Tukumbushane: Hivi Diamond alimpiga bao wapi Belle 9? Kwani wote walitoka kipindi kimoja!

Mkuu Diamond alianza kuonekana ana nyota ya kukubalika zaidi kuliko belle 9 wakati waliposhindana kwenye tuzo za kili music awards....ikumbukwe kuwa wakati huo 2010 wote hao walikuwa ni underground na hawakuwa na beef na media au wadau wakubwa wa bongofleva...hivyo ni wazi kuwa wote walikuwa wanategemea nguvu ya mashabiki...pia ikumbukwe kipindi hicho diamond hata hizo skendo alikuwa hana kbs yani bado kinda.

Sasa nashangaa unaposema belle 9 alikuwa juu zaidi ya diamond wakati wanaanza kutoka,na ilhali mashabiki waliamua kwenye tuzo za kili kwa kumtunukia diamond tuzo 3 kwa mpigo...baada ya hapo ndipo dogo akaanza kuinyoosha bongofleva maana kama chura ndo keshapigwa teke.

Wimbo wa mbagala huwezi kuufananisha na ngoma yeyote ambayo ilitoka kwa wakati ule...yaani kipindi cha mbagala kulikuwa hakuna takataka unaweza ilinganisha hapo...hii ngoma ilibamba mpk kero tena kwa rika na jinsia zote.

Belle 9 alikuwa mkali kwa kiasi chake lakini hakuwahi kumfikia diamond na hata kwa popularity ya ngoma zao hakuna ngoma hata moja ya belle ambayo ilikuwa most popular kushinda ya diamond kidoooogo kwenye masogange alikaza ila nyengine hazikuwa za kutisha sana ukilinganisha na pini za mondi....ukikaa na kuvuta picha kwa makini sana utaungana na mimi katika hili.

Ngoma kama, mbagala, nalia na mengi ft chidi benz, moyo wangu, mawazo ilikuwa ni misumari ya hatari kwa taifa aise...
 
Diamond ajaanza na belle 9 .
Mondi alikuwa na pacha wake anaitwa shetta sasa ndo ujiulize kwann Mondi kampiga gepu shetta ?

Belle 9 so talented boy bt mfumo wa watu wa ghorofani pale mlalakua ulimu underrate Sana . Jiulize yule demu Ruby yupo wapi ? Clouds imewapotezea wengi sana future.
 
Kwa wenzetu mamtoni hili liko wazi ila kwa bongo hawataki kulikubali ila ndio fact utake usi take, ili uwe famous and rich lazima uwe chamani.

Huu ndio ukweli mchungu kwa hiyo mnaposhangilia mafanikio yake mkubali pia kumeza huu ukweli mchungu.
 
Jiulize tna n hii alikiba alitoka pamoja na z anto ila z yupo wapi nbka leo.....
Alikiba hajatoka na Z Anto, Alikiba alitoka na Marlaw tena walikuwa na kaupinzani enzi hizo, kipindi Alikiba anatamba na Cinderella Marlaw alikuwa anakimbiza na Bembeleza. Mtoa mada ukiweza andika makala jinsi Alikiba alivyompiga gap Marlaw baada ya kumuoa Besta, kipindi kile Alikiba alikuwa anaumizwa kichwa na Marlaw, maana hata tuzo za Kili alikuwa anazizoa mbele yake
 
Mkuu Diamond alianza kuonekana ana nyota ya kukubalika zaidi kuliko belle 9 wakati waliposhindana kwenye tuzo za kili music awards....ikumbukwe kuwa wakati huo 2010 wote hao walikuwa ni underground na hawakuwa na beef na media au wadau wakubwa wa bongofleva...hivyo ni wazi kuwa wote walikuwa wanategemea nguvu ya mashabiki...pia ikumbukwe kipindi hicho diamond hata hizo skendo alikuwa hana kbs yani bado kinda.

Sasa nashangaa unaposema belle 9 alikuwa juu zaidi ya diamond wakati wanaanza kutoka,na ilhali mashabiki waliamua kwenye tuzo za kili kwa kumtunukia diamond tuzo 3 kwa mpigo...baada ya hapo ndipo dogo akaanza kuinyoosha bongofleva maana kama chura ndo keshapigwa teke.

Wimbo wa mbagala huwezi kuufananisha na ngoma yeyote ambayo ilitoka kwa wakati ule...yaani kipindi cha mbagala kulikuwa hakuna takataka unaweza ilinganisha hapo...hii ngoma ilibamba mpk kero tena kwa rika na jinsia zote.

Belle 9 alikuwa mkali kwa kiasi chake lakini hakuwahi kumfikia diamond na hata kwa popularity ya ngoma zao hakuna ngoma hata moja ya belle ambayo ilikuwa most popular kushinda ya diamond kidoooogo kwenye masogange alikaza ila nyengine hazikuwa za kutisha sana ukilinganisha na pini za mondi....ukikaa na kuvuta picha kwa makini sana utaungana na mimi katika hili.

Ngoma kama, mbagala, nalia na mengi ft chidi benz, moyo wangu, mawazo ilikuwa ni misumari ya hatari kwa taifa aise...
IMG_5953.jpg
kwa kweli shida ilianzia hapa, kwa kipindi hicho ilikuwa ni tukio la ajabu msanii kuchukua tuzo 3 kwa mpigo, wakina Lady Jaydee waliwahi kuchukua tuzo 2 ila sio 3, so ilimpa attention kubwa Diamond kwa kipindi hicho ukifungulia redio story ni yeye na tuzo 3, na dogo aliitumia hiyo nafasi vizuri kutoboa kwa hiyo tumsifu kwa hilo. Kina 20% walipata attention kwa tuzo 5 lakini hawakufanya lolote la maana baada ya hapo
 
View attachment 655324kwa kweli shida ilianzia hapa, kwa kipindi hicho ilikuwa ni tukio la ajabu msanii kuchukua tuzo 3 kwa mpigo, wakina Lady Jaydee waliwahi kuchukua tuzo 2 ila sio 3, so ilimpa attention kubwa Diamond kwa kipindi hicho ukifungulia redio story ni yeye na tuzo 3, na dogo aliitumia hiyo nafasi vizuri kutoboa kwa hiyo tumsifu kwa hilo. Kina 20% walipata attention kwa tuzo 5 lakini hawakufanya lolote la maana baada ya hapo
Umenikumbusha kitu kingine katika kutumia fursa...ndo maana hata baada ya kuvunja record ya 20% kwa kuchukua tuzo 7 kwa pamoja (bado haijavunjwa hii rekodi) mondi hakujibweteka alizidi kukaza sana mpk hapa alipofikia leo...tutake tusitake dogo anajua hlf mjanja sana
 
Usizunguke mbuyu Diamond skendo ndo zilimuweka juu + tuzo 3 za kili awards akaanza kuwacheza shele bongo muvi hapo akawini udaku wote

huu ni ukweli mtupu. skendo zinasaidia sana kukupa attention kwenye vichwa vya watu, belle 9 enzi hizo skendo aliyoipata ni moja tu ya kutoka na aggy masogange ila diamond kachepuka kwa mastar wenzie na data zake zilikuwa rahisi kupatikana kwa mapaparazi. sometimes unaweza ukakaa na celebrity wa kike hata kama sio demu wako you have to do something kwa mapaparazi kesho uwe kwenye "fent ford" na ndicho alichokifanya diamond. Muangalie harmorapa kuimba hajui ila angalia vituko vyake kwa celebrities wenzie mbele ya mapaparazi vilivyomfanya akapata Fame yakutosha kuliko hata mziki wake. na ilimsaidia hata "kiboko ya mabishoo" kusikilizwa na kutazamwa. Unapopunguza kuonekana kwenye medias ndipo watu wanapokupotezea taratibu na kukuona wa kawaida. mfano kama umechaguliwa kuwania tuzo flani wiki ijayo basi do something for the sake of makachero wiki yote uwe on air tu alafu uone kama hujashinda tuzo.
 
Ndio hapo, Diamond baada ya kuchukua tuzo 3 kwa mpigo, akafuatia na ngoma baada ya ngoma na zote kali. Watu wakaanza kumvesha masikio marefu Ali Kiba, na yeye akalinunua bifu bila sababu, akasema nimekuja kufuta vumbi kiti changu. Ndio akatoa wimbo wa Kimasomaso Mwanangu Usimuone.
 
sijaisoma makala yako yote
ila mimi nitajibu swali lako tokana na mujibu wa heading yako

nihivi katika maisha wote mnaweza mkawa mnafanya jambo moja lakini mkawa mnatofautiana vision ..mimi nimebahatika kuwa karibu na belle mnooo
belle alikuwa anahang na watu wakawaida ambao hawakuwa na malengo makubwa dhidi ya future yao ifahamike kuwa diamond hakufika pale alipo kwa bahati mbaya but alikuwa nimtu anayetembea huku akiwa namchoro wenye pictr kubwa unaomfnya atamani kufika pahala flani kwenye mafanikio aliyoyalenga ...
wakati diamond alikuwa anapambana kutafuta network mbalimbali zakumfikisha pale alipo Leo ...belle9 alirudi morogoro huku akawa anaendesha Nazi zake zamziki huko nawakati anafnya huvyo alikiwa ndio yupo juu mnoo
so akachagua kurudi Moro sehemu ambayo inaufinyu wa fursa za music so alitegemea nani wakumfuata huko nakumpa michongo...then alikuwa anafnya kazi kienyeji hkuwa kuwa na manager ..alikuwa na washkaji tu kina monagangster watu ambao sio wazoefu kiasi hcho katk tasnia ya music ...alipokuja kushtuka nakurudi dar...akakuta wenzake wapo mbali mnoo
sasa hivi amepitwa mpka nakina youngkiller
 
Kwa wasiojua Diamond na Belle 9 wote walitoka kipindi kimoja kama sijakosea mwaka 2009 hivi. Wote hawa walikuwa maunderground. Belle 9 akitokea Morogoro mji kasoro bahari pale mtaa wa Mafiga. Wengi walianza kutabiri kuwa kijana huyo mdogo ( Belle 9 ) alikuwa amekuja kujaza nafasi ya mkongwe na mwakilishi wa mziki mkoa wa Morogoro yaani Afande sele ambaye alikuwa ameanza kufifia kiutunzi na nyota pia.
Diamond yeye alitokea mkoa wa Dar es Salaam pale Tandale.

Wawili hawa wote walikuwa wadogo sana kiumri tuseme walikuwa under 20 na walitoka na ngoma kali.

Belle 9 yeye alitoka na ngoma iitwayo Sumu ya Mapenzi ngoma iliyomtambulisha vyema sana kwenye medani za mziki hapa tanzania. Ngoma hii ilikuwa imetulia ki melodi na saiti pia.
Diamond yeye alitoka na ngoma iitwae Nenda kamwambie wimbo ulomtambulisha nae pia vizuri kwenye medani za muziki hapa nchini.

Nakumbuka kipindi kile Radio Free Africa walikuwa na kipindi cha Mpambano wa wasanii ambao wanaimba mziki unaofanana na kuwashindanisha kwamashabiki walokuwa wakipiga kura kwa njia ya simu. Kipindi hiki kilikuwa pendwa sana na bora.
Siku moja walishindanishwa hawa wasanii ( Belle 9 na Diamond) na kura kutoka ngoma draw basi ilibidi mpambao huo urudiwe wiki inayofata ambapo Belle 9 alishinda alishinda kwa kishindo.

Mwaka 2010

Belle 9 alitoa ngoma nyongine iitwayo Masogange ambayo nayo pia ilikuwa kali sana na ilitikisa inchi nzima huku akijizolea umaarufu maradufu.

Diamond nae alitoa ngoma iitwayo Mbagala amabayo nayo vile vile ilitamba sana tena sana kutokana na maudhui mazuri na melodi iliyojaa ufundi. Nae pia kama ilivo kwa Belle 9 alizidi kujizolea umaarufu maradufu kwa watanzania ila hakumfikia Belle 9.

Mpaka hapa ambapo kila mmoja alikuwa ana single mbili mbili hit songs; Belle 9 alikuwa yuko juu kutokana kwamba watu wengi walikuwa wanamkubali sana yeye kutokana na kwamba ngoma zake ( Sumu ya mapenzi na Masogange) ziliweza kuwakosha nyoyo watanzania.

Baada ya muda Belle 9 aliachia ngoma nyingine iitwayo Wewe ni wangu au Wewe unanifaa ambayo pia ilimpaisha juu sana huyu kijana na wana Morogoro wakanyosha mikono wakisema kuwa sasa zile enzi za utawala wa Afande sele yule mkali wa Rhyms na Dogo Ditto wake zimeisha na sasa huyu dogo amekuwa Icon ya wana mji kasoro bahari. Dogo alitamba sana tena sana.

Diamond nae hakuwa nyuma; nae alitoa ngoa iitway Ntarejea ambayo nayo pia ilifanya viziri japo kuwa haikuifikia hiyo ya Belle 9 ( Wewe ni inanifaa)

Mpaka hapo Belle 9 alikuwa juu kweli ukimlinganisha na Diamond. Mtoto kutoka Moro alikuwa akitingisha kwa nyimbo zake hizo yaani Sumu ya mapenzi, Masogange na Wewe unanifaa. Diamond alikuwa hafui dafu hata. Hata kwenye fiesata 2010 Belle 9 alizidi kuwa kivutio sana

Si kuwa Belle 9 alikuwa akipendwa kwa hizo nyimbo tu na sauti yake bali hata sura; yeye alionekana kuwa baby face yaani handsome ukilinganisha na Dimond ambae yeye Sauti tu ndo ilikuwa ikimbeba ila kwa upanda wa sura ilikuwa shida!!! Belle 9 akivaa alikuwa akilipuka ile mbaya ila kwa mwenzangu na mimi Diamondi nguo zilikuwa zikimkataa kutokana na ukweli kwamba alikuwa na sura NGUMU!

Nakwambia kila hawa wasanii walipokuwa wakipambanishwa Belle 9 mtoto wa mji kasoro bahari alikiwa akiibuka kidedea!!

ZAMA ZA DIAMOND NA KUMPIGA GAP BELLE 9

Belle 9 baada ya kuwa na hizo hit songs na kuona kuwa yuko juu alianza kusua kusua kiutunzi huku mwenzake Diamond akikomaa na kukesha akitunga mashairi.

Diamond alituletea ngoma kama Binadamu; Kizaizai na Moyo wangu ambazo zilifanya vizuri sana hasa wimbo Moyo wangu ndo ulikuwa funga kazi. Toka hapo ndipo Diamond akaanza kuwa juu kwa umaarufu na kuwa kipenzi kwa watanzania.

Mapenzi na Mastaa Maarufu wa Bongo Movie na walembo kadhaa kumuongezea umaarufu na mashabiki


Wahenga walisema " Pesa ni sabuni ya Roho" wengine wakasema "Pesa ndo kila kitu" Mwanamziki yuhu Diamond mambo yalipoanza kumnyokea ndipo tulipoanza kusikia kuwa warembo kibao wanamnyemelea na wengine kumgombania kabisa hasa pale tu alipojizolea TUZO 3 za kili music award mwaka 2010.

Mwanzoni watu walimuwa wakimkejeli kuwa anasura mbaya; mara hooo ana mdomo mkubwa ( mrefu na mpana) na wengine kusema kila tusi walokuwa wakiliona linamfaa. Yote hayo yalisahaulika sasa kijana Diamond akaanza kushine; akaanza kutakata akapendeza mbaya. Nakumbuka kwenyevizuri kwenye video za nyimbo zake na shoo zake alikuwa akipenda kuvaa shuti na Necktie nyekundu.

Hapo sasa ndipo alipo mpata Mrembo Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu na kuwa nae kimapenzi kisha kuishi wote. Ile kufanukiwa kudate na mrembo huyo miss tanzania mwaka 2006, Diamond alipaa kwa umaarufu na kujulikana sana nchini.

Hapo ndipo magazeti ya udaku na mengineo hapa nchini yalipoanza kuwandika front pages. Kila siku Diamond alikuwa akionekana page za mbele na story zake kuzidi kusambaa.

Pia kwa umri wake mdogo na kudate na Wema Sepetu aliyeonekana kumzidi umri nayo pia ilizidi kuwa habadi mjini na nchini na hapo ilikuwa miaka ya 2011 hivi.

Diamond alipata mashabiki wengi sana kwani mashabiki wote wa Wema Sepetu ilibidi wawe pia mashabiki zake kwani walimwita shemeji. Ikumbukwe kuwa Wema Sepetu alikuwa tayari maarufu kwa kipindi cha miaka kama 5 kwa hiyo alikuwa na mashabiki lukuki.

Belle 9 nae hakukaa kimya nae alizinduka na kuja na wimbo uitwae ' Nilipe Nisepe' wimbo ambao haulufanya vizuri kama zile nyingine za awali na ulizidi kufunikwa na upepo wa nyimbo za Diamond!

Baada ya wimbo huo wa Belle 9 ulofanya vibaya ; aliamua kukaa kimya kwa muda bila ya kutoa nyimbo huku mwenzie Diamond akizidi kufanya bandika bandua ya nyimbo tena zote zikiwa hit songs kama anavyofanya sasa hivi huyu bwana Mdogo Aslay!

Diamond alizidi kuachilia ngoma kali kama ' Lala salma; Mawazo; Nimpende Nani; Ukimwona; Nataka kulewa na Kesho. Nyimbo zote hizi zilikuwa mashine na zilizidi kupasua anga hapa nchini. Ndo hapo sasa unaambia Diamond alipozidi kupata mashoo ya ukweli na ya mtonyo mnene ndani na nje ya nchi. Aliweza kupiga kolabo nyongi na wasanii kibao wa ndani na njee.

Hakuishia hapo; Nyota yake ilizidi kuwaka na kung'ara sana na alizidi kuwa na uwezo mzuri wa utungaji wa mashairi huku akiwakosha watanzania kwa sauti yake ya kipekee!

Aliachia nyimbo nyingi sana zilizotikisa hapa nchini na nje ya nchi pia kama:
  • “Mapenzi Basi”
  • “Uswazi take away remix”
  • “Nieleze”
  • “Natamani”
  • “Number One”
  • “Number One Remix” (featuring Davido)
  • “Mdogo mdogo”
  • “Bum Bum” (featuring Iyanya)
  • Lala Ukisinzia,Ntampata, Wapi,Nasema Nawe”,Nakupenda pia Nana.
  • Utanipendaga
  • Salome
  • Marry you
  • Hallelluya
  • Sikomi
  • Niache
  • N. k
MAFANIKIO YAKE. (Diamond)

July; mwaka 2016 Jarida la Forbes la nchini marekani lilitoa wasanii matajiri zaidi duniani ,Africa na kanda mbali mbali ambapo kwa upande wa Africa mashariki.

Diamond platinum aliogoza kwa kuwa na utajiri wa dollar million 4.5 ambazo ni zaidi ya bilioni 10 za kitanzania hasa baada ya kununua Nyumba yake ya south Africa.

Vitu vingine anavyomiliki ni Majumba ya kifahari Dar,Magari ya kifahari , Berber shop, Maduka ya nguo za mitindo ya kisasa na vingine Vingi.

Katika jarida hilo lilionyesha diamond akiwa anafanya wastani wa show 2 kwa wiki show 8 kwa mwezi na show 100 kwa mwaka ambapo show yake ya chini anakadiriwa kulipwa wastani wa dollar elfu 20,000 na show ya juu analipwa wastani wa dollar elfu 75,000

Mikataba yake na makampuni kama Cocacola,Vodacom na DSTV

Anamiliki lebel yake ya Wasafi Classic Baby! WBC. Ambayo kasign wasanii wengine wengi tu na lebel hiyo kuwa kivutio cha kila msanii ama chipukizi au mkongwe kupata nafasi ya kuingia ( kusajiliwa)

Jarida ilo linaonyesha pia diamond anaweza vaa vitu vyenye thamani ya dollar laki 150,000 ambazo ni zaidi ya milioni 350,000,000 za tanzania mwilini mwake kwenye shoo moja ambavyo ni Pete,cheni,viatu kofia,shati na suruali na vingine!


Nb: Kupitia Diamond; msanii nyota hapa nchini tunajifunza kuwa mafanikio huja kwa kujituma tu! Diamond ni msanii tajiri hapa Tanzania na kwa sasa ni Billionnaire. Hela zake si za kutia shaka kwani toka anaanza safari yake ya mziki tulikuwa tukiona mafanikio yake mpaka hapa alipo kwa sasa.

Mwanzo nimejaribu kuwaonesha jinsi gani alivyoanza masiaha ya kimziki pamoja na msanii mwenzie wote wakiwa ma underground nyota na baadae yeye kumzidi mwenzake mpaka hapa alipo!

Kila mtu akikazana na kupiga boot kwa kufanya kazi kwa kujtuma huku ukiwa na malengo hakika tutafanikiwa!
mkuu umechambua vizuri, aiseeh

sasa weka uchambuzi wa Diamond kumzidi Ally K



nataka ona K aliteleza wapi?

alafu uje uchambue kwa nn mr Blue yuko palepale hashuki wala hapotei,

pia uje uchambue muelekeo wa P Funk
 
Nakumbuka siku ya kwanza "nenda kamwambie" inatambulishwa Kama ngoma mpya mida ya jioni......siku hyo brother angu alinambia "huyu msanii anaimba vzuri Sana atafika mbali"" mi nikaona Kama ananipigia kelele Tu hata sikumjibu kitu.
 
Back
Top Bottom