Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,791
- 218,420
Spika Dr. Tulia amesema anaowawakilisha yaani wananchi wote wa Mbeya Mjini wanaunga mkono Uwekezaji wa Bandari.
Dr. Tulia amesema Mkoa wa Mbeya ni wakulima hivyo Uwekezaji wa Bandari utasaidia Mazao yao kufika kwenye Masoko kwa haraka.
Nanukuu
Baada ya kuitaja Bandari, maneno mengi yametoka huku Mbeya, nataka niseme hivi... Mimi ndiye mbunge wa hapa Mbeya Mjini na ni mwakilishi wa wananchi hawa walio wengi hapa. Kama mwakilishi wao, sisi wanambeya mimi kama mwakilishi wao tumekaa wameniambia wanakuunga mkono Rais kwenye uwekezaji ambao unafanyika kwenye bandari ya Dar es Salaam.
Na katika kukuunga mkono kwenye uwekezaji ambao Serikali inawekeza, wanakuunga mkono kwenye kutafuta wawekezaji wengine kuja kuboresha bandari ya Dar es Salaam ili mazao yanayotoka Nyanda za Juu Kusini yaweze kuwahi masoko ya nje.
---
Hili ni dhahiri kwamba Tulia Ackson ameamua kumdanganya Mh Rais kwa lengo la kumpotosha ili ajipatie umaarufu.
Kabla ya kuendelea hebu tuangalie maana halisi ya Uongo kama ilivyoelezwa kwenye kamusi ya kiswahili
Sasa kauli hii ambayo ametoa Tulia Ackson bila uoga mbele ya kiongozi wa Nchi maana yake nini? Kamshirikisha Mwana Mbeya yupi ikiwa sisi watu wa Mbeya hatutaki Mkataba huo?
Hivi kwanini hawa viongozi wanatudharau kiasi hiki , Tufanyeje ili tuheshimike ?