Bonde la Baraka
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 4,580
- 7,955
Habari za usiku wazee!
Mara nyingi huwa tunapigiana simu au kuandikiana sms kuomba tuvushane kifedha.
Sasa shida inakuja mara baada ya kutumiana hiyo fedha.
Wengine wanarudisha bila kupiga hesabu ya fedha ya kutolea. Yaani kama nilikukopesha 50,000/= ukiituma vilevile hapo unakuwa umenifanya nipate fedha isiyo kamili. Ya kutolea na ya kutumia usiisahau ili angalau fedha yangu yote niipate mkononi.
Suala lingine ni kutokujali muda ulioahidi kulipa deni. Kama mtu kakubali kukukopesha bila riba tena bila masharti basi ili kuendeleza uaminifu ni vyema kurudisha ndani ya muda uliojikomiti. Na si kuzima simu au kujifanya uko bize.
Mungu si mnafiki, usipokuwa mwaminifu ataruhusu upate aibu nyingine kubwa na hutamwona wa kumkopa fedha.