Tukumbushane "table manners" mbovu

Tukumbushane "table manners" mbovu

_mnakula pamoja mfano ugali, mtu aacha kula upande wake anakuja kumega upande wako

_mnakula pamoja , ghafla mtu anastop anaenda msalani akirudi anaendeleza kupiga menu na mnashea

_mnakula mfano nyama, mtu anachagua chagua ,badae anaona kipande kinachomfaa ndio anakichukua

_mnakula pamoja, mtu anapiga chafya hazibi mdomo, particles zinawarukia

_mnakula wali maharage may be na mchuzi wa nyama, vimechanganywa kwenye sinia, mtu anafinyanga Kama tonge adi michuzi inachuruzika kwenye kiganja , inatia kinyaa

Ongezea nyingezo
 
Njooni huku pwani muone mpaka leo bado watu wananawa sehemu moja ,yaani anaanza baba anatia mikono kwenye beseni wanafuata watoto na kula kwenye sinia moja,tena wanaona kawaida sana!
 
Njooni huku pwani muone mpaka leo bado watu wananawa sehemu moja ,yaani anaanza baba anatia mikono kwenye beseni wanafuata watoto na kula kwenye sinia moja,tena wanaona kawaida sana!
Khaa! Kumbe kuna watu bado wana hii tabia
 
1) Mfano mnakunywa chai ya Ofisi, Miakte labda inanunuliwa minne. Mmoja ushafunguyliwa na haujaisha but mtuu anakuja anafungua mwengine.

2) Hapo juu mtu anafungua mkate anatoa vipande vyake na haufungu uliobaki, bila kujali Mende na Hewa vyaweza kuingia ukaharibika.

3) Labda vijiko vya chai viko vichache. Mtu anakoroga chai kisha anaonja na kurudishia kijiko kwenye sukari. Kawaida inabid ujue saizi yako, hakuna kuonja kama vijiko ni vya kushea.

4) Mnakula wengi kwenye sahani moja (mtu Kati). Mtu anafinyanga wali akishautia mdomoni anakung'utia mkono kwenye sinia yale mabaki. Kisha anendelea kula.

5) Mchuzi umemiminiwa kwenye wali sahani nzima. Inabidi ule wali kulingana na mchuzi uliomiminwa (Vertically). Sasa wewe unakula kwa kukwangua juu juu (Horizontally) ule wenye mchuzi. Matokeo yake unabakia wa chini ambao hauna mchuzi.
Mkuu umeua, pata coke Baridi hapo kwa mangi
 
Ndio mnaanza kula ugali na kuku-jogoo mchuzi, ghafla jirani anaingia na kukaribishwa kwa heshima na taadhima. Anajibu: " Aaaa, nimeshiba, nimetoka kula muda si mrefu uliopita, lakini ngoja nitie baraka kidogo" anamega tonge mbili halafu anageukia bakuli la finyago na kuchukua bonge la paja!! Halafu: Aaa! asanteni nimeshiba" Ananawa mkono na kuodoka akimung'unya paja la jogoo!
 
Njooni huku pwani muone mpaka leo bado watu wananawa sehemu moja ,yaani anaanza baba anatia mikono kwenye beseni wanafuata watoto na kula kwenye sinia moja,tena wanaona kawaida sana!
Kinyaa, wanalishana uchafu
 
Ndio mnaanza kula ugali na kuku-jogoo mchuzi, ghafla jirani anaingia na kukaribishwa kwa heshima na taadhima. Anajibu: " Aaaa, nimeshiba, nimetoka kula muda si mrefu uliopita, lakini ngoja nitie baraka kidogo" anamega tonge mbili halafu anageukia bakuli la finyago na kuchukua bonge la paja!! Halafu: Aaa! asanteni nimeshiba" Ananawa mkono na kuodoka akimung'unya paja la jogoo!
kizuri kula na jirani
 
Mnakula lnatokea jitu lina mafua linaanza kuyavuta ile sauti inakeraaa. Unataman umwambie akayatoe na asirudi mana n kama atarudi na uchafu
 
Mpo mezani mtu anakunywa chai kama anapenga kamasi

anavuuutaaaaa yani unamkata jicho 1,unamwambia kama ya moto si ukapooze aseee
 
Hii story niyakweli,miaka ya 90's kweusi,Digi alikua na wake wawili so tukawa natabia ya kila mama akipika chakula kinaletwa na tuna Kuna watoto wote kwa pamoja.huku kapika wali marage huyu kapika makande.sinia zinakuja mpaka tushibe.sasa Kuna dogo letu mmoja alikua Hana kipimo mzee tumekula sinia la kwanza,mtu Kama nane,sinia la pili dah kufika la tatu dogo kumbe alishiba kwanini asitapikeee dah alfu wali arageeee....ikawa mwisho
 
sema mimi kula mviringo kwenye sinia mtanisamehe ndugu zangu,yamenishindaga
 
Back
Top Bottom