Tukumbushane watu wa Tabora-Mboka Manyema

Mkuu kipi kimekujuza km mie ni mdugu wa marehemu Ibrahim mgumia!?
Maana sijatoa details zote za msingi, zaidi ya kusema eneo nililokuwa naishi ambalo walikuwa wanaishi watu mamia kwa mamia.
Ning'ate sikio kidogo
Na ndugu yako mwingine Dotto Koloko yuko wapi mkuu?Yule kijana wa mwl.Mgumia wa S/Msingi Mkoani zamani.
 
Hapana mkuu, ila nina uhakika atakuwa ni ndugu yangu, kibaya niliondoka tabora mdogo toka 98 sikurud tena hadi mwaka huu, nmefanya kama kupita kwenda urambo katika mazishi ya kaka yangu.. Mie ni miraji hemedi mgumia, anaweza akawa ananijua, mie sikukaa sana upande wa faza wangu, but i wish niwajue ndugu zangu, naskia tupo wengi kupita maelezo

Hapa Mzee umejitambulisha tena kwa majina yako yote Matatu.

Nakushauri fanya Editing uondoe kama hupendi watu wakujue.
 
Hapa Mzee umejitambulisha tena kwa majina yako yote Matatu.

Nakushauri fanya Editing uondoe kama hupendi watu wakujue.
Hahaa!! Haya sawa mkuu, sikujua km nilijitambulisha huko nyuma, nashukuru.
Kwa mapenzi ya kuwasaka ndugu zangu nikajikuta nimejitambulisha

Hahaa..
 
[QUOTE="Bubu fulani alikuwa na mashuti sana[/QUOTE] alikuwa anaitwa Jumanne Mikidadi!
 
Haya haya wale vijana wa kombe la mgulunde tuliokuwa milambo boys njoo tuimbe ule wimbo wetu tuliokuwa tunawachachafya watoto wa uyui secondary hapo tupo uwanja wa vita watoto wa majugwa utuambii kitu haya tuanze kuimba

Hapo kuna game kati ya uyui vs milambo boys

Wanafunzi: Hodi hodi humu ndani
Wanafunzi: Karibu
Wanafunzi: Medy tumemkuta
Wanafunzi: Hayupo
Wanafunzi: Kaenda wapi

Wanafunzi: Kaenda kupigwa bao kaenda kupigwa bao kaenda kupigwa bao😀😀😀😀

Mtoto wa kiarabu medy alikuwa naupiga sana mpira hivi yupo wapi uyu medy hapa naongerea miaka ya 90's hivi
 
Ha ha ha ha Ntalali na Ntonga!pale Tabora Boys alikuwepo Yahaya Akilimali..kafupi lakn kanapiga chenga mpaka balaaa...mwalimu alikuwa Bundala na Brasband ya Kanyaboya....unakutana mtbni na demu bomba ajabu lakin anatoka nyumba ya mbavu za mbwa!jambo la kawaida kukuta mauzauza njia panda..kuku kachinjwa na nazi imebanduliwa!!....watu wanaishi kwa kula vipande vya mihogo vilivyokatwa sokoni.......mtaa wa Marando Ng'ambo unasifika kwa wauza makopa wakiwa na vibatari!FIFI anamiliki pikipiki na ndo Digala....Tabora haiendelei licha ya ukongwe na umaarufu wake!imetoa watu maarufu na imesomesha viongozi pale Tbora Boys!Ngoma ya Waswezi na ushirikina!Wapi Dr.Othman kada wa CUF?U.M.D na NRA ndo ngome zao!1995 Mrema yupo moto..kaja na Makongoro Nyerere uwanja wa Kazima Sec..Nakumbuka Nukuu ya Makongoro "Mfupa uliomshinda Fisi Mbwa ataweza?"...kwamba ye kazaliwa Ikulu na kukulia humo lakn yupo NCCR!Tukamsukuma Mrema mpaka hoteli flani ipo BOMA-Road
Bundala na Kanyaboya walikuwepo Boyzia had 2005 kama ulipita T boys naamini story za Tukutuku utakua nazo nyingi sana
 
Nilisoma shule ya msingi na mtoto wa mwl.Kanyaboya,Damas.Jamaa alikuwa na akili halafu mchoraji mzuri toka darasa la kwanza.Sijui yuko wapi yule jamaa!
Mmoja alikua na Saluni meneo ya Madafu makutano ya njia ya kwenda Cheyo National na Kuteremka get la Boys
 
Hahahhaa hii thread nouma!! inanikumbusha life la Tabora wakuu, maeneo ya Ng'ambo kwenye pilau usiku usiku!! Tukutuku kuchota maji, kwa Sonda kucheki UEFA, hahaha nilikuwapo miaka 10 hadi 12 iliyopita wakuu pale Tabora Boys.
Mhh pilau almaarufu Kipuche 'hii huduma c ilikua inapatikana pale DH kuanzia saa sita usiku ?Au ulikua unafata na mambo mengine N'gambo
 
Mkuu umenikumbusha mbali sana...mwehu maarufu enzi zile alikuwa anaitwa malingumu mzee mmoja kichaa alikuwa soko kuu, mimi nilizaliwa ng'ambo mtaa maarufu unaitwa kwihara street, baba yangu alikuwa ana shamba kijiji cha usenge karibu na jumba la makumbusho(livingstone)...pale kwihara kulikuwa na waarabu kina zahoro nasikia aliuza ile ardhi kwa chuo cha st augustine au tumaini university......ujio wa papa binafsi ulinigusa sana nilikuwa mdogo ila kwa kweli papa John Paul II alikuwa charismatic...na kwa kweli huko alipo ni mtakatifu...jet yake ilitua uwanja wa tabora wa vumbi, tukiwa nyumbani mida ya saa tisa hivi tulishangaa ndege nyeupe ina mlio mkali(jet) ikitua....majambazi niliokuwa na wakumbuka mimi ni kina mohamed romba...pale ng'ambo kulikuwa na mpakistan mmoja na familia yake alikuwa anaitwa Nuru din alikuwa na wasichana mabinti wareeembo...hakika maisha ni safari yenye uchungu sana kwa sisi tuliopitia mambo magumu....kanisa katoliki ilikuwa ni nguzo muhimu ...namkumbuka marehemu padre John Mageda, ndiye alinibatiza......akikuwa anajua sana kuimba zile sala za ekaristi takatifu...bwaaana awe naaaanyiiiiiii, inuuueeeeeniiii mioyooooooooooo! tumeinuuua kwa bwanaaaaa! mimi nilisoma Uyui sekondari
Unauhusiano na marehemu mzee James Shigela ?
 
Daaah wakuu mmetiririka sana kuhusu Tabora a.k.a Mboka Manyema
Mkuu umemikumbusha uwanja wa Chipukizi,jirani yake kulikuwa na shule ya viziwi na mabubu
Yaani Misa ya watoto pale kanisa katoliki jioni ikiongozwa na Padre Tengi au Padre Dino
Wale mabubh walikuwa tunawaogopa sana dadeki,nao wakawa wanatutandika mbaya tukiwacheka
Pale Maktaba karibu na TMP ndio palinifanya niwe mpenzi wa kusoma Novels mpaka leo,na nimejifunza kumbe utamadunu wa kujisomea vitabu unatengenezwa,ninafanya hivyo kwa wanangu ili wawe na huo utamaduni baadae
Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mnaingia wakati wa "fungulia Mbwa" au unaingia na mlemavu
Kuokoata mpira mpaka uwe na sare za scout au chipukizi
Daaaaah wapi watu wa Mboka Manyemaaaaaaaaa back 1990's
Padre Tengi bana aliwachimbaga biti wanajeshi[Milambo barracks] kanisani tena pasipo uwoga wowote ule na hawakuwahi kumfanya kitu chochote kile.
 
Ni Majubwa sio Majugwa. Kimbembe kilikuwa hatari Sana miaka hiyo. Mimi ni Alumni wa Milambo wanaume pia wa kipindi cha Majubwa late 90's to early 2000's
Haya haya wale vijana wa kombe la mgulunde tuliokuwa milambo boys njoo tuimbe ule wimbo wetu tuliokuwa tunawachachafya watoto wa uyui secondary hapo tupo uwanja wa vita watoto wa majugwa utuambii kitu haya tuanze kuimba

Hapo kuna game kati ya uyui vs milambo boys

Wanafunzi: Hodi hodi humu ndani
Wanafunzi: Karibu
Wanafunzi: Medy tumemkuta
Wanafunzi: Hayupo
Wanafunzi: Kaenda wapi

Wanafunzi: Kaenda kupigwa bao kaenda kupigwa bao kaenda kupigwa bao

Mtoto wa kiarabu medy alikuwa naupiga sana mpira hivi yupo wapi uyu medy hapa naongerea miaka ya 90's hivi
 
Back
Top Bottom