Tulia Ackson ana uroho wa Madaraka

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Amechukua fomu ya kugombea kiti cha Spika pasipo kujiuzulu U Naibu Spika kwa lengo la kuwa akishindwa aendelee kuwa Naibu Spika, Huu ndio unaoitwa uroho wa madaraka wenyewe.

Anasema, “kwa mujibu wa katiba waliotajwa kutogombea uspika ni Mwaziri na watu wenye madaraka ya umma”, kwani cheo cha Naibu Spika sio madaraka ya umma? vile vile anasema, “hata kama nimechukua fomu si kwamba kiti cha Naibu Spika kiko wazi, hapana”. Ina maana anazuia wengine kugombea U Naibu Spika hadi ajihakikishie ameupata U Spika.

Sawa pamoja na kuwa ni haki yake na sheria haimzuii kufanya hivyo, angeonekana ni mtu mwenye busara na hekima kama angesema, kama ni kuwatumikia wananchi kwa hadhi niliyonayo inatosha sana, lkn kwa kitendo alichofanya machoni pa watu anaonekana ni mtu dhaifu na mwenye tamaa.

C5966F28-4CDE-4D30-A444-F82908D196E2.jpeg
 
Haya ndio mambo ambayo hata role model wake JPM alikua hayataki. Tunakumbuka uchaguzi wa 2020, hata kama ni kwenye kura za maoni za chama, ukitangaz nia tu unakua automatically umeachia nafasi yako uliyonayo wakati huo iwe ya ajira au uongozi wa kisiasa

This should be a wakeup call kwa CCM au hata watu wa vetting. Kwa uroho huu wa madaraka huyu atakuja kusumbua saana siku zijazo.

Na attitude aliyoionyesha ya kuupamba muhimili wa Executive ndio kabisaa inam disqualify. Anataka kuingia kwenye kiti kwa false pretext kwamba she will always compromise na Executive lakini anamalengo ya mbali sna yenye kutia wasiwasi
 
Amechukua fomu ya kugombea kiti cha Spika pasipo kujiuzulu U Naibu Spika kwa lengo la kuwa akishindwa aendelee kuwa Naibu Spika, Huu ndio unaoitwa uroho wa madaraka wenyewe.
Hakuna ubaya kwa mtu yoyote to aim higher, kitu cha muhimu ni kufuata katiba, sheria, taratibu na kanuni.
Anasema, “kwa mujibu wa katiba waliotajwa kutogombea uspika ni Mwaziri na watu wenye madaraka ya umma”, kwani cheo cha Naibu Spika sio madaraka ya umma?,
Huyu ni mwalimu wangu wa sheria pale UDSM, kiukweli kwenye hili, mwalimu wangu amechemsha!. Alipaswa ajiuzulu kwanza u naibu spika ndipo agombee u spika!. Mimi huu nimeuita ubatili
vile vile anasema, “hata kama nimechukua fomu si kwamba kiti cha Naibu Spika kiko wazi, hapana”. Ina maana anazuia wengine kugombea U Naibu Spika hadi ajihakikishie ameupata U Spika.
This is not right
Sawa pamoja na kuwa ni haki yake na sheria haimzuii kufanya hivyo,
Sio haki yake na sheria inazuia, ila wanaopaswa kumzuia Tulia, wamenyamazia!.
angeonekana ni mtu mwenye busara na hekima kama angesema, kama ni kuwatumikia wananchi kwa hadhi niliyonayo inatosha sana, lkn kwa kitendo alichofanya machoni pa watu anaonekana ni mtu dhaifu na mwenye tamaa.
Ili mtu atumie busara, kitu cha kwanza ni hiyo busara yanyewe kwanza iwepo kisha ndipo itumike!. Kama hiyo busara yenyewe haipo, kwa mtu kama huyo unategemea nini?.
P
 
Viongozi wetu wengi hawana maadili na wamejawa tamaa na madharau,walifundishwaga kujiamulia mambo watakavyo na kibabe nakuwa katiba,sheria na taratibu za jamii sio muhimu.

Tukiacha unafiki kwanamna spika anavyolipwa kupitiliza na maisha yalivyo magumu hukunje na alivyopewa nguvu kujiamulia atakavyo hakuna namna MTU ataacha kutamani hikicheo.

Ilipaswa kuangaliwa upya namna wanasiasa wanavyojilimbikizia malipo makuubwa bila aibu huku wavujajasho wengine wakilipwa mishahara isiyotosha hata kumlisha mbwa kwamwezi mfano walimu...

Mzee kama Change ameshika madaraka miaka kibao lakini bila aibu bado anatamani kula mahela ya kodizetu kwafujo! Mbabu kabisa anataka kuliongoza binge na mkongoja kiss mihela...kwanini asiende kufundisha vijana hats vyuoni??? Anafata kwenyehela zabure!!! Wananchi tunakufa njaa na kuduwaa huku tukisifu wanaotunyonya....hopeless

Nionavyo wanavyojilipa nisawa na uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya madaraka!!

Tusikubali kuwa mazuzu,katiba mpya ni muhimu mmmmno
 
Back
Top Bottom