No matter what, I still believe on Mkapa's capacity. Hv kwa khali ya mashirika ilivyokuwa yalikuwa yakisurvive kwa ruzuku ya serikali.mishahara ilikuwa 3yrs watu hawajapata mishahara. Serikali haipati kodi unadhani yangekuwa wapi leo hiii??
Na hayo mnayosema yalikuwa yanaenda vizuri mlitaka nayo yaishe ndo tukumbuke kubinafsisha?? Nadhani we need to use our common sence to analyse situations badala ya kupiga kelele. Hembu advise mlitaka afanyeje??
Mkapa huenda alikuwa ni 'right person' kwa kipindi kile baada ya kuwa na hali ngumu ya maisha. Serikali inakopa tu huku na huku na chachu ya uchumi haipo. Kama mlihudhuria au kuona kwenye TV mdahalo wa siku ya kigoda cha Mwalimu Nyerere, kwa maneno unashawishika kama Mkapa anao uwezo wa kiuchumi wa kujitahidi katika kuielekeza TZ mahala fulani. Anao mwono wa nini kifanyike. Tatizo la Mkapa ni Mkali mno kiasi kwamba wenye mawazo wanaseza kusita kusema wakihofia kufokewa. Kwa sera ya kubinafsisha kuna madudu ndiyo lakini hakukuwa na njia ya kutoka pale, tayari kulikuwa na makosa ya kiutawala katika kila sekta inayotuhusu utadhani waliowekwa katika mashirika yale walikuwa wamerogwa. Siwezi kusahau jinsi ATC ilivyokuwa inafika Ujerumani (enzi hizo Boeng 737) nzuri kweli kweli halafu wanaamua kwenda kukaa mahotelini marubani na maafisa wa ndege halafu abiria wanafika wanakuta kibao tu kwamba safari imefutwa. Hata wakaandika katika vitabu vya 'tourists guide' kuwa 'never board ATC, always delay, always cancellation' wakati huo huyu NUNDU alikuwa mshirika katika ufundi wa ATC oneni CV yake.
Kwa upande mwingine na sisi wa-tz tujaribu kuwa wakali katika kurasimisha ardhi tulizo nazo vijijini ili tuzitumie kuomba mikopo benki na tuanzishe ujasiriamali kuweza kuajiri wenzetu (yaani wa bongo wanaowakilishwa kwenye bendera ya taifa kwa maana wengine hawamo - zijue vizuri rangi za bendera yetu na maana yake. Mi ninachojua ni kwamba rangi nyeusi ndiyo inayowakilisha watu wa nchi hii kwa hiyo kama wengine wamo ni waliodandia basi lisilolao ila kwa sababu linasafiri basi watakuwemo tu...ila si wakugawiwa viwanda vyetu kama inavyofanywa sasa n.k)
Baada ya Mkapa angekuwa Salimu Ahmed Salimu akahujumiwa na wazanzibari wanaowakilishwa kwenye bendera ya nchi yetu...akaingia mheshimiwa mwenzetu...ndipo balaa likawa kubwa zaidi...mfumko tusisingizie mtikisiko wa uchumi kuna shida katika serikali yetu na katika maisha yetu sisi wabongo...tulione hili na tulifanyie kazi.
Way forward: Kila mtanzania alipo akatae kwa nguvu zake zote kutoa rushwa kwa yeyote hata hospitalini, bora kufa ili vizazi vijavyo vikute Tanzania nzuri, kila mtanzania atumie sanduku la kupigia kura na kulinda kura kwa kumchagua anayeona anasifa za kutokuwa fisadi, na kila mtanzania anyanyuke bila woga na kusema popote atakapoona ufisadi hata kama ni serikalini, shirika la umma, kanisani, msikitini, dukani kwako, uwanja wa mpira, darasani n.k Tutafika kama tukiamka, tukiendelea kulala tutaamka tukiwa hatuna Tanzania bali wakimbizi wa ndani ya Tanzania. Viva M4C