Tulia Ackson: Wanaotaka Kugombea Ubunge Jimbo la Mbeya Mjini Wapime Kina Cha Maji

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,485
7,927
Mbunge wa Mbeya mjini kupitia CCM, Dkt. Tulia Ackson amesema lengo la kugawanya jimbo la Mbeya mjini ni kusogeza huduma kwa wananchi na mchakato huo sio wa Mbeya pekee. Dkt Tulia aliongea hayo wakati akihojiwa na kituo cha redio cha wasafi leo asubuhi.

Tulia amesema ubunge wake yeye haijalishi kama jimbo litagawanywa ama halitagawanywa, amedai kama alimtoa mtu(Sugu) kata zikiwa 36 ataweza kumtoa kata zikiwa chache? Alihoji mbunge Tulia.

Tulia amesema anaona akijadiliwa na wao inawapa sifa na katika mambo ambayo amasema huwa anayafurahia ni kujadiliwa hivyo ameupenda mjadala unaoendelea.

Tulia amesema wanaosema watamfuata amefurahi, anataka wajipime na kama wanaona kina cha maji kinawatosha wamfate.

Tulia amesema hata zikibaki kata 36 anawafyeka

Kwa msaada wa mwendazake. Tulia hana ushawishi wa wapiga kura hata ndani ya CCM ni anabebwa na mfumo tu

Tulia Trust Foundation inayomilikiwa na Tulia Akson ilifanya kazi kubwa sana kumuandalia mazingira ya ushindi spika wa bunge, kina mama walipata mikopo ya bila riba, vijana wa Mbeya walipewa bajaj na bodaboda za mikopo nafuu za kutosha

Tulia hakubebwa alijijenga vizuri mpaka leo Mbeya inamuimba vzr Tulia nenda kajionee
 
Mbunge wa Mbeya mjini kupitia CCM, Dkt. Tulia Ackson amesema lengo la kugawanya jimbo la Mbeya mjini ni kusogeza huduma kwa wananchi na mchakato huo sio wa Mbeya pekee. Dkt Tulia aliongea hayo wakati akihojiwa na kituo cha redio cha wasafi leo asubuhi.
...
Tulia bila wizi wa kura ulioratibiwa na yule mwovu wa chato asingeweza kupata ubunge.
 
Tulia Trust Foundation inayomilikiwa na Tulia Akson ilifanya kazi kubwa sana kumuandalia mazingira ya ushindi spika wa bung, kina mama walipata mkopo ya bira riba, vijana wa Mbeya walipewa bajaj na bodaboda za mikopo nafuu za kutosha

Tulia hakubebwa alijijenga vizuri mpaka leo Mbeya inamuimba vzr Tulia nenda kajionee
Unadanganya kwa faida ya nani? kama sio msaada wa JPM hakuna namna angeshinda lile jimbo. Hana mvuto wa kisiasa, na Kwa Sasa ndio kaharibu zaidi maana bunge kaliendesha vibaya kiasi imekua eneo la kumpongeza Rais badala ya kuibana serikali.

Hiyo 2025 sioni namna Gani atarudi Tena labda JWTZ ije na vifaru kutisha wapiga kura.
 
Kipimo cha Tulia ni wingi wa kata, kwamba ana hakika kata zikiwa chache pia lazima ashinde, vipi kama nyingi ya kata zitazobaki ni zile zilizompa ushindi Sugu?

Au alishinda kata zote?!

Awe makini sponsor hayupo.
 
Tulia Trust Foundation inayomilikiwa na Tulia Akson ilifanya kazi kubwa sana kumuandalia mazingira ya ushindi spika wa bung, kina mama walipata mkopo ya bira riba, vijana wa Mbeya walipewa bajaj na bodaboda za mikopo nafuu za kutosha

Tulia hakubebwa alijijenga vizuri mpaka leo Mbeya inamuimba vzr Tulia nenda kajionee
Hiyo Foundation haiwezi msaidia chochote kwenye Box la kura. Tulia hana ushawishi ndo maana unaona anaangaika hata yeye mwenyewe analijua hilo, ndo maana kaibuka na hoja ya jimbo kugawanywa

Amepima ameona na ana wasiwasi kama mfumo utambeba kama enzi za mwendazake, ndo maana ameanza kutatapa, Ameona kikipigwa fair ni ngumu kutoboa..
 
Tulia Trust Foundation inayomilikiwa na Tulia Akson ilifanya kazi kubwa sana kumuandalia mazingira ya ushindi spika wa bung, kina mama walipata mkopo ya bira riba, vijana wa Mbeya walipewa bajaj na bodaboda za mikopo nafuu za kutosha

Tulia hakubebwa alijijenga vizuri mpaka leo Mbeya inamuimba vzr Tulia nenda kajionee

Wewe unatoka Mbeya kata ipi?
Mtaa upi?
Sehemu gani?
Mambo ya kuambiwa unayaleta hapa?
Tulia hawezi mshinda Sugu uchaguzi halali Mbeya mjini
Mengine ni porojo tu
 
Mbunge wa Mbeya mjini kupitia CCM, Dkt. Tulia Ackson amesema lengo la kugawanya jimbo la Mbeya mjini ni kusogeza huduma kwa wananchi na mchakato huo sio wa Mbeya pekee. Dkt Tulia aliongea hayo wakati akihojiwa na kituo cha redio cha wasafi leo asubuhi...
Hata yeye mwenyewe Tulia Ackson anajuwa kuwa alitoa Tsh 100,000 kwa wajumbe wote 800 wa Mkutano wa Jimbo la Mbeya Mjini ambao ndiyo waliompitisha kugombea kwa Tiketi ya CCM.

Pamoja na kuwekewa kinda na hawara yake Magufuli bado alitumia kama Tsh 100 Milioni kupita kura za maoni za CCM

Kuhusu kwenda Mahakamani jibu ni kwamba kipindi cha Magufuli ilikuwa ni vigumu kwa vile Majaji na Mahakimu kwa kesi kama hiyo ingekuwa ni vigumu kushinda. Mahakama zilikuwa zinatishiwa na kufuata maelekezo ya mwendazake.

Kwenye ushindani wa haki Tulia hawezi kushinda Mbeya, anasema tu kufurahisha wasikilizaji
 
Tulia Trust Foundation inayomilikiwa na Tulia Akson ilifanya kazi kubwa sana kumuandalia mazingira ya ushindi spika wa bung, kina mama walipata mkopo ya bira riba, vijana wa Mbeya walipewa bajaj na bodaboda za mikopo nafuu za kutosha

Tulia hakubebwa alijijenga vizuri mpaka leo Mbeya inamuimba vzr Tulia nenda kajionee
Tulia Trust imeharibu mazingira ya Mbeya. Hivi ni sahihi kweli Jiji la Mbeya kuwa na utitiri wa Bajaj kiasi kile. Inakadiriwa kuwa Mbeya Jiji kuna Bajaj takriban 10,000. Anayekopesha bajaja hizo ni ni Tulia kupitia Tulia Trust. Na hizo pesa alipewa na Magufuli.

Na ndiyo zina operate kama daladala. This is Bulshit
 
Tulia Trust Foundation inayomilikiwa na Tulia Akson ilifanya kazi kubwa sana kumuandalia mazingira ya ushindi spika wa bung, kina mama walipata mkopo ya bira riba, vijana wa Mbeya walipewa bajaj na bodaboda za mikopo nafuu za kutosha

Tulia hakubebwa alijijenga vizuri mpaka leo Mbeya inamuimba vzr Tulia nenda kajionee
Acha uongo kijana, bila mbeleko ya JPM asingetoboa kabia. Kiufupi hana mvuto wa kisiasa na hivyo unavyovitaja vina impact ndogo sana ukilinganisha na idadi ya wapiga kura
 
Spika wa Bunge na mbunge wa Mbeya Mjini amemtahadharisha Sugu kwamba ataaibika Kwa mara nyingine Kwa hiyo kabla ya kufikiria Kugombea Jimbo la Mbeya apime kina Cha Maji..
---
Hatimaye Spika wa Bunge, Tulia Ackson amevunja ukimya kwa kusema wanaotaka kugombea ubunge Mbeya Mjini wapime kina cha maji kama kinawatosha waingie kwenye kinya’ng’anyiro.

Spika Tulia ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini ametoa kauli hiyo leo Mei 4, 2023 Alhamisi wakati wa mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini akiwa katika makazi yake Jijini Dodoma.

Katika mahojiano hayo Dk Tulia ameeleza sababu za kutaka jimbo hilo kugawanywa akisema suala hilo halihusu Mbeya Mjini pekee bali katika majimbo mbalimbali makubwa na hatua hiyo itasaidia kusogeza huduma karibu.

“Ubunge wangu haijalishi jimbo limegawanya au halijagawanywa, mimi ndio Mbunge kama nilimtoa mtu (Sugu) katika kata 36, hataweza kunitoa kata zikiwaa chache kweli? Mbona itakuwa mtihani, zikibaki kata 36 nitawafyeka.

“Nisingeshangaa kujadiliwa na wao, tena napenda sana wao wameanzisha huo mjadala nimefurahi na wanaposema watanifuata, nataka wajipime kama wanaona kina cha maji cha kinawatosha waje, kama niliwatoa na kata 36 wataniweza wapi na kata chache? amehoji Dk Tulia.
 
Back
Top Bottom