtunukia ukinara na uasisi wa ufisadi mkuu wa pili wa taifa hili (ukiwaondoa wale wa kwanza walioua Azimio la Arusha)....
Nyie mnaobeba bango la Mkapa mtuambie ni kwa kiasi gani amejenga taifa la "JUJITEGEMEA"?! (achilia mbali ujamaa)
Je mnakumbuka kuwa alikiri kwa kinywa chake kuwa "alikisahau kilimo"??
Sasa tumuweke wapi huyu mtu??
Nini yalikuwa maono yake juu ya hili Taifa??
Mnaomtetea kuhusu ubinafsishaji ila ye kashindwa kujibu maswali ya Shivji kuwa ubinafsishaji wa njia kuu za uchumi kama BIMA na BANKS ilikuwa ni kulipeleka taifa golgota!!
Namalizia kwa kusema kuwa tusijipe moyo kwa kuangalia matapishi yaliyo na afadhali, matapishi ni matapishi tu sababu yote ni najisi kwa utakatifu wa Taifa,
hili taifa halijawahi kuwa na KIONGOZI toka mwaka 1985!