Tukumbushane haya Majarida!..

Tukumbushane haya Majarida!..

Nyakwec's Bro

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2012
Posts
820
Reaction score
174
Nakumbuka miaka ya 90 na mwanzoni mwa 2000 kulikuwa na majarida ambayo yalikuwa gumzo mtaani kila

yakitoka,majarida haya yalikuwa yakitoka mara moja kwa mwezi.

Kulikuwa na Sani -burudisho la wasomaji,Bongo,Tabasamu,Ambha.

Leo ningependa tukumbushane vichwa vya magazeti hayo unavyovikumbuka,magazeti haya yalikuwa yakitoka yanatoka

na kichwa ambacho kinakuwa na stori inayohusiana na hicho kichwa,mimi ninakumbuka zizi;

1.Kula ni Kula Mbaya Kukomba Mboga

2.Kitanda Kilichonilea

3.No Parking Mabuzi Adimu

Pia kulikuwa na hadithi nzuri sana za michoro kukiwa na wachoraji mahili kama;

John Kaduma - Huyu ni marehem nilisikia alifariki.

Fortunatus Ndila - Sijui yuko wapi

Marco Tibasima - Huyu yupo nimemwona Fb

Tukumbushe unachokumbuka kuhusu majarida hayo na mengine ambayo inawezekana nimeyasahau.
 
Back
Top Bottom