Nitazipata wapi hizi hadithi zilizowahi kuvuma kwenye majarida?

mageta

Member
Joined
Aug 26, 2009
Posts
64
Reaction score
33
Habarini wana jamvini?

Nilikuwa msomaji mzuri sana wa majarida ya mwezi kama Bongo, Sani na Tabasamu. Ndani ya haya majarida kulikuwa na riwaya nzuri sana za kusisimua kama MUSAKO WA HAYAWANI, MSAKO WAMR X (riwaya za Eddie Ganzel, na baadae Ray Ganzel ktk jarida la Bongo), DAMU NZITO ya Amri Bawji kwny jarida la Sani.

Na hata kwenye jarida la Tabasamu kulikuwa na mtunzi maarufu wa riwayaa ajulikanae kama Emmanuel P. Ndonde alikuwa akitunga hadithiza wapelelezi maarufuakina Micky Reuben na Dick Masamba (kama sijakosea).

Hizo ni baadhi ya hadithi nazozikumbuka, zipo nyingi tu zilizowahi kutungwa na kuchapishwa kwny majarida hayo..kuna baadhi ya hadithi za michoro chini ya wachoraji maarufu kama Fortunatus Ndilla (mtaalam), John Mohamed Kaduma(R.I.P), Aloyce Jacob, Daud Masasi n.k walitunga hadithi za michoro kama, Mlinzi wa zamu, Anga za wenyewe, Hofu ya vizito, hadithi za akina mzee ole, obi, linda n.k.

Hiyo ilikuwa ni miaka ya tisini katikati mpaka alfu mbili mwanzoni, magazeti haya yalikuwa maarufu sana. Nilikuwa mdogo kipindi hicho lkn nilikuwa navizia kwa majirani walionunua nami naazima.

Kwa kipindi cha hivi karibun nimekuwa nikipita k'koo kwa wauza vitabu, majarida na magezeti kubahatisha kama wanaweza kuwa na vitabu vya hadithi hizo. Nilibahatisha kupata kimoja tu cha MSAKO WA HAYAWANI.

Je hakuna utaratibu wowote wa kuwashauri watunzi au wamiliki wa hizi hadith wakachapisha kitabu kimoja kila hadithi na kuviuza?.. Maana hadithi hizi zilikuwa nzuri sana na zenye kufundisha.
 
Kuna ile hadithi ilikuwa gazeti la bongo. George ni mpelelezi hatari. Kubwa la majamba likamtuma mrembo Vicky akajitongozeshe na kummaliza George. Vicky kamfananisha Raymond na George na kuzama penzini. Niliipenda sana.

Vitabu vingi Ulaya, hasa vya zamani vilianza kama series za magazetini.
 
Zama zimebadilika, ukizisoma leo hizo wala hautazifurahia tena kiviiiiileee!!
 
Namshukuru mamangu ni mpenzi wa kusoma vitabu, magazeti, majarida n.k huwezi amini mpaka leo hii hivyo vitabu vipo ni mtu ukijisikia kujikumbusha unaenda kwenye library yake unachukua na kuburidika, mpaka magazeti ya jitambue na mshauri wako yapo mpaka leo hii na ukiyasoma bado yana ladha taam,.kwa hakika vya kale dhahabu.

Mfano vitabu vya marehemu H.H Katalambula na watunzi wengine mashuhuri ambavyo vipo hapa:
Lawalawa, pili pilipili, najisikia kuwa tena, simu ya kifo,msako wa hayawani, hofu, aisee ni vingi mnoo
 
Kuna ile hadithi ilikuwa gazeti la bongo. George ni mpelelezi hatari. Kubwa la majamba likamtuma mrembo Vicky akajitongozeshe na kummaliza George. Vicky kamfananisha Raymond na George na kuzama penzini. Niliipenda sana.

Vitabu vingi Ulaya, hasa vya zamani vilianza kama series za magazetini.
Inaitwa Anga za Wenyewe, chini ya mtaalam Fortunatus (4T) Ndilla.. sijui yuko wapi huyu mwamba ila heshima yake popote pale alipo! Alikuwa mchoraji smart sana, baadaye akaja Abdulrahman Dohu, naye alikuwa mtata ila si kama 4T Ndilla.
 
Wamama wana nguvu sana katika kuwafanya watoto wapende kujisomea.
 
Inaitwa Anga za Wenyewe, chini ya mtaalam Fortunatus (4T) Ndilla.. sijui yuko wapi huyu mwamba ila heshima yake popote pale alipo! Alikuwa mchoraji smart sana, baadaye akaja Abdulrahman Dohu, naye alikuwa mtata ila si kama 4T Ndilla.
Nasikia alikufa huyu bwana.
 
Siku hizi watu wanafuatilia sana tamthilia kwenye TV au mitandao sio kupekua makaratasi kama zamani. Nakumbuka vitabu kama sikisei Wile Gamba Zawadi ya ushindi daaaa
 
Namshukuru mamangu ni mpenzi wa kusoma vitabu, magazeti, majarida n.k huwezi amini mpaka leo hii hivyo vitabu vipo ni mtu ukijisikia kujikumbusha unaenda kwenye library yake unachukua na kuburidika, mpaka magazeti ya jitambue na mshauri wako yapo mpaka leo hii na ukiyasoma bado yana ladha taam,.kwa hakika vya kale dhahabu.

Mfano vitabu vya marehemu H.H Katalambula na watunzi wengine mashuhuri ambavyo vipo hapa:
Lawalawa, pili pilipili, najisikia kuwa tena, simu ya kifo,msako wa hayawani, hofu, aisee ni vingi mnoo
Daah ametisha bi mkubwa hapo kwa Jitambue na mshauri wako nimemkumbuka marehemu Munga Tehenani....alale pema.
 
Habarini wana jamvini?

Nilikuwa msomaji mzuri sana wa majarida ya mwezi kama Bongo, Sani na Tabasamu. Ndani ya haya majarida kulikuwa na riwaya nzuri sana za kusisimua kama MUSAKO WA HAYAWANI, MSAKO WAMR X (riwaya za Eddie Ganzel, na baadae Ray Ganzel ktk jarida la Bongo), DAMU NZITO ya Amri Bawji kwny jarida la Sani.

Na hata kwenye jarida la Tabasamu kulikuwa na mtunzi maarufu wa riwayaa ajulikanae kama Emmanuel P. Ndonde alikuwa akitunga hadithiza wapelelezi maarufuakina Micky Reuben na Dick Masamba (kama sijakosea).

Hizo ni baadhi ya hadithi nazozikumbuka, zipo nyingi tu zilizowahi kutungwa na kuchapishwa kwny majarida hayo..kuna baadhi ya hadithi za michoro chini ya wachoraji maarufu kama Fortunatus Ndilla (mtaalam), John Mohamed Kaduma(R.I.P), Aloyce Jacob, Daud Masasi n.k walitunga hadithi za michoro kama, Mlinzi wa zamu, Anga za wenyewe, Hofu ya vizito, hadithi za akina mzee ole, obi, linda n.k.

Hiyo ilikuwa ni miaka ya tisini katikati mpaka alfu mbili mwanzoni, magazeti haya yalikuwa maarufu sana. Nilikuwa mdogo kipindi hicho lkn nilikuwa navizia kwa majirani walionunua nami naazima.

Kwa kipindi cha hivi karibun nimekuwa nikipita k'koo kwa wauza vitabu, majarida na magezeti kubahatisha kama wanaweza kuwa na vitabu vya hadithi hizo. Nilibahatisha kupata kimoja tu cha MSAKO WA HAYAWANI.

Je hakuna utaratibu wowote wa kuwashauri watunzi au wamiliki wa hizi hadith wakachapisha kitabu kimoja kila hadithi na kuviuza?.. Maana hadithi hizi zilikuwa nzuri sana na zenye kufundisha.

Magazeti zamani tulikuwa tunasoma kwenye Mabati.
 
Jitambue na mshauri yako yatunze hayo magazeti maudhui yake yataishi hata miaka 1000 mbele
 
Daah ametisha bi mkubwa hapo kwa Jitambue na mshauri wako nimemkumbuka marehemu Munga Tehenani....alale pema.
Mimi pia namkubali maza kinoma kwenye mambo ya kusoma na kutunza kumbukumbu yuko vizuri,.siku akiamua kutusimulia hadithi za hayo magazeti kwa mfano story ya kwenye jitambue ile ya "jinsi nilivyo fedheheka" utafurahi+ vinogesho vyake basi tunaenjoy kwakweli..
 
Kuna ile hadithi ilikuwa gazeti la bongo. George ni mpelelezi hatari. Kubwa la majamba likamtuma mrembo Vicky akajitongozeshe na kummaliza George. Vicky kamfananisha Raymond na George na kuzama penzini. Niliipenda sana.

Vitabu vingi Ulaya, hasa vya zamani vilianza kama series za magazetini.
Mpelelezi ni George lkn wanafanana sana na Raymond..wakawa wansmchezea mzee Jumbo..hii hadithi inaitwa ANGA ZA WENYEWE au mwendelezo wake zikiwa zimetungwa na 4T Ndilla, jarida la BONGO.
 
Namshukuru mamangu ni mpenzi wa kusoma vitabu, magazeti, majarida n.k huwezi amini mpaka leo hii hivyo vitabu vipo ni mtu ukijisikia kujikumbusha unaenda kwenye library yake unachukua na kuburidika, mpaka magazeti ya jitambue na mshauri wako yapo mpaka leo hii na ukiyasoma bado yana ladha taam,.kwa hakika vya kale dhahabu.

Mfano vitabu vya marehemu H.H Katalambula na watunzi wengine mashuhuri ambavyo vipo hapa:
Lawalawa, pili pilipili, najisikia kuwa tena, simu ya kifo,msako wa hayawani, hofu, aisee ni vingi mnoo
Huu ni utamaduni mzuri sana wa kutunza vitu vya zamani..mpe kongole kwa niaba yangu
 
Back
Top Bottom