Tukumbushane kidogo ghetto time!

Tukumbushane kidogo ghetto time!

Tulianza wawili mwisho nikajikuta wamefika 5.
Geto halikatiki mademu wapya wapya tu.
Tatizo majukumu ya getho anaachiwa mwenye geto. Chakula na kodi na bill ndogo ndogo husaidiwi hata kidogo.

Geto lilipoanza kuonekana kama la Bob Marley nilibadilika nikaanza kuwaambia wapange maana kama pesa sote tulizipata na tulikuwa twafanya kazi pamoja.
Ghetto kuna visanga!nakumbuka wakati nakaa ghetto basi nilikuwa nimepanga chumba maeneo Fulani karibu kabisa na town basi nikajikuta ghetto masela kama wote na wapita njia ndio usiseme!unajikuta sometimes kwenye kitanda cha futi 4 mnalala hadi MTU sita na mnaenea na panachuka!
Basi washkaji wa tatu ndio wakaamia kabisa na kuwafukuza nikashindwa!bahati nzuri mwenye nyumba alikuwa sio mtata!
Kila mshkaji nikamkabidhi funguo yake ili kuondoa usumbufu wa hapa na pale!

Sasa kimbembe kilikuwa kulipa kodi hata nifulie vipi kila MTU anadai hana pesa Mzee najituma mishe zangu nalipa mwenyewe!
Kumbuka hapo ghetto kila kitu ni changu!
Basi washkaji full kuleta Mademu kila time yaani wanasubiriana foleni!na mashuka no kufuliwa full kulalia NY****G**!
Nilivumilia mwaka mzima nikaona isiwe tabu maana kuhama mitaa ile karibu kabisa na town haiwezekani na washkaji kila nikiwaambia wajipange watafute maghetto hawana habari ni full kuhonga tu Mademu na kwenda viwanja vikali!

Sasa siku nikawaamulia tu nikabadilisha kitasa pia nikaweka na Bonge la kufuli!nikaenda kujipa likizo sehemu Fulani wiki nzima!
Hadi narudi kila MTU alikuja tu kuchukua begi lake nyambavu
 
Mambo ya kuishi na masela ni ya kijinga sana.

Kuna jamaa wawili niliwahifadhi ghetto kwangu kwa kama miezi 6 hivi, Wanakula, vyombo vinakaa hata wiki hawaoshi hadi nioshe mimi, Ndani vumbi linajaa, michanga wanakaa tu, hamna wa kujishughulisha nna Usafi isipokuwa mimi. Ilikua inanikera sana.

Watu wanabeba Viepe wanakula wanaacha mifuko na makaratasi juu ya meza, maganda ya ndizi.

Nilivumilia nikashindwa, siku moja nikawatolea uvivu, ila nikaonekana nawanyanyasa na kuwababaisha kisa wanaishi kwangu. Nikawaambia kama hawawezi kubadilika wasepe, Baada ya muda Wakasepa. Hivi sasa naishi mwenyewe mambo safi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom