Tukumbushane "table manners" mbovu

Tukumbushane "table manners" mbovu

Nimekumbuka kabisa babu yangu, RIP wajina wangu
Chakula kikija yeye ananza bakuli la mchuzi, anakunywa kwanza hadikifike kiwango akitakacho then ndio mnaanza kula.
Wazee wazamani miyeyusho kweli...
Alooo
 
_mnakula pamoja mfano ugali, mtu aacha kula upande wake anakuja kumega upande wako

_mnakula pamoja , ghafla mtu anastop anaenda msalani akirudi anaendeleza kupiga menu na mnashea

_mnakula mfano nyama, mtu anachagua chagua ,badae anaona kipande kinachomfaa ndio anakichukua

_mnakula pamoja, mtu anapiga chafya hazibi mdomo, particles zinawarukia

_mnakula wali maharage may be na mchuzi wa nyama, vimechanganywa kwenye sinia, mtu anafinyanga Kama tonge adi michuzi inachuruzika kwenye kiganja , inatia kinyaa

Ongezea nyingezo
1) Mfano mnakunywa chai ya Ofisi, Miakte labda inanunuliwa minne. Mmoja ushafunguyliwa na haujaisha but mtuu anakuja anafungua mwengine.

2) Hapo juu mtu anafungua mkate anatoa vipande vyake na haufungu uliobaki, bila kujali Mende na Hewa vyaweza kuingia ukaharibika.

3) Labda vijiko vya chai viko vichache. Mtu anakoroga chai kisha anaonja na kurudishia kijiko kwenye sukari. Kawaida inabid ujue saizi yako, hakuna kuonja kama vijiko ni vya kushea.

4) Mnakula wengi kwenye sahani moja (mtu Kati). Mtu anafinyanga wali akishautia mdomoni anakung'utia mkono kwenye sinia yale mabaki. Kisha anendelea kula.

5) Mchuzi umemiminiwa kwenye wali sahani nzima. Inabidi ule wali kulingana na mchuzi uliomiminwa (Vertically). Sasa wewe unakula kwa kukwangua juu juu (Horizontally) ule wenye mchuzi. Matokeo yake unabakia wa chini ambao hauna mchuzi.
 
Mbinu na kijesi!plus uchoyo...mnakula unapega jamasi unafuta then unarudi kwenye sinia. Lazima waondoke mezani
 
Back
Top Bottom