Tukumbushane "table manners" mbovu

Tukumbushane "table manners" mbovu

_mnakula pamoja mfano ugali, mtu aacha kula upande wake anakuja kumega upande wako [emoji3185]

_mnakula pamoja , ghafla mtu anastop anaenda msalani akirudi anaendeleza kupiga menu na mnashea [emoji34]

_mnakula mfano nyama, mtu anachagua chagua ,badae anaona kipande kinachomfaa ndio anakichukua [emoji2957]

_mnakula pamoja, mtu anapiga chafya hazibi mdomo, particles zinawarukia [emoji855]

_mnakula wali maharage may be na mchuzi wa nyama, vimechanganywa kwenye sinia, mtu anafinyanga Kama tonge adi michuzi inachuruzika kwenye kiganja , inatia kinyaa [emoji34]

Ongezea nyingezo [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Mkeo kaleta wali na nyama, mgeni analazimisha kunawa na kuomba aongezewe nyama. Mnaanza kula tu, yeye anatafuta nyama kubwa kubwa huku akiongea kwa furaha kana kwamba yuko kwake na kulalamika kuwa chakula ni kidogo hamta shiba huku akimuita mkeo. Shemeji mbona hiki chakula umepakua kidogo hivi, hakuna kilichobaki huko jikoni?
 
Back
Top Bottom