Tukumbushane: Hivi Diamond alimpiga bao wapi Belle 9? Kwani wote walitoka kipindi kimoja!

Simba atatafuna Pori zima na hataacha hata nyumbu Porini, Hata Balozi wa Wanyama atatafunwa na Simba soon
 
Nakumbuka siku ya kwanza "nenda kamwambie" inatambulishwa Kama ngoma mpya mida ya jioni......siku hyo brother angu alinambia "huyu msanii anaimba vzuri Sana atafika mbali"" mi nikaona Kama ananipigia kelele Tu hata sikumjibu kitu.
Mimi mwenyewe sikuwa naona kama mkali tena nilikuwa namuona msanii wa msimu tu ila belle nilikuwa naona atafanikiwa sana
 
Diamond ajaanza na belle 9 .
Mondi alikuwa na pacha wake anaitwa shetta sasa ndo ujiulize kwann Mondi kampiga gepu shetta ?

Belle 9 so talented boy bt mfumo wa watu wa ghorofani pale mlalakua ulimu underrate Sana . Jiulize yule demu Ruby yupo wapi ? Clouds imewapotezea wengi sana future.
Ndio wakome kutegemea media house moja tu
 
Hongera sana mwandishi kwa mada nzuri pia umechambua vizuri mno hakika Wewe ni fan wa music,binafsi nadhani Belle9 aliridhika mapema sana na ndio ugonjwa Wetu Tanzania yaani Hatuna njaa ya mafanikio binafsi Nilipoona tu wimbo Kamwambie na Msanii anaitwa Diamond Nilijua tu atafika mbali sababu uchaguzi wa jina pia ni kitu cha kuzingatia kwenye Sanaa pia alivaa na kupendeza zaidi alipiga bao alipotoka na Wema pale ndio fungakazi lakini jamaa ana vision(maono)makubwa haridhiki na alipo Tunalo la kujifunza pia Nafurahi Harmonize pia ataleta mapinduzi kwenye muziki sababu vision yake ni mbele sio bongo
 
Peter principle. Utapanda mpaka kufikia kiwango fulani kinachoendana na uwezo wako. Baada ya hapo huwezi. Diamond pamoja na mambo mengine ana uwezo wa kusimamia mambo makubwa kuliko wengine.0
 
TTHread bomba ya mwaka kutoka jukwaa la ubuyu...

hv ni mafanikio gani aliyonayo Belle o9k?
Ana account Insta
Maksai wanne ambao hua anakodisha kwa wakulima msimu wa kilimo ukifika
Baiskeli 3 za abiria ziko ruti ya Kwamakunganya-Dakawa
Water pump moja ya Honda ndogo kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji
Tv ya singsung 24", deki ya ZEC na bufa ya Sea Piano
Mamsumeno mawili yale makubwa ya kupasulia mbao ambayo gogo linawekwa juu ya shimo then baharia mmoja anakua juu na mwingine ndani ya shimo
Kibanda umiza cha movie za Dj Afro eneo la Bigwa
Ananunua tairi used kwa ajili ya kiwanda chake cha malapa ya tairi.
Kila jumamosi anapiga shoo baa fulani mixer bia na pombe za kienyeji wanazungushia turubai then kiingilio inakuwa buku kwa wanaume ladies free.

Jamaa ana mafanikio kwa pale Moro anashika shika namba ya wenye nazo
 
Nimecheka kama mwendawazimu sasa wewe umejuaje yote hayo au wewe ndio belle 9

Back
Top Bottom