sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,021
- 5,253
Darasa la 7 hesabu zilikuwa zinanipa shida Shule ya Msingi Wilolesi, mtihani wa kwanza wa ujirani-mwema nikapata 21/50 kama sikosei. Mwalimu Mkuu wetu, Mwl. Mapunda akaja na wazo zuri kwa wanafunzi kuhusu somo la hesbu kuwa unapoingia kwenye mtihani hakikisha swali la 1 mpaka la 33 ambazo ni hesabu nyepesi nyepesi unapata yote, yaani fanya kwa usahihi swali la 1 mpaka 33, kuanzia swali la 34 ni maumbo na mafumbo, hapo donoa donoa ukipata maswali 7 kati ya 17 yaliyobaki unakuwa umepata maksi 40/50. Aisee, niliitumia kanuni hiyo na mpaka namaliza sikuwahi kupata chini ya 43/50. Na mpaka leo nikikutana na somo la hesabu huwa naendelea kutumia kanuni hiyo, puuza maswali magumu komaa kwa uhakika na mepesi yenye maksi nyingi, magumu waachie wataalamu, donoa donoa tu.Nikiwa darasa la tano nilikuwa na mwalimu wa kuitwa Mponji,ehhh bwana eeeh!Hiyo topic ilikuwa inaitwa vigao na vigawe Mara vipeo na vipeuo,jamani alikuwa anaingia na fimbo ndefu inanesanesa ni ule mti unaotumika kutengeneza viti vya kukunja,nilikuwa nikimuona tu tumbo lote linanikata,sikuwahi kuelewa zile hesabu hata siku moja kila uchao nilikuwa nmapaja jamevilia damu,hapo ndio ilikuwa mwisho wa safari yangu ya kimahesabu!nimekuwa na allergy na Hilo somo mpaka chuo,alifanya nipate tabu Sana na Statistics for!Mungu mlaze mahali pema peponi mwalimu.