Tukumbushane enzi hizo Wasanii wanazindua Albamu zao!!

Aisee humu nacheka.. Sikuudhuria ya Juma Nature Ugali ila nilisikia hot pots za Ugali zilitembezwa
 
Mi nakumbuka jinsi Solo Thang alivyoshindwa kuzindua album yake baada ya kutekwa na kikosi...sasa sijui alitekwa kweli ama zilikuwa kiki tu.
Album ilijulikana kama KIMA CHA CHINI (KCC)
Ni moja ya Album bora kuwahi kutokea katika Bongo Fleva.
nasikia ni kweli walimteka. jamaa ni mmoja ya wasanii bora wa hiphop kueahi kutokea Tz.
 
Umenikumbusha Ali Choki na kisa cha Farasi pale Diamond Jubilee.

Ali Choki akiwa katika ubora wa pekee katika dansi alizindua albamu yake siikumbuki jina, sasa akamua kuingia na farasi jukwaani.

Akatokea " mwehu " mmoja akaenda kumtekenya yule farasi aliyepanda Ali Choki.

Basi kilichofuata hapo ni Ali Choki kuanguka chini na toka siku hiyo akaanza kujulikana kwa jina la " Mzee wa Farasi ".

Nje ya mada:
Wangapi mnakumbuka vile viatu ( open shoes ) vilivyokuwa vinaitwa ali choki?

Point of correction. Farasi hakutekenywa, aliminywa pumb*
 
Umenikumbusha Ali Choki na kisa cha Farasi pale Diamond Jubilee.

Ali Choki akiwa katika ubora wa pekee katika dansi alizindua albamu yake siikumbuki jina, sasa akamua kuingia na farasi jukwaani.

Akatokea " mwehu " mmoja akaenda kumtekenya yule farasi aliyepanda Ali Choki.

Basi kilichofuata hapo ni Ali Choki kuanguka chini na toka siku hiyo akaanza kujulikana kwa jina la " Mzee wa Farasi ".

Nje ya mada:
Wangapi mnakumbuka vile viatu ( open shoes ) vilivyokuwa vinaitwa ali choki?
Ahahaja long time sana
 
Ila Choki kipindi kile alikuwa na vitu Fulani hivi adimu, kiki kama za wabongofleva wa leo. Nakumbuka kuna uzinduzi wa Album moja ya Twangapepeta alitokea juu ya paa, almanusura akatwe na pangaboi
 
Pia nakumbuka kuliwahi kuwa na mpambano kati ya TID vs DULLY SYKES, nadhani walikuwa wanazindua album. Hivi nani alishinda?
 
Tid na dully walizindua album kwa pamoja 2002 pale diamond jubilee, dully "historia ya kweli"hit salome huku tid "sauti ya dhahabu"hit song zeze aisee tid akawa anamepangwa apande wa mwisho dully kutangulia akapanda na style za kudance za tid yeye kuja kupanda hamna kitu tid alikasirika sana akadai alihujumiwa style zake zikaibiwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom